Nawaomba radhi niliowakwaza, CHADEMA ni chama sahihi kwa Watanzania

Hapana ni wewe ndo hujatambua athari ya siasa katika maisha yetu sitaki kutoa mifano ya
nje hapa hapa nchini wakati wabunge wa majimbo mengine wanaomba wapelekewe miradi
ya maji na barabara wa kwetu aliomba aletewe pingu za kutosha.

Pia mafanikio ya nchi nyingi yanategemea sana aina ya wanasiasa na siasa ya nchi hiyo.

Ikiwa watu wenyewe ni kama wewe, huyo mbunge wala hajakosea.
 
Wewe ungekuwa CCM ungejiunga na dhahaka zaa vijisenti?

Wewe ni kiwanda tu cha uongo.
 
Acha hasira. CDM tuko wahaya, wahehe, wasukuma, warangi nk. Ila CCM sasa akitoka baba anaingia mtoto. Hiki ni cha kifalme.

Huyu simiyu sifa zake ndo zile zimeelezwa hapo juu na Dr mo,wala usihangaike na mwehu huyu wa gamboshi
 
Habarini wana Jf,
Mimi ni binadamu kama walivyo binadamu wengine hivyo wakati mwingine huwa ninakosea
iwe kwa bahati mbaya au kwa kukusudia, mara kadhaa humu ndani nimekuwa nikiipinga Chadema humu jukwaani tena kwa kauli mbaya na za kuudhi, tena wakati mwingine nimekuwa nikijifanya kuwa mfuasi wa CUF ili kunogesha mpasuko ndani ya UPINZANI. Ukweli mimi ni mwanaCCM ambaye nina kadi yangu ya Mwanachama hai, hivyo nawaomba radhi kwa wote niliowakwaza kwa namna moja au nyingine kwani nimegundua kuwa ninachokifanya ni unafiki na si uungwana.

Nayasema hayo baada ya kufuatilia mchakato nzima wa katiba ya nchi yangu unaoendelea kwenye Bunge Maalum, nimeufuatilia mchakato kwa kina na kujiridhisha kuwa chama changu hakina watu makini, hakina nia ya dhati ya kuleta Tanzania wanayoitaka wananchi pia sio wapenda demokrasia ya kweli. Chama changu si tu hakifai kuongoza nchi bali wanastahili adhabu kwa kile wanachokifanya, hata kama nimejificha nyuma ya keyboard bado najihisi kuwa ni mtu ambaye niko katika kundi la Mataahira na watu katili, Nasema mataahira kwa sababu naamini kwa mambo yanayofanywa na baadhi ya WanaCCM wana upungufu wa akili pia ni wakatili kwa sababu kuna wale ambao wako tayari Watanganyika wateketee lakini CCM isimame, hivyo nimeamua Rasmi kuachana na Chama hiki ambacho hakina
nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo wananchi. Sababu zangu napenda kuziainisha hapa chini;

1.KUPINGA MCHAKATO WA KATIBA
Tulikuwa wa kwanza kupinga katiba mpya huku tukiona hakuna sababu ya msingi ya kuwa na mchakato huo, lakini jambo la ajabu leo tumekuwa mstari wa mbele na kuufanya mpango wa Katiba mpya kama ni sera yetu huku tukiwatuhumu wapinzani kutaka kuuharibu.

2.TABIA NDANI YA BUNGE LA KATIBA
Ni wazi kuwa tumesimama imara kutaka wapinzani washindwe kwa kila jambo ambalo halina maslahi kwa Chama hata kama jambo hilo lina maslahi kwa wanachi na wao ndio wanaolitaka.

3. HATUKO HURU
Kuwa mwanaccm ni sawa na kuwa kifungoni, huna maamuzi huru kwani maamuzi yote huwa ni ya wakubwa wa chama, mfano nzuri ni katika mfumo wa kura ya wazi na siri, wana CCM tumekuwa kituko cha mwaka kwa kile ambacho tulikisimamia kwa nguvu zote, KURA YA WAZI, tulikuwa na haja gani ya kusimamia kwa nguvu jambo kama hili kama si kutaka yale malengo tunayopanga kwenye vikao vyetu yapitishwe kwa lazima na kwamba kama kuna atakayepinga kufanya hivyo chama kitamuadhibu?
Kwanini mikataba ya muhimu inayowahusu watanzania moja kwa moja tunaifanya kwa Usiri
lakini hili dogo tu la kura tunataka liwe wazi?

3.DHULMA
Ukiwa ndani ya CCM ni wazi kuwa wewe ni dhalimu, hili ni la mwisho ambalo linaniumiza sana.
Nikiwa Dodoma nimewahi kuiona Barua ambayo ilitoka kwa katibu wa CCM wa wilaya Fulani ambao ni wakulima wazuri wa korosho ikimtaka waziri mkuu kudhibiti kikundi fulani cha umoja wa wakulima ambacho kilisababisha Bei ya korosho kuwa kubwa na hivyo kukikosesha Chama mapato na kutishia mustakabali wa chama wilayani hapo. Hii ni dhuluma ya wazi kwani nimekuwa nikijionea wazi jinsi chama kinavyojichotea fedha za wakulima kupitia mgongo wa Stakabadhi Ghalani.

Hizo ni baadhi ya sababu chache ambazo zimenishawishi kuachana na chama hiki, Mwisho niseme kuwa nimevutiwa na Wabunge wa Upinzani Hususani Chadema kutokana na Ujengaji nzuri wa hoja na kile kinachoonekana kuwa ni dhamira ya dhati ya kutaka mabadiliko ya kweli yenye manufaa kwa watanzania.

MWISHO, MUUNGWANA AKIVULIWA NGUO HUCHUTAMA, KWA HIKI KINACHOFANYWA NA CCM SASA
NI AIBU KUBWA SI TU NDANI YA TANZANIA BALI HATA KWA WALE WANAOTUTAZAMA NJE YA TANZANIA
(KURA YA SIRIWAZI!!!!) NAWAOMBENI RADHI WANACHADEMA KWA MATUSI YANGU KWENU PIA
NAWAOMBA MNIPOKEE KUNDINI.

Umeongea facts tupu, lakini kama kawaida yao Lumumba team, aka buku 7 squad watakupiga madongo, lakini kiukweli dhambi waliyoifanya wanamagamba kwa kulazimisha kura ya wazi kwenye bunge la katiba, kwa lengo moja tu la kuwadhibiti wale wanaowahisi wasaliti, ili waitupe kapuni Rasimu ya Tume ya Warioba, licha ya kutumia pesa zetu walipa kodi zaidi ya bilioni 250, na badala yake watuletee katiba mbadala ya CCM!

Kwa kweli kwa hili linalofanywa na vgogo wa CCM itabidi kila mzalendo wa kweli wa nchi hii alilaani kwa nguvu zake zote, bila kuangalia itikadi za kisiasa, kwa maana hiyo hata wanaccm wengi wa kawaida, wameungana na wanamageuzi na wanaharakati wengine kulaani vikali mchezo huu mchafu wa vigogo wa CCM ambao unaweza kuliaangamiza Taifa letu
 
pamoja na kwamba binafsi sina chama (sina kadi ya chama chochote cha siasa wala sijawahi kujiunga na chama chochote cha siasa) lakini uliyoandika hapa yanaingia akilini. Kura ya siriWAZI kwenye jambo la mustakabali wa nchi??? Naomba hansard iweke kumbukumbu vizuri ili historia isipotee.

Tangu Horace Kolimba (RIP) aseme chama kimepoteza mwelekeo, kila mwaka ukweli huu unazidi kudhihirika. Chama dume sasa kimejaa HOFU, hakiwaamini hata wabunge wake kwa sababu kimehama kutoka kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi na kimejigeuza kuwa chama cha mafisadi na wababaishaji.

Bado mengi yanakuja...tusubiri

cb
 
Nyiye wafuasi wa mbowe acheni unafiki,eti unajifanya wewe ccm.Ndio maana hii SACCOS inakufa,watu wake hawana hoja ni matusi tu.Tarehe ya mazishi inaandaliwa na kamati ya mazishi ila mazishi yatafanyika nyumbani kwa mtei.R.I.P cdm.
 
Huyu vijisenti ni mamluki mkubwa.hajawahi kuwa mwanachama wa chama chenye ridhaa ya wananchI _CCM
 
3. HATUKO HURU
Kuwa mwanaccm ni sawa na kuwa kifungoni, huna maamuzi huru kwani maamuzi yote huwa ni ya wakubwa wa chama, mfano nzuri ni katika mfumo wa kura ya wazi na siri, wana CCM tumekuwa kituko cha mwaka kwa kile ambacho tulikisimamia kwa nguvu zote, KURA YA WAZI, tulikuwa na haja gani ya kusimamia kwa nguvu jambo kama hili kama si kutaka yale malengo tunayopanga kwenye vikao vyetu yapitishwe kwa lazima na kwamba kama kuna atakayepinga kufanya hivyo chama kitamuadhibu?
Kwanini mikataba ya muhimu inayowahusu watanzania moja kwa moja tunaifanya kwa Usiri
lakini hili dogo tu la kura tunataka liwe wazi?

Hapo pananiumiza sana,CCM HAWAAMINIANI,Wazalendo waliojificha ndani CCM wangependa kupiga kura ya SIRI, lakini CCM ndo hivyo tena wamestukiwa kitu wazi usikike na usaliti wa chama ujulikane.................NI UTUMWA WA KISIASA
Mkuu ukisoma post ya Malecela jr akimtuhumu filikonjombe utaamin ukiwa ccm unakuwa mtumwa
 
UTARATIBU WA CCM ni KUTANGULIZA TUMBO LAKO MBELE WANANCHI BAADAYE .
 
Huyu vijisenti ni mamluki mkubwa.hajawahi kuwa mwanachama wa chama chenye ridhaa ya wananchI _CCM

hahaaaa! Mbona alipo kuwa anaiunga mkono ccm hukuyasema hayoo???pitia post zake za nyuma basi ili ujiridhishe kuwa ameamua kuwa muungwana mbele la taifa lake ,,ameona watanzania wanavyo pata shida ya maisha,umeme juu,hosp hakuna dawa,kinamama wana lala kitanda kimoja watatu,watoto mashuleni wanakaa chini,walimu hakuna,shule mbovu halafu ccm wanatumia pesa nyingi kuhonga kina zitto ili wahujumu juhudi za kupigania taifa ,wana husika kuua tembo kama ulivo sikia tembo mil 4 wameuliwa na majangili wa ccm, wanafuja pesa za uma kwa maslahi yao,wanatorosha pesa za taifa kwenda uswis wakati taifa linachangamoto lukuki,, kweli ccm ni wauwaji wakubwa sana hawafai kupendwa hata na alshaabab
 
Nyiye wafuasi wa mbowe acheni unafiki,eti unajifanya wewe ccm.Ndio maana hii SACCOS inakufa,watu wake hawana hoja ni matusi tu.Tarehe ya mazishi inaandaliwa na kamati ya mazishi ila mazishi yatafanyika nyumbani kwa mtei.R.I.P cdm.

huna jipya zaidi ya ushabiki wa kipuuz!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom