Rais Samia, bado nalia na NHIF dhidi ya Agenda iliyopenyezwa

Megalodon

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,259
4,128
Kinachoendelea kwa sasa ni siasa za kuzima kelele kupitia magezeti na mitandao.

Nikiwa kama mtanzania, nashauri IKULU iunde SPECIAL FORCE kuchunguza malalamiko ya wananchi na uhalisia wa kitita kipya cha NHIF.

Mambo bado ni ya moto sana kwenye ground na uhalisia unakuwa covered na propaganda zinazoendeshwa na NHIF na Management ya NHIF kwa kushirikiana na viongozi wa wazira ya Afya.

Kuondoa hii bias na misleading inayoendelea against uhalisia kwenye ground, lazima kamati maalum iundwe kutoka IKULU kuchunguza uhalisia wa kitita cha NHIF na wale wote waliohusika.

Kamati ya waziri kukusanya maoni bado sio independent entity , ni kamati ambayo inakuwa influenced na bias, confounding na third part.

Msingi wa malalamiko sio tu kuondolewa kwa baadhi ya dawa lakini pia bei zilizotumika ni bei ambazo hakuna Hosp itakayoweza kutoa huduma za NHIF hata hizo za serikali endapo tutaacha siasa kwenye afya. matokeo yake Hosp za serikali zitakufa.

Kwa mfano magonjwa ya saratani na figo dawa na huduma zao ni ghali, kama dawa za saratani au figo nimenunua laki 7 kwa dose moja, NHIF anakuja kulipa hiyo dawa kwa laki 4 ndani ya kitita kipya ; je ni mazingira gani nitamuhudumia mgonjwa wa NHIF? Hapa nita deal na wagonjwa wa cash tu ili hospital isipate big loss, hiki ndio kinachotokea kwa sasa mtaani ambacho wewe Rais wa JMT labda wanakuficha. It is agenda setting chini ya baadhi ya watu .

Kama tutaendelea kulazimisha kitita kipya cha NHIF kitumike maana yake wagonjwa wengi wa NHIF watapata tabu sana na hospital nyingi zitapata hasara. Zile Hosp zote za Serikali zilizokuwa kimbelembele kusema kitita kipo sawa zimekuwa za kwanza kucheza na mifumo ili dawa zionekane out of stock hasa kwa wateja wa bima, hii ni kwa sababu hasara wanayoiona mbele yao ni ANGUKO. aidha ukienda private hospital, watakujibu huduma hii haipatikani kuna shida ya system, njoo kesho. Hii yote ni kukwepa big loss ahead .

Utengezaji wa kitita cha NHIF haukuwa shirikishi kwa wadau muhimu tangu mwanzo. Ni kama ilikuwa Agenda setting then ikatafutwa advocacy kufanya promo, blah blah za magazeti, mbaya sana.

Pia kuna viashiria vya RUSHWA kwenye hili swala, special Force kutoka IKULU iingilie kufanya special audit kutambua involvement ya kila mdau na uhalisia wa hiki kitita dhidi ya management ya NHIF pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya.

Pia timu iliyoandaa kitita kipya itambulike na kuchunguza expertism na ni vigezo gani as a minimum criteria zilizotumika kuwapata.

Special Committee ( Independent Committee) kutoka IKULU, ifike kwenye hospital zote kubwa hasa zinazotoa huduma za figo, saratani n.k ifanye survey kwa health workers wale wenyewe kabisa ili kuuona uhalisia. Hawa wavaa tai na wanaochomwa na AC muda wote wengi wao ni MANIPULATORS na lengo Lao ni kulinda vyeo vyao na wakiumwa wanakimbilia South Africa.

Hatuwezi kuleta mzaha na siasa kwenye afya za watazania kwa ajili ya maslahi ya watu wachache yenye agenda setting , tunajua watanzania wenye dhamana ni wazuri wa kusukuma kete sehemu yenye maslahi yao binafsi.

Inawezekana kabisa UONGOZI
wa NHIF na baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Afya wanatakiwa KUWAJIBISHWA kwa hii misconduct . Aidha, Hospital zinatakiwa kutoa loss report tangu implementation ya kitita kipya kuanza.
 
Hana ari wala uwezo wa utendaji wa kuchunguza hayo.

Anachoweza ni kuandaa warsha kama futari, kuhudhuria mikitano mbalimbali hususani ya nje ya nchi n.k, sio mfuatiliaji kabisa.

Omba Mungu 2025 apumzike.
 
Hana ari wala uwezo wa utendaji wa kuchunguza hayo.

Anachoweza ni kuandaa warsha kama futari, kuhudhuria mikitano mbalimbali hususani ya nje ya nchi n.k, sio mfuatiliaji kabisa.

Omba Mungu 2025 apumzike.

ulimsikia Makamba alivosema. 2025 FORM ni moja tu.

Na yeye anayapenda madaraka. Hawezi kupumzika
 
Back
Top Bottom