Nauza Samaki aina ya Jodari

Nauza Samaki aina ya Jodari

Sijakuelewa

Wabaya kivipi ?
Sehewa sio samaki wa kula aisee

Sehewa ni hao samaki ambao wako kwenye picha

Sehewa sio jodari

Ubaya wake wakilala siku moja kama umewatunza kwenye fridge ukiwala wanawasha saana mdomoni hata ukuwakaanga ukawatunza bado wanawasha


Sehewa sio samaki wa kula tunakula sababu ya shida
 
Jodari akiwa hivyo basi labda ni Jodari mtoto, lile samaki kubwa haswa, huwezi kuta mdogo kiasi hicho
 
Hebu achaneni na stori za yupi mtamu zaidi; mention the health benefits of each! Tuzingatie faida za kiafya zaidi kuliko utamu wa mdomoni.
Sio kila kitu kinaliwa kwa ajili ya afya. Vingine tunakula kwa kuwa ni vitamu, mfano chipsi yai
 
Jodari na sehewa ni tafauti ingawa wanafanana umbo. Aliyepewa hadhi kubwa ni jodari.
Kanadi hafanani na jodari wala sehewa. Anafanana na nguru.
Dar watu wanauziwa sehewa na kuambiwa ni jodari na wanauziwa kanadi na kuambiwa ni nguru.
Ni sawa na Ngisi na Dome, wanaufanano flani hivi, kwa wavuvi na walioshio pwani ya bahari ndio wanaweza kuwatofautisha. ila dar watu wanauziwa Dome wanaambiwa ni ngisi
 
Wakuu habari

Nina aina hii ya samaki Jodari wadogo.. Ni samaki mwenye stake nyingi kuliko miba.. Ni mzuri na ni mtam sana.

Kama upo hapa Dar, nakuletea mpka ulipo , gharama za usafiri inategemea mahali ulipo.

Bei ni 12000 tu, kwa mmoja

0616274277.

Napatikana Kigamboni

View attachment 3353575View attachment 3353576View attachment 3353577View attachment 3353578
Wenzako wengi wanauza samaki wabichi kwa kipimo cha kilo! Inakuwaje wewe unauza mmoja mmoja kwa elfu 12?
 
Back
Top Bottom