Vladimir Lenin
JF-Expert Member
- Jul 21, 2018
- 3,613
- 5,139
Shujaa wako na ukoo wako, hilo neno wetu ondoa tafadhali.Huu uzi siyo wa nabii wala mtume isipokua ndiyo hawa walipanga mabaya dhidi ya shujaa wetu JPM

Kwishnei!Wanabodi salaam.
Enzi zake Colonel Muammar Ghadafi alitamba , Ghadafi aliogopeka na alitisha hasaa hususan miongoni mwa raia aliokuwa akiwaongoza.
Mataifa ya magharibu yalijaribu mara kadhaa kumtikisa Colonel lakini yaliambulia patupu maana Walibya walimkubali kiongozi wao.
Lakini punde tu America na nchi nyingine za Ulaya zilipofanikiwa kuchochea mgogoro kutokea ndani ya Libya miongoni mwa Walibya wenyewe Ghadafi hakuweza kuchukua raundi na hivyo mapema sana alifurushwa madarakani.
Mwanzoni mwa mtafaruku ulioanzishwa na Walivya vibaraka Colonel alidhani shughuli ni nyepesi na hivyo akang'aka na kutoa vitisho vikubwa . Ghadafi alisema Libya itawaka moto na atateketeza kila mpinzani. Hali haikuwa hivyo bali aliteketea yeye. " im very sorry for him.
Lakini pia kuna nchi ya Iran na Korea Kaskazini. Nchi hizi viongozi wake wamefanikiwa kudhibiti upinzani ndani ya nchi na hivyo kupelekea Wairan kuwa wamoja na imara mbele ya vitisho vya USA. hali kadhalika Wakorea pia na hali hii ndio hasa inayowafanya Wamarekani kutoingia Iran na Korea maana wanajua hali haitakuwa nyepesi.
Back to Magufuli:
Tangu aingie madarakani JPM amekuwa akijaribu jaribu kutikisa kiberiti mara kadhaa kuona kama anaweza kuongoza nchi kwa mkono wa chuma. Amewawageuza wapinzani kama chapati na hawajaweza kumfanya lolote na hii ni kwa vile tu hawa watu hawako organized na ni waoga kuliko hata wanavyomuona JPM ni muoga, Namaanisha wapinzani nchi hii ni waoga kuliko hata JPM. Na kukosekana kwa umoja baina yao ndio kete muhimu ambayo JPM na serikali yake wameitumia kuwasambaratisha. Mathalani hakuna uhusiano wa uhakika baina ya viongozi wa upinzani na ukaribu wao umekaa kinafiki zaidi.
Ghafla na shahiri imeonekana JPM tayari ana upinzani mkubwa kutokea ndani ya CCM yenyewe. Hii ndio hatari kubwa iliyowaondoa Ghadafi, Sadam Hussein na hata Idd Amin Dada. Hakuna upinzani mgumu kuushinda kama upinzani wa ndani maana hutoa fursa kwa maadui wa nje kupata nguvu zaidi na kwa hakika mwisho wa Magufuli ndio huu huu labda itokee muujiza tu.
Mwl. Nyerere alipata kusema kwamba upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM.
Nawasilisha.
I am very very sorry,nime-misquote.Nisamehe.Mkuu wapi umeona nimefurahia ?
Vipi mwisho umeuona?Wanabodi salaam.