Nawachukia ma DOKTA na MAPOLISI

Bora madr kwa upande wangu! Mapolisi na matrafic nikikuta wanauwawa nitachangia kupiga jiwe, nawachikia kupita maelezo, wanapenda rushwaaaaaaa, lakini wachafuuuuuu, tena hawana maisha, kutwa kutuambia kila kosa faini ni sh 30,000! Ndilo hilo tu wanalojua kusema, wanadhani tunaokota, sasa ukimuambia sina, bilka aibu utasikia leta nusu yake, sishuki zaidi ya hapo, hapo kakukamata kwedikwazu! Puuuuuuu nawatema!
 
tatizo mfumo mzima umeoza unanuka kuanzia ngazi ya juu kabisa mpaka ya chini...... Nani atamfunga paka kengele?

chini ni rahisi sana kurekebishwa kama juu kutakuwa safi. Nani anayetaka kupoteza kazi? Laiti rais asingekuwa mchafu asingekuwa anawalinda wachafu. Kila siku analalamika, kwa nini asifute takukuru na kuijenga upya? Takukuru wenyewe ukiwapa taarifa za rushwa wanampigia simu muhusika na kutibua mpango mzima. Unadhani tutaendelea?
 
Kwakweli hawa watu nawachukia sana ndani ya moyo wangu wote. Hospital ya serikali ,vitanda vya serikali, dawa za serikali + mnalipwa pesa nzuri tu . BADO MNATAKA RUSHWA TENA KWA WAGONJWA MAHUTUTI, polisi nao wamegeuza uniform zao na ofisi kuwa vijiwe vya kujipatia hela. Moyo unaniuma sana.

kwa hiyo ukiwapenda utafaidika nini!!
 
kipindi hiki cha skukuu hata kutoka ni kero kila hatua kadhaa unapigwa mkono na trafiki wanatafuta mpunga wa sikukuu......

Hospotali za serikali hususanz temeke sina hamu nayo, mgonjwa wangu alitakiwa apigwe xray nikaambiwa mbovu (hapa nailaumu serikali ya kifisadi, pesa wanakwapua wao wanatibiwa india sie tunakufa) nikaambiwa niende hospitali ya masawe kupiga, kweli alipiga kurudi nayo daktari akatuambia yupo busy sana hawezi kuisoma......... Wodini manesi wakatuibia dawa 2 na cannula 6 sina hamu nao

ukimuuliza kosa lako anatafuta akikosa anakwambia ulikuwa unaonekana kama unasinzia wakati unaendesha.
kitu gani bwan akupotezeana muda. waacha tabia hizi zisizo na msingi au anatafuta kosa akikosa anakugandisha kukuruhu hakuruhusu hasemi anachotaka yani wanaboa.
 
mfumo ndo unafanya hawa waonekane hivyo! sector yeyote inayohusuka na huduma kwa jamii lazima ionekane ina matatizo maana hata wateja wenyewe wana matatizo! wewe unasema unawachukia Madaktari! Piga ua katika maisha yako lazima utaenda hosp tu! either alive or dead! mbona ma Drs hao hao wakiwa private hosp mnawasifu!
 
nchi yakuchukiana tu, polisi na daktari nao pia wakienda kuomba viwanja kwenye halmashauri kwa ajili ya kujenga nyumba bila kitu kidogo hapati. polisi na daktari watoto wao wakipangwa shule za kata zilizombali na makazi yao wakienda wizara ya elimu kuomba watoto wao wahamishiwe shule za kata zilizokaribu bila kitu kidogo hapati,polisi na daktari wakiwa na shida mahakamani hata ya kusainiwa hati mbalimbali bila kitu kidogo hapati,polisi na daktari kuungiwa mita ya luku na tanesco bila kitu kidogo hapati na maeneo mengine mengi je? ni wao tu, wa kuwachukia? au ni wapi? tupachukie? je? chuki zetu zitasaidia? kama hazitasaidia tufanye nini?
 
Back
Top Bottom