Naumia sana Mtu wangu wa karibu akifanikiwa, inanidhoofisha mwili

kikoozi

JF-Expert Member
Jun 24, 2015
2,030
2,930
Habari za asubuhi hii wakuu, poleni na majukumu ya hapa na pale.

Nina shida kidogo inanikabili ndugu zangu, tangu nilipokuwa na umri wa miaka 15 kuna hali ndani yangu ambayo sio ya kawaida, iliyonipelekea kuwa na kama ugonjwa wa kudhoofika mwili wangu na akili.

Nina umri wa miaka 38, nina elimu nzuri tu ya degree ya kwanza katika mambo ya utawala. Kwa sasa napitia katika hali ngumu sana ya kiuchumi, tangu nimalize chuo sijawahi kupata kazi katika maisha yangu.

Tangu nikiwa na umri wa miaka 15 ikitokea mwenzangu akifanikiwa roho inaniuma sana. Yaani roho inaniuma mpaka kuna muda nashindwa kula kabisa, ile hali inapelekea kuona kwanini nisifanikiwe mimi kwanini awe huyo mtu?

Ndugu zangu tangu miaka 15 mpaka sasahivi 38 hiyo hali inaniumiza sana, nimepoteza marafiki wengi sana. Nikiona amefanikiwa tu halafu mimi bado nipo hapa hapa nilipo leo basi na namba yake ya simu nafuta na sitaki tena urafiki maana roho inakuwa inanifukuta na kuona mbona mimi nafaa kukaa katika hiyo nafasi, kwanini huyo ndio akae hapo?

Mfano rafiki yangu anaweza kuja kunieleza jambo lake ambalo lipo katika njia ya kufanikiwa, najikuta naumia ndani kwa ndani huku nikimuomba Mungu jambo hilo lifeli (lisifanikiwe) kabisa kwa huyo mtu na ikitokea amefanikiwa basi nakuwa sipo katika hali nzuri.

Rafiki yangu akija kunieleza jambo lake ambalo ni la shida au amepata matatizo fulani kazini au sehemu nyingine, basi roho yangu huwa kama na furaha na ahueni tena nikimuona mtu huyo nimemzidi hata mavazi nakuwa na furaha sana.

Juzi tulienda kufanya mitihani ya utumishi pale DUCE mimi na rafiki yangu mmoja hivi, sasa kwa bahati mbaya mimi sikufanikiwa na yule rafiki yangu akapata nafasi ya ile kazi. Akaja kuniambia malengo yake baada ya hiyo kazi, akasema anataka kwanza avute usafiri wa kutembelea nikajikuta naishiwa nguvu kabisa huku mapigo ya moyo yakienda kasi na kuhisi napoteza fahamu kabisa. Roho iliniuma sana sana sana, nikatamani niende ofisini kwake nikawaambie huyo mtu mliyemchagua hafai kabisa, mfukuzeni.

Kuna rafiki yangu fulani aliniambia kuwa ana mpango wa kuacha kazi afanye biashara, akaniomba nimpe wazo la biashara, nikamuambia anipe muda kidogo. Nikaanza kufanya utafiti kuhusu biashara ambayo ni mbaya sana ambayo mtu akiingia tu huko basi afilisike kabisaaa na achakae vibaya mnooo. Nikapata wazo la biashara ya network marketing basi nikamuunganisha uko, akaingia akaanza hizo biashara pamoja na forex, akaanza uza vitu vyake ili awekeze huko, akaanza kufilisika kidogokidogo, mpaka akaja kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa anakaa, hali ilikuwa mbaya sana kwake, mimi moyo wangu ulikuwa na amani tele.

Wakuu hii hali inanitesa sana, mpaka nimeamua kuleta hapa inaniumiza sana, mwezi uliopita nilipata kazi sehemu flani ambayo sio fani niliosomea mshahara ulikuwa ni wa kawaida sana nilisaini mkataba wa malipo, sasa week ya kwanza kazini kuna mfanyakazi moja wakati tunapiga story za hapa na pale akaniambia "kaka unajua nafanya kazi ila mshahara naona hautoshi kabisa", nikamuuliza kwani unalipwa sh ngapi akaniambia analipwa pesa ndogo tu, kumbe analipwa kubwa zaidi ya kwangu, mimi nilisaini mkataba wa laki 4 na nusu, yeye analipwa milion 1 na laki 2, nilijikuta roho imeniuma vibaya mnoo nikajikaza tu, nikaanza kumshawishi kama ana akiba afanye biashara aachane na ile kazi huku roho ikiniambia aondoke ili mimi nikamate ile nafasi pale kazini.

Nilijaribu sana kumsisitiza aache ile kazi akafanye biashara ya kulima tangawizi, niamuambia tangazawizi na vitunguu vinalipa sana. Kiukweli kabisa mwisho wa siku yule kaka alianza kuhisi nafanya jitihada aache kazi, maana nilikuwa naongea na boss namuambia utakaaje na mfanyakazi haridhiki na mshahara wa milion 1.2, boss akaenda kumuambia yule jamaa akaniona mimi mmbea na mnafiki, basi nahisi waanza kuniwekea fitina za kunitoa kazini, yule boss siku iyo kaniita akasema anaona kama sifai kuendelea na mkataba katika kampuni yao kwahiyo anihitaji tena, nilidumu kwenye ile ofisi siku 19 tu (week 2 na siku 5) nikafukuzwa, mpaka naleta hapa kwenu nimepitia mengi san

Kwa kifupi nikiona mtu wangu wa karibu kafanikiwa iwe ni ndugu, jamaa au rafiki basi roho yangu huwa kama inataka kutoka hivi kwa maumivu makali sana.

Ndio hali inayonikabili ndugu zangu, sijui nafanyaje niache, ushauri wenu wakuu.
 
Hiyo ni roho ya kwa nini,ni mbaya sana...kuna mawili yanaweza kukutokea usipojifunza kukubali na kuwaunga mkono wenzako wanaofanikiwa...udhoofike na ufe kabisa,au uwe mchawi uroge wenzako.

Funga uombe MUNGU akuondolee hilo tatizo.
Shukrani mkuu.
 
Aisee kwanza pole sana wivu kila mtu anao,
Ila mwenzako akifanikiwa usifikie hatua ya kumuwazia vibaya sana unafunga riziki zako mwenyewe, hebu jaribu kwenda kanisani hii yote ni sababu unakaa mbali na Mungu..
 
Tiba ya huu ugonjwa ninayo; sijui nitakupataje! Utapona kabisa na ndiyo chanzo cha mafanikio yako yalipo! Karibu nikupatie dozi
 
shukrani kaka, nilidhani ni tatizo mkuu.
Boss.....

Usijifariji, hilo ni tatizo tena kubwa sana huwezi kuniombea mabaya mimi ukadhani wewe utabaki salama coz mara nyingi binadamu huwa tunainuana tu-assume huyo uliyemfifisha mpaka akafukuzwa kwenye nyumba ya kupanga ungempa wazo zuri la biashara huoni kama angeweza kuwa na uhitaji wa msaidizi nafsi yake ikakupendekeza wewe akakupa kitengo ukaondokana na kuzura mitaani bila ishu?

Pia nahisi Kiimani wewe ni mfu kabisa, hiyo siyo hali ya kawaida kwa mtu mwenye hofu ya Mungu nakushauri badilika hao hao unaowaombea mabaya inaweza kuwa ridhiki yako imepangwa ipitie kwao so anza sasa kuwajali na kujiweka nao karibu huku ukiwapa ushauri sahihi kama watahitaji!
 
Back
Top Bottom