Nauliza hivi, hawa watu ni ndugu?

Nauliza hivi, hawa watu ni ndugu?



Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi na yamenisumbua sana, Mh Membe na Rais Kikwete ni ndugu? maana wanafanana sana, Hata nyie angalieni hizi picha.
Kaitaba, kuna watu mna maono kama Manabii, hapa umeuliza swali simple sana wengine wanafanya masikhara ila itakapofika Jumamosi ya Octobar 31, 2015, pale uwanja wa Taifa, siku ya kuapishwa rais mpya, nakuhakikishia, wenye kumbukumbu nzuri, watalikumbuka swali lako hili!.
 
Haahaaaaa......ila si nasikia hiyo ni sifa ya makada wa CCM Mtandao??

Membe alishaitwa JOKA LA MDIMU. Na uzuri ni kuwa hata mwenyewe alikiri kuwa NI YEYE.

Darhotwire.com
RoughGreenSnake.jpg
 
Mabingwa wa kujenga network CCM ni Membe na Lowasa.Watu wa kuuma na kupulizia.Na wakija kupambana hawa 2015 basi moto utawaka.
 
Si unaelewa hapa ni barazani? mada zinazojadiliwa nyingi hazaa mambo mengine kabisa nje ya mada
ambayo hayahusiani na mada inayojadiliwa, kama umetembelea vijiwe vya kahawa basi utaelewa mambo ya hapo
kwani hapo huanzishwa mada na wengine katika kujadili huwa wanatoka nje ya mada kabisa kabisa.

Si kweli, nasikitika kutulinganisha ''home of great thinkes'' na vijiwe vya kahawa.Michango ya hapa mingi imewaweka sawa Watz na inaendelea kufanya hivyo.Naungana na KTK anapoonya hapo juu '' lazima na vitu vya ndani vinavyofanya hao wafanane viwekwe ''
 
nisivopenda kumwangalia nyoka,natamani nianze kumkemea hapa ashindwe na alegee shetani huyu..ndo maana kalaaniwa kutembelea tumbo
 
Kaitaba umewasha moto usio wa lazima na kama unafuatilia siasa za nchi yetu utajua kwamba watu hawa si ndugu, maana hata siyo kabila moja. Kuhusu wanafanana au la, hilo nawaachia wajuzi wa kufananisha ili watuambie wanachofanana ni nini, japo wewe umesema ni sauti zao wakiongea redioni na kile ulichoita kubadilishana ofisi. Lakini mbona hata ofisi hawajabadilishana? Labda mmoja kumuachia mwenzake ambayo kwangu mimi, tha is just a coincidence!
 
huyu bwana muanzisha mada kuna jambo analolifahamu aidha kwa kusikia au kwa uhakika ambalo angependa kulisema hapa jamvini...shida ni kuwa wachangiaji wote hapo juu hamjaweza kumpatia angle ili aweze kulisema..

mkuu sema tu kile kinachosemwa na wengi mitaani....laa kama hapa si pahala pake basi hamisha mada iende kule kwenye udaku walau ukiulizwa kama una ushahidi basi utajitetea kuwa aah mbona jukwaa lenyewe linaruhusu jokes/utani na udaku/gossips...maana hicho unachokijua hakuna anayeweza kukithibitisha labda wahusika wafanye DNA testing...
 
nisivopenda kumwangalia nyoka,natamani nianze kumkemea hapa ashindwe na alegee shetani huyu..

mkuu...kwani nyoka si ni kiumbe wa mungu..kosa lake nini?

..ndo maana kalaaniwa kutembelea tumbo

kutembea na tumbo ndiyo maumbile yake na wala haimpi shida usidhani kwake ni adhabu..si unamuona anayoteleza kwenye majani...yaani pale ni kama wewe ukiwa na kipando chako halafu uko kwenye lami...

usiniulize mbona kwenye sakafu anapata shida...jibu ni kuwa hayo si mazingira muafaka kwake kujidai...kama vile wewe na kipando chako halafu uko kwenye barabara yenye mashimo au tope na utelezi wa mvua...

hizi dini zisitufanye tukaacha hata kufikiri kisa eti maandiko..kwani kaandika mungu..si ni watu tu kama sisi????
 
Kaitaba kuna kitu umetuficha hapo. Si utuambie tu. Maana mimi nikiwaangalia wala! Mimi sijui kufananisha lakini mbona hata hawafanani?! Kaitaba ndugu yangu tuchombeze wandugu!
 
Kaitaba umewasha moto usio wa lazima na kama unafuatilia siasa za nchi yetu utajua kwamba watu hawa si ndugu, maana hata siyo kabila moja. Kuhusu wanafanana au la, hilo nawaachia wajuzi wa kufananisha ili watuambie wanachofanana ni nini, japo wewe umesema ni sauti zao wakiongea redioni na kile ulichoita kubadilishana ofisi. Lakini mbona hata ofisi hawajabadilishana? Labda mmoja kumuachia mwenzake ambayo kwangu mimi, tha is just a coincidence!

mkuu it is good point. But kwani wewe ikiwa kabila ya baba yako ni x na mama yako ni x na baba yako katika kufanya safari akajikuta yuko machimboni mpanda, akaishi miaka mitatu akamega mtu akawa na mtoto na akaondoka kurudi kwenu. Kwa kukosa matunzo huyo mtoto akapewa majina ya ujombani kwa mama na kwa kuwa amekulia upimbweni hawezi kujulikana kuwa mpimbwe wa mpanda, japo baba yake ni kabila x?.

ANGALIZO: Jibu langu ni kuhusiana na hiyo kwenye red. PLEAAASE!
 
Back
Top Bottom