Nauona mwisho wa Rais Magufuli

Nauona mwisho wa Rais Magufuli

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,577
Reaction score
14,338
Wanabodi salaam.

Enzi zake Colonel Muammar Ghadafi alitamba , Ghadafi aliogopeka na alitisha hasaa hususan miongoni mwa raia aliokuwa akiwaongoza.

Mataifa ya magharibu yalijaribu mara kadhaa kumtikisa Colonel lakini yaliambulia patupu maana Walibya walimkubali kiongozi wao.

Lakini punde tu America na nchi nyingine za Ulaya zilipofanikiwa kuchochea mgogoro kutokea ndani ya Libya miongoni mwa Walibya wenyewe Ghadafi hakuweza kuchukua raundi na hivyo mapema sana alifurushwa madarakani.

Mwanzoni mwa mtafaruku ulioanzishwa na Walivya vibaraka Colonel alidhani shughuli ni nyepesi na hivyo akang'aka na kutoa vitisho vikubwa . Ghadafi alisema Libya itawaka moto na atateketeza kila mpinzani. Hali haikuwa hivyo bali aliteketea yeye. " im very sorry for him.

Lakini pia kuna nchi ya Iran na Korea Kaskazini. Nchi hizi viongozi wake wamefanikiwa kudhibiti upinzani ndani ya nchi na hivyo kupelekea Wairan kuwa wamoja na imara mbele ya vitisho vya USA. hali kadhalika Wakorea pia na hali hii ndio hasa inayowafanya Wamarekani kutoingia Iran na Korea maana wanajua hali haitakuwa nyepesi.

Back to Magufuli:
Tangu aingie madarakani JPM amekuwa akijaribu jaribu kutikisa kiberiti mara kadhaa kuona kama anaweza kuongoza nchi kwa mkono wa chuma. Amewawageuza wapinzani kama chapati na hawajaweza kumfanya lolote na hii ni kwa vile tu hawa watu hawako organized na ni waoga kuliko hata wanavyomuona JPM ni muoga, Namaanisha wapinzani nchi hii ni waoga kuliko hata JPM. Na kukosekana kwa umoja baina yao ndio kete muhimu ambayo JPM na serikali yake wameitumia kuwasambaratisha. Mathalani hakuna uhusiano wa uhakika baina ya viongozi wa upinzani na ukaribu wao umekaa kinafiki zaidi.

Ghafla na shahiri imeonekana JPM tayari ana upinzani mkubwa kutokea ndani ya CCM yenyewe. Hii ndio hatari kubwa iliyowaondoa Ghadafi, Sadam Hussein na hata Idd Amin Dada. Hakuna upinzani mgumu kuushinda kama upinzani wa ndani maana hutoa fursa kwa maadui wa nje kupata nguvu zaidi na kwa hakika mwisho wa Magufuli ndio huu huu labda itokee muujiza tu.

Mwl. Nyerere alipata kusema kwamba upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM.

Nawasilisha.
 
Unaposema wapinzani ni waoga kuliko hata huyo una maana gani.

Je wewe uko kundi lipi ,ni mpinzani wa ndani au?

Wewe umefanya nini kupambana na huyo unayesema anawageuza wapinzani kama chapati.

Unasema wapinzani ni waoga, hebu tuambie wewe ambaye ni jasiri ungefanya nini ili kupambana na JPM?

Nasubiri majibu yako.
 
Unaposema wapinzani ni waoga kuliko hata huyo una maana gani.

Je wewe uko kundi lipi ,ni mpinzani wa ndani au?

Wewe umefanya nini kupambana na huyo unayesema anawageuza wapinzani kama chapati.

Unasema wapinzani ni waoga, hebu tuambie wewe ambaye ni jasiri ungefanya nini ili kupambana na JPM?

Nasubiri majibu yako.
Wapinzani hawapaswi kupambana na JPM direct bali wanapaswa kupambania haki zao zilizomo kwenye katiba. mfano walitaka kuandamana kupinga walichokiita udikteta je waliishia wapi?

Wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi wanaichezea na kuinajisi demokrasia mchana kweupe je wapinzani wamefanya lolote seriously kushughulikia hilo?
 
Wapinzani hawapaswi kupambana na JPM direct bali wanapaswa kupambania haki zao zilizomo kwenye katiba. mfano walitaka kuandamana kupinga walichokiita udikteta je waliishia wapi?

Wasimamizi wa majimbo ya uchaguzi wanaichezea na kuinajisi demokrasia mchana kweupe je wapinzani wamefanya lolote seriously kushughulikia hilo?
Bado tuna safari ndefu, unajua maana ya katiba!? Unadhani ni jukumu la wapinzani ama wenye mawazo mbadala pekee kudai na kusimamia katiba!? Unajua Rais,wabunge na viongozi wakuu kwanini huapa kulinda na kuheshimu katiba!? Ni wajibu wetu Watanzania kudai maboresho na kulinda katiba yetu.
 
😀😀😀
nchi yetu haijafika huko aisee, Libya jeshi lilikua linapambana na wananchi kisha waasi wenye dhana za kivita, hapa kwetu hali ni mbaya kuliko awamu ya 3 na 4 lakini haijafikia huko, JPM atamaliza mwaka wake mmoja aliobakiza kwa amani kisha chama na wananchi kwa ujumla tutamfanyia tathmini 2020, kama amefanya vema tutampa mingine mitano ya MWISHO!
 
Upinzani wa sasa wa hovyo kuwahi kutokea toka nchi ipate uhuru.
 
CCM ina kawaida ya kutingisha Ma Rais wake ili wajirekebishe, hivyo msidhan ni mwisho wa Rais Magufuli au wa Ccm

Kwa watoto wadogo ngoja kidogo tuwape Historia ya Ccm na Wazee wastaafu wa Ccm

Wazee wastaafu wakiona mambo hayaendi sawia ndio hujitokeza kwa namna tofauti

1984, Hayati Sheikh Thabeet Kombo Katibu Mkuu mstaafu wa ASP aliokoa Jahazi kwny Siasa za Znz baada ya Mkwamo ule na hata Jina la Rais Ally Hassan Mwinyi kupendekezwa kuwa Rais wa Znz lilitoka kwa huyu Mzee

1993 Wakati wa Mkwamo wa Kisiasa kuhusu Serikal tatu , Mzee Mstaafu Julius Nyerere ndio aliokoa jahazi wakati huo tayari mpaka Bunge limeshapitisha Azimio la kuvunja muungano kwa kuruhusu Serikal 3

1997 Katibu mkuu mstaafu aliingilia Kati kuhusu mchakato usio Mwema wa Chama kuporwa na Mabwanyeye akikaripia Kuwa Chama kinakosa dira na Mwelekeo lakin bahati mbaya akafia kwny Kikao cha Kamati kuu Dodoma akiwa kwny mjadala

2005-2015 Wazee wa Kigoda cha Mel Nyerere hawakuchoka kukosoa mapungufu ya Kiuongozi hali ambayo ilimsaidia Rais wa wakati huo kuachana na Rafiki zake wa Miaka yote

2019 kama kawaida Wazee wamejitokeza tena kumsaidia Rais aweze kutambua Vibaraka wanaojifanya wana mapenzi Mema na Rais


Tunaposema Wazee ni Hazina yetu tuna maanisha

Mnaotegemea watu kugawana mbao endeleeni kusuburi kwa kuwa Subira siku hizi yavuta Bhangi
 
Back
Top Bottom