Nauliza kiasi kilichopatikana baada ya michango yetu pale Chadema Square (Jangwani)

Mambo mengine ni siri ya chama sio kila kitu mpaka mfahamishwe...au umetumwa kuja kukichafua chama.

mkubwa!...hivi ni wewe kweli ninae kujua hapa jamvini!hizi busara umetoa wap?au ndo kuanza kuvua gamba taratibu na kuva gwanda?....labda nimekufananisha nini?
 
Mkuu wangu Tumaini Makene (Afisa Habari wa CHADEMA) na John Mnyika (Mkurugenzi wa Habari na uenezi) pamoja na makanda wengine ndani ya CDM mimi ni miongoni mwa wadau tuliohudhuria ule mkutano wetu mkubwa pale CHADEMA Square a.k.a Jangwani na ni mmoja kati ya tuliochangia pesa za ili ziwapeleka makamanda Lindi na Mtwara kwa ajili ya kupeleka ukombozi wa fikra.

Nauliza tu ni kiasi gani kilipatikana maana imechukua muda taarifa rasmi kutolewa.

je ulishikiwa bastola kwamba ni lazima utoe mchango? jibu ni hapana, basi tunakushukuru endele na moyo huo sababu bado tunahitaji mchango wako, kama utapenda, hulazimishwi, ila na wasiwasi unaweza kufunguka kwa hili ulitoa kiasi gani? na wasiwasi kwa kifupi taarifa rasmi ni kwamba makamanda wanaendelea huko lindi na mtwara, taarifa hiyo inakutosha tena hatuhitaji taarifa yoyote kwamba kiasi gani kilipatikana, tunachohitaji ni mabadiliko ya utawala ambalo ni muhimu kuliko hiyo taarifa unayoitaka
 
Naanza kwa kujitanabaisha kwamba mimi ni mwanachadema tena hai na ni diwani mtarajiwa.. Ninakipenda chama changu tena sana, ninapenda mifumo yake ya kiuongozi. Lakini ninawachukia baadhi ya wanachama wa CDM waliopo JF.. Na hawa ndio wanakizorotesha chama na kuwapa magamba la kusema, wao wanadhanqg ndio wanakijenga.. Mbaya zaidi wengi wanajidadavua kama wasomi, but very shallow in arguing.. They responds to technical question like the above by using personal emotions not with facts and logic (this applies to some and not all)

Mtoa mada ameuliza kiasi kilichopitikana, hakukuwa na haja ya kumshambulia au kumwita gamba, wakati the question is obvious and straight.. Shughuli yoyote inayohusisha fedha kutoka mifukoni mwa watu usio na ubini nao inapaswa kutolewa ripoti za makusanyo kwa waliochangia ikiwezekana na matumizi yake, ili si tu kumpa moyo mchangiaji na wengne kuchanga, bali kuheshmu mfumo wa matumizi ya fedha ktk taasis isiyo ya hiari kama chama cha siasa.

Jibu lilipaswa kuwa "mapato ni haya.." au in-short tusubiri uongozi utasema.. Sio kukurupuka tu hapa na kujibu insensible kisa anonymous..

Let's apart ourselves from magambaz by acting and practicing "great thnkernes" in making a motion and arguing on matterz.

NB: don't misquote my comment it appliez to some CDM memberz in JF.. Soma comments zote utawajua!

Mbumbumbu intelligent!

hoja mfu inahitaji majibu kimfu, wewe ndo unaqulify kama hapo nyekundu, tunataka hoja hai zinazodeliver kwa taifa
 
Bado kazi ni kubwa na ngumu mno.....kwa style hii ya kujibu hoja.....bado wananchi wengi ni kama shamba la bibi

Mwanachama anahoji mapato na matumizi ya hela ya chama anaambulia matusi na kejeli namna hii?????

Mimi sina maswali kwa wanachama wala majibu yao hapa mtandaoni.......ila kwa viongozi wa chama kama mlivyotajwa na muweka uzi

Jambo kama hili si la kuchukuliwa kimzaha na wepesi .....hii ni hoja ya mantiki kaeni na mtoe maelezo hata.....on progress basis kuliko kukaa kimya mpaka muhojiwe kwa kitu ambacho ni obvious

Hoja ya kuwa hii ni endelevu is soo light as itaenda mpaka 2015.....so kwa muda wote huu itakuwa kimya????? Is this procedural an bureaucratic??????

Ajisemea Zitto (Mb)....."eyes on hands off"........we are watching and objectively evaluating the way you move towards expected changes.......
 
Niliichangia CDM kwa lengo moja tu, kuwawezesha kufika Mtwara na Lindi,
wamefika huko na kazi yao tunaiona. hivyo kwangu mimi lengo limetimia na
nafsi yangu imefarijika. Sina cha kuhoji hapo.
 
CDM kikianza kufanya usiri ndio mwanzo wa udikteta, ilitakiwa kiwaeleze wananchi michango inayopatikana na matumizi yake. wewe unaelaumu mtoa mada wakati huu utakuja kujutia baada ya cdm kukamata dola kama hawajaanza saiv utaratibu.
 
Back
Top Bottom