Natubu: Nilikuwa simuelewi Mwamposa, ila kwa idadi ya viwete walioponyeshwa Songea naanza kumuamini

Acha kukufuru, unamlinganisha tapeli Mwamposa na yesu.Mwamposa atapata heshima akijikita kwenye kuhubiri, lakini figisu za kutayarisha watu wazima na kuwapa magongo ili watoe ushuhuda wa uongo ajue ni dhambi. HANA TOFAUTI NA MATAPELI YA KALYNDA. Anajishushia heshima.
Amekutapeli nini??kwanini hammpeleki mahakamani kama ni tapeli??

#MaendeleoHayanaChama
 
Sijaona mtu wa Mungu ana mitusi kama wewe. Nilifikri utageuza shavu la pili, kumbe tukikuambia Mwamposa ni tapeli unakasirika. Basi usingeleta hii mada huku. Usijekutuiambukiza ujinga na sisi tukakubali kutapeliwa. Hata wale wa Kalynda walitumwa kuaminisha watu ule utapeli ilikuwa ukombozi wa umaskini. Kama Mwamposa anazo hizo nguvu, kwa nini analilia sadaka. Si amuombe amshushie $ na Euro kuliko kuwanyang'anya maskini kile kidogo walichonacho kwa kuwadanganya Mungu atawarudishia mara saba! Tapeli na mwizi wa imani huyo nabii wako.
Wengi mnao mponda mwamposa ni wachungaji uchwara mnaona waumini wanawakimbia mmeanza kukosa sadaka sasa kilichobaki ni kuanzisha bifu na chuki dhidi ya mwamposa kama yule shehe ubwabwa wa dsm.

Upako wa kweli upo kwa mwamposa chuki na bifu dhidi yake havitawasaidia.

#MaendeleoHayanaChama
 
time will tell kwani gwaji boy yuko wapi si alianza hivi hivi. hawa manabii uchwara ni moto wa kifuu baada ya mda wanapotea km hawakuwepo maana ubaya ukifanya vitu bila nguvu za Roho mtakatifu kuna mwisho wake tu.
note. huwezi ukadanganya watu wote kwa wakati wote
Kama kupotea kila mtu atapotea hao manabii na mitume wote walishapotea kila kiumbe duniani kitapotea hilo sio geni.

Ila kwa sasa habari ya mjini ni mwamposa..akiondoka Mungu ataleta nabii na mtume mwingine kama ama zaidi ya mwamposa kama ilivyokua kwa akina kulola..kakobe n.k

Kwangu mimi chamsingi injili inahubiriwa watu wanafunguliwa shida zao mengine atajua yeye mwamposa.

#MaendeleoHayanaChama
 
bandiko la post limelenga kumuinua mwamposa ila si kumtukuza Mungu si shangai ndo maana hakuna sehemu ametajwa Mungu wala Yesu hata kwny matangazo mengine unakuta anasifiwa yeye tu.

Mungu akimuita mtu kuwa nabii ni lazima utukufu apewe Mungu. ila ukiona utukufu hapewi Mungu unajua kwa huyo nabii Mungu hayupo
Ila nayehubiriwa ni nani..?au yeye mwamposa ana biblia yake kutoka mbeya..??

#MaendeleoHayanaChama
 
Yule mdada WAKONTA MAPUNDA kila siku wanampita kama hawamuoni, Namuomba mwamposa aende kumuombea yule dada kwa jina la yesu.
Uponyaji wa kiimani haupo hivyo..yani kila sehemu wewe ni kuombea watu tu wenye shida..hata Yesu hakufanya hivyo..bali wenyeshida ndio waliokuja kwake na yeye aliwaponya na kisha kuwaambia imani yako imekuponya..first imani itoke kwa muhitaji wa uponyaji ndio uponyaji utatenda kazi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkuu hilo ni swala la imani so hata kama nikikupa sababu mia bado huwezi nielewa kwani imani yako iko kwake kama ambavyo imani yangu haiko kwake
Basi kaa utulie kama huna hoja ya msingi..baki na imani yako.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kuna mzee leo kajitokeza kutoa usuhuda kuwa alikuwa hawezi kutembea kwa miaka 15 anatembelea gongo lakini mamposa kamponya ila cha ajabu gongo lake naye ni jipya
Kama alitengeneza siku za karibuni kuna ubaya..hivi mbona una akili ndogo hivi..kwahiyo ulitaka maisha yake yote awe na gongo la miaka 15 ilo pita..kwamba magongo haya chakai na kuharibika.?

#MaendeleoHayanaChama
 
Hata Bwana wetu Yesu hakuponya wote aisee.
Tuelekeze pia mahali ambapo watu walikanyagana mpaka wakafa kwa kutafuta huduma yake.
Bwana Yesu kuna aliowaponya wakiwa majumbani/barabarani.
Tuletee ushahidi ambao Mwamposa kafanya hivyo nje ya huduma ya majukwaani
 
Jamani jamani jamani

Yule kiwete karudi na uwete wake, analalamika kichwa kinamuuma kapigwa na jua siku tat
 
Mim nikajua na wew upo hapo uwanjan umeleta ndugu mlemavu kapona, kumbe upo Kwenu Tegeta unaangalia kwa Tv yako hisense isio na stand 😂😂
 
Mleta mada au nikupe na kapicha ka huyu mama jirani aliyeenda kuchomeka juani na kumulikwa na camera pale matarawe? Na karudi na uwete wake
 
Nashangaa mtu anaeamini yale maigizo,,

Wagonjwa wamejaa mahospitali wanapumulia mipira,

Wagonjwa wa kansa wamejaa ocean road,

Wenye matatizo ya moyo wamejaa taasisi ya JK

Vichaa wamejaa mirembe,

Wagonjwa wa figo wapo muhimbili,

Kwanini huyo mwamposa asinde kuwaponya hao wagonjwa wanateseka na hawajui hatma yao??
 
Ukiona hivyo hawana imani..halafu faith healing haiendi mnavyotaka nyie..lazima ianzie moyoni kwa mhuhusika yana yule anayehitaji uponyaji..tusema mara ngapi muelewe.

Imani kwanza ndio itakayokupa uponyaji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nashangaa mtu anaeamini yale maigizo,,

Wagonjwa wamejaa mahospitali wanapumulia mipira,

Wagonjwa wa kansa wamejaa ocean road,

Wenye matatizo ya moyo wamejaa taasisi ya JK

Vichaa wamejaa mirembe,

Wagonjwa wa figo wapo muhimbili,

Kwanini huyo mwamposa asinde kuwaponya hao wagonjwa wanateseka na hawajui hatma yao??
Faith healing haifanyi kazi hivyo..hata Yesu hakuenda hospitali bali walimfuata alipo ili awaponye na mwisho wasiku aliwaambia imani yako imekuponya.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukiona hivyo hawana imani..halafu faith healing haiendi mnavyotaka nyie..lazima ianzie moyoni kwa mhuhusika yana yule anayehitaji uponyaji..tusema mara ngapi muelewe.

Imani kwanza ndio itakayokupa uponyaji.

#MaendeleoHayanaChama
Mtu anafunga safari kutoka Mtwara mpaka Songea na anarudi kama alivyokwenda.
Hivi mnataka mtu awe na imani ya namna gani au ajipange vipi moyoni mwake ndipo uponyaji huo umguse ?
Kwamba watu ninao wafahamu mimi wote hakuna hata mmoja aliyepona then nije kuamini ngonjera za TV !
 
Back
Top Bottom