Nawaamasisha Watanzania tuandamane kupinga Ujenzi wa Bandari Bagamoyo

Nebuchadinezzer

JF-Expert Member
Oct 1, 2018
1,403
2,545
Ndugu zangu watanzania,

Hii nchi sio ya Ndugai wala Wabunge, hii nchi ni yetu sote sisi na watoto wetu.

Kumbukeni hatuna sehemu duniani ila hapa Tanzania.

Huu ujenzi wa bandari hii ni kujifunga na kuuza nchi yetu kwa mataifa mengine. Hebu fikirieni kuna nchi mpaka sasa zimekabwa mashirika yao kama fidia ya mikopo mikubwa waliokopa.

Sisi hatutaki kwenda huko...tumeoneshwa njia hebu tuifate. Mifano ipo mingi sana angalia nchi ya Zambia, na SriLanka wanachopotia sasa.

Tuandamaneni mitandaoni na kwa wajasiri tuingie hata barabarani kupinga kuuzwa kwa aridhi yetu kinyemela.

Maandamano yawe ya amani tusivuruge tunu ya amani.

Niwatakie siku njema wazalendo wote.
 
Si busara kwani mkataba uwekwe wazi Kwanza ndio tuone umuhimu wa kufanya hivyo
 
Kwa maelezo madogo tu niliyosikia mpk nikapata wasiwasi na hiyo bandari! Tunahitaji majasusi wa kiuchumi walahi
 
Ndugu zangu watanzania,
Hii nchi sio ya Ndugai wala Wabunge, hii nchi ni yetu sote sisi na watoto wetu...
Si ndio nyie mlikuwa mkikejeli maandamano ya vikundi vingine (eg wapinzani) na kusema kuwa huu ni wakati wa kuchapa kazi na sio kuandamana?

Hahahahaha... kweli muda ni mwalimu mzuri sana. Leo hii Mataga nao wanataka kuandamana.
 
Back
Top Bottom