Nauchukulia ubingwa wa Simba kuwa sadaka ya kumfanya Manara aondoke; alikuwa mwiba kwetu Yanga

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,032
Kwanza niseme tu hewa imekuwa nyepesi mno baada ya kusikia manara kaondoka.

Mechi ya juzi kiukweli Yanga tulistahili kushindwa, Mukoko kitu alichofanya sio cha kiungwana kabisa na matokeo yake akaipa timu mzigo mkubwa wa kucheza pungufu, Ila bado niliona vijana walijitahidi licha ya kucheza pungufu.

Mechi ya juzi laiti Yanga ingeshinda basi uwezekano wa Manara kubaki ngekuwa mkubwa ila simba iliposhinda wakajipa matumaini na kuona wanaweza bila hata Manara, kwa hio hana umuhimu kivile.

Kiufupi nilikuwa naombea tu simba ishinde bao moja tu japo ntaumia kwa siku chache ila faida kwa upande wa Yanga itaonekana msimu ujao pale ambapo Manara hayupo na yanga kama mnavyojua saizi changamoto iliyokuwa ikitusumbua ya ukosefu wa pesa itatatuliwa na zile milioni 260 kutoka azam ila mwezi kujumlisha na zile milioni 50 za kila timu kwahio tutarudi kwenye form

Tunamshukuru pia GSM ambae katutoa kimaso maso miaka miwili hii ili timu isiabike kwa umaskini.

Huyu kiumbe Manara alikuwa ni mwiba sana kiukweli, kebehi zake, zarau zake, maudhi yake, kukera, n.k yani mimi kama shabiki ywa Yanga nilikuwa natamani hata aajiriwe tu kuwa balozi huko kwa bakhresa alipwe mamilioni aachane na haya mambo yake.

Kubwa kuzidi lote Manara alikuwa anawafanya mashabiki wa simba kuwa kama wehu yani, kuna misemo yake kama hatoki mtu, war in dar, next levo, n.k ilikuwa inawapa sana munkari mashabiki wa simba, hakuishia hapo alipenya hadi kwenye kusifia wachezaji na wakaonekana kama ni kina messi au ronaldo, kiukweli alikuwa ni silaha hatari mno.

Aliewahi kumweza ni Jerry Muro tu enzi za Mnaji, lakini hata Jerry Muro angebaki Yanga angeshindwa maana Manji aliiacha team ikawa na matatizo ya kiuchumi.

Laiti hata wanasimba wangekuja na ofa kwamba tuwaachie Makombe yote ligi kuu, FA na Mapinduzi basi kiroho safi kabisa tungewaachia kwa kkubaliana mtufunge hata bao mbili kila mechi tukikutana.
 
Manara inaonekana kuondolewa Simba inakuuma sana, kwanza uliwalalamikia Simba kukulipa laki saba lakini Simba waliposema walikupa mkataba wa milioni 4 ukaja na post nyingine ya kuzuiwa kufanya kazi sehemu nyingine Simba wameamua kuachana na wewe kiroho safi ni bora ukarudi kwenye timu ya baba yako.
 
Manara inaonekana kuondolewa Simba inakuuma sana, kwanza uliwalalamikia Simba kukulipa laki saba lakini Simba waliposema walikupa mkataba wa milioni 4 ukaja na post nyingine ya kuzuiwa kufanya kazi sehemu nyingine Simba wameamua kuachana na wewe kiroho safi ni bora ukarudi kwenye timu ya baba yako
Mimi ni Yanga Dam Dam, ile mshahara wa laki 7 mikia walitita aibu aisee 😂 😂 😂 yani Manara kwa simba ni kama Bunduki lakini wao wanamfanya kama bakora ya watoto, Simba wamejawa tamaa sana na hii yote ni sababu ya muhindi wao yule, Mwakani Yanga tunarudi kwenye form,

Manara alikuwa ana matusi sana ya kutukera sana huku yanga amaneno yake ya shombo yaliliza wengi sana, aondoke tu kwakweli, aje huyo gift macha
 
Hivi Manara angekuwa anatangaza products kama adidas,,,nike au Samsung simu ingekuaje?
 
Hivi Manara angekuwa anatangaza products kama adidas,,,nike au Samsung simu ingekuaje???
ingekuwa safi sana, Heri atangaze hizo bidhaa abanwe asijihusishe kabisa na mambo ya usemaji 😂 😂
 
Kwanza niseme tu hewa imekuwa nyepesi mno baada ya kusikia manara kaondoka.

mechi ya juzi kiukweli Yanga tulistahili kushindwa, Mukoko kitu alichofanya sio cha kiungwana kabisa na matokeo yake akaipa timu mzigo mkubwa wa kucheza pungufu, Ila bado niliona vijana walijitahidi licha ya kucheza pungufu...
Daaaaaaaah ndio maana sishabikii kikundi cha wajinga utopolo. Yaani mlikua mnashindwa kufanya vizuri kisa utani wa Manara. Huko ni ubogasi kabsa
 
Mimi ni Yanga Dam Dam, ile mshahara wa laki 7 mikia walitita aibu aisee yani Manara kwa simba ni kama Bunduki lakini wao wanamfanya kama bakora ya watoto, Simba wamejawa tamaa sana na hii yote ni sababu ya muhindi wao yule, Mwakani Yanga tunarudi kwenye form,

Manara alikuwa ana matusi sana ya kutukera sana huku yanga amaneno yake ya shombo yaliliza wengi sana, aondoke tu kwakweli, aje huyo gift macha
Laki Saba ilikuwa posho ya mawasiliano, mshahara wa m 4 aliukataa kwa vile hela ya usaliti aliyokuwa anavuta kwa GSM ilikuwa zaidi ya hiyo m4.
 
...
IMG-20210728-WA0018.jpg
 
Somba wamewekeza kwenye timu uwanjani, kambi bora, wachezaji bora wanaolipwa vizuri, hiyo Manara na ule mdomo wake alikuwa hachezi mpira uwanjani.
 
Back
Top Bottom