Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 57,243
- 90,302
Wapentekoste waliingia Tanganyika zamani sana miaka ya kati ya 1900's. Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) walianza kuwepo Tanzania mwaka 1932, hata hivyo hawakuweza kupata mafanikio makubwa mpaka miaka ya mwishoni ya 1980 na mwanzoni miaka ya 1990. Walipoanza kuingia kwa nguvu katika jamii walionekana watu wavurugaji tu na wapiga kelele hadi wakabatizwa jina la kejeli la "walokole".
Hata hivyo kadri muda ulivyoendelea waliendelea kuvuna wafuasi kutoka Katoliki, Lutheran, Anglican hadi na Uislamu, taratibu nao wakaanza kuchukuliwa kwa uzito na heshima kubwa katika jamii, mwishowe wakaweza kupenya hadi kwa watawala wa nchi na kuwa sehemu muhimu ya ushiriki wa siasa za nchi, wakapewa kipaumbele katika viti vya mbele vya nchi na hadi sasa kufikia kuwa karata turufu ya kisiasa katika nchi. Kwa safari hii ndefu na mahangaiko mikubwa sana waliyopitia ni vigumu wao kujiondoa katika karamu kutoka meza kuu kwa sasa, tuwavumilie na kuwaelewa tu, ni wakati wao wa kula nao.