Nauliza kiasi kilichopatikana baada ya michango yetu pale Chadema Square (Jangwani)

CULCULUS

JF-Expert Member
Nov 17, 2011
316
619
Mkuu wangu Tumaini Makene (Afisa Habari wa CHADEMA) na John Mnyika (Mkurugenzi wa Habari na uenezi) pamoja na makanda wengine ndani ya CDM mimi ni miongoni mwa wadau tuliohudhuria ule mkutano wetu mkubwa pale CHADEMA Square a.k.a Jangwani na ni mmoja kati ya tuliochangia pesa za ili ziwapeleka makamanda Lindi na Mtwara kwa ajili ya kupeleka ukombozi wa fikra.

Nauliza tu ni kiasi gani kilipatikana maana imechukua muda taarifa rasmi kutolewa.
 
Mkuu CULCULUS kama unavyojua team nzima baada ya jangwani waliondoka kuelekea kusini subiri wamalize mission ya huko wakirudi watatuambia . tusikurupuke kama magamba kwasababu nafikiri hata hela yenyewe hakutosha hata robo ya siku wanazokaa huko kusini unataka kuwapa Rejao na Ritz mahali pa kusemea kwasababu kila thread kwao inawaka moto
 
Mkuu una haraka sana!
La muhimu ni kwamba tumewawezesha kufika huko Mtwara, Lindi na kwengineko. Kama wasingeenda huko tulikowatuma tungehoji kwanini, kwani tulichanga kiasi gani, nini imepelea.

By the way, una haki ya kujua mapato na matumizi ya chama chako.
Ninavyodhani, ni kwamba michango yetu ni sehemu tu ya kufanikisha harakati za M4C.
 
Mkuu wangu Tumaini Makene (Afisa Habari wa CHADEMA) na John Mnyika (Mkurugenzi wa Habari na uenezi) pamoja na makanda wengine ndani ya CDM mimi ni miongoni mwa wadau tuliohudhuria ule mkutano wetu mkubwa pale CHADEMA Square a.k.a Jangwani na ni mmoja kati ya tuliochangia pesa za ili ziwapeleka makamanda Lindi na Mtwara kwa ajili ya kupeleka ukombozi wa fikra.

Nauliza tu ni kiasi gani kilipatikana maana imechukua muda taarifa rasmi kutolewa.

Nenda makao makuu ya chama pale kinondoni.
 
CULCULUS,
Ngoja nimpigie simu Mbowe nikupe jibu Kaka.

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com
 
Last edited by a moderator:
Inawezekana Calculas ni gamba kimtindo ameamua kuleta timbwili kiaina. Kuwa na imani na viongozi wenu, wamesema watakwenda Mtwara wamekwenda na bado wapo na kazi inaonekana unataka nini sasa? Kama ulichangia sana labda elfu kumi kama ni sadaka.

Mara kumi ungeuliza mapato ya M- Pesa.
 
Kaka ni haraka sana embu piga gharama za mafuta kutoka dar hadi mtwara halafu fikiria mda waliokaa huko na kazi wanazozifanya je kwa mchango wa siku ile zinaweza zikawa zimetosha?maana wamegawana wilaya,kata na mitaa hivyo hawawezi kula sehemu moja,kulala sehem moja kutumia usafiri mmoja, ila una haki ya kuhoji mapato na matumizi ya chama chako, hongera kwa kutaka kujua mwenendo wa chama chako
 
Bado wahusika wanaendelea kuhesabu. Kwa umati ule wa watu unadhani miamia na hamsihamsini utahesabu kwa siku mbili? Tatizo coin zilikuwa nyingi kuliko noti. Hadi watoto walitupia chenji zao za kuendea video.
 
Mambo mengine ni siri ya chama sio kila kitu mpaka mfahamishwe...au umetumwa kuja kukichafua chama.
 
Mambo mengine ni siri ya chama sio kila kitu mpaka mfahamishwe...au umetumwa kuja kukichafua chama.

Ha ha haaah, sikuwa na mpango wa kucheka leo, ila duh! Nasikia tetesi eti wewe ndiye uliyesoma dua ya kislamu pale m4c Jangwani?
 
CULCULUS,
Ngoja nimpigie simu Mbowe nikupe jibu Kaka.

TUMBIRI (PhD, Hull University - UK),
tumbiri@jamiiforums.com

Aisee! Kwa hiyo wafuasi wote wa Chadema wakitaka kujua michango yao wanayotoa mpaka wapitie kwako kisha wewe upige simu kwa Mbowe, mbona kwenye kuomba michango wanakuja kwetu.
 
Last edited by a moderator:
Sadaka unayotoa msikitini/kanisani unahoji imetumikaje?inawezekana ni lazima kujua kilicho patikana lakini si muhimu. Kwani kazi wanayofanya Viongozi wetu tunaiona.
 
Hapa hoja siyo ugamba au vinginevyo. kama tunazungumzia dhana ya uwazi na maadili mazuri ndani ya chama yenye lengo la kuuaminisha umma wa Tanzania kuwa chadema ni chama makini ambacho kinafaa kuaminiwa na kupewa dhamana ya kuongoza taifa siku za usoni, hoja ya kueleza kiasi cha fedha kinachopatikana baada ya kufanyika harambee za chapchap haikwepeki. Hata makanisani kiasi cha zaka zinazokusanywa hutangazwa. Natumaini hili ni zoezi dogo tu kwa uongozi wa chadema, halitawashinda.
 
Back
Top Bottom