Naumia sana kubaguliwa na wazungu kila wakati

Wadada hawabagui sana, maana wanaujua mziki wetu, wadada wabaguzi wapo Italy , lakin wadada wa Urusi wapo after money hata uwe mbwa ilimradi anahisi atabenefit kitu kwako haeez kukuonesha,

Kuna watu wanatangaza nyumba za kupanga au hotel ana spesfy kwamba for Italian, au Kabayan only (wafilipino) saa nyingine mnaweza ongea na mtu Kwa simu akigundua ni Niga anakublock bila sababu
Duuuuh hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
" wazungu Wazuri " unamaanisha nini ? . Hivi unajua jinsi majimbo ya kusini kama kentucky , Texas , Oklahoma , Virginia , Tennessee n.k .Ndo kuna maconcord ya ubaguzi . Huko kuna wazungu wanaitwa rednecks . Hata rafudhi yao ni tofauti na whites wa northern states kama Newyork n.k.

Wengi wa majimbo ya huko kusini ndo walimpigia kura Trump . Na ndio wengi wao ni illiterates na masikini . Hao bado wanaresentment kubwa na black skinned individuals kutokana na mentality waliyokuzwa nayo ya kuamini mtu mweusi ni mtumwa . Ndio maana waliwahi kuwa na vita kubwa juu ya hilo , north states ( union ) vs southern states ( confederates ) . Mwisho wa siku south walikuwa defeated

Ndio mdogo wangu, nalijua hilo tatizo la Down South. Huko ndio ovyo kabisa. Na kuhusu kumpigia kura Trump, sio tu Rednecks, hata wale wanao jifanya wanapenda diversity walimpigia kura Trump. Afadhali Rednecks wapo wazi na ubaguzi, wabaya ni wale wa Wall street wanao jifanya ni marafiki zako, kumbe behind you...hao ndio walio msapoti Trump akapita.
 
Hahahahaa umetisha mzeiyaaa
Wakihama kqenye sit we lala kabisa au kama unakitabu jisomeee mpaka mwisho wa safari.

Halafu siku nyingine unategeneza false book cover tena kubwa ambayo imeandikwa
your first mother was
a
White Chimpanzee
volume 1.
halafu unakifunua mwanzo mwisho wa safari ili kila aliye kupisha apate ujumbe huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mara nyingi sana mtu unabaguliwa lakini basi tu. Yaani unapanda treni ya mwendo kasi ukikaa kwenye siti wanahama wote. Nimejisikia vibaya sana aisee.

Ni zaid ya kunyanyapaliwa
Mind your own business .Wakihama sawa Ni haki yao ya kidemokrasia kukaa seat yeyote
 
Mabeberu ni wapuuzi

Endeleeni kuwanyenyekea msiojitambua
Kwani Lazima wakae na Wewe kiti kimoja? Nilikuwa ujerumani siku moja Niko kwenye ndege nimekaa na wajerumani wawili wakamwita mhudumu kuwa awahamishe wakakae siti zingine hawataki kukaa na Mimi walikuwa wakiongea kwa sauti kwa kiingereza.Mhudumu akaja akawa ananiomba samahani kwa kubaguliwa akasema ile sio policy ya shirika lao

Nikamwambia Wala usijipe shida mtu Yuko huru kukaa popote Ni haki yake nikamwambia Niko ok sio lazima wakae karibu na mimi.Na Mimi nikiona hii seat siko comforatable nitakuomba ruksa nikakae seat nyingine it is not a big deal
 
Bad enough wabongo wanawashobokea sana hizi ngozi nyeupe. Ukienda moshi utashuhudia hili.
 
Pole wapuuzie tu, japo Nina maswali mengi ya kuuliza kuhusu nchi hizo za ughaibuni
 
Waambie wewe ni ndugu yake Lisu labda watakuelewa.
Wakikomaa wambie wewe ni UFO's halafu wakazie macho usipepese
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom