Natoa wito kwa TAKUKURU Tanzania

Enzi na Enzi

JF-Expert Member
May 29, 2020
530
500
Kama watu wa Takukuru mnapitia hum JF. Natoa taarifa kupitia jukwaa hili pendwa.

Naomba msiishie kuichunguza Chadema na CCM kuhusiana na rushwa za matumizi mabaya ya fedha kwa Chadema na wagombea wa CCM ambao kila siku mnawafuatilia katika majimbo yetu kwa misaada wanayotupa kama ni rushwa.

Niwaombe, kipindi hiki cha uchaguzi, na hasa baada ya bunge na mabaraza ya madiwani kuvunjwa! Naomba msisahau kuziangazia shule zetu za sekondari na misingi.

Kamati za shule na baadhi ya walimu wameanza mikakati ya kukusanya pesa pamoja na chakula kwa lengo la kujinufaisha!

Najua mna weledi wakiuchunguzi, kuliko mbinu wanazotumia walimu na kundi lao kupiga, walimu wanatumia mihitasari ya kamati za shule na baadhi yawazazi ambao nisehem ya michezo hii, huku wakiitisha vikao vya siri kubariki wizi huu.

Kwani! Wazo la kuongeza mda wa masomo ili kufidia mda kwa ajiri ya kumaliza topic nadiriki kusema siyo wakweli. Kuna shule zetu za serikari hususani za kata (baadhi) hata kabla ya covid-19 huwa hazimalizi topic kwa muhula mzima.

Sasa wamejipanga kutumia sababu hii kupiga wananchi na kwa shule za msingi wanajipanga kupiga kwenye uandikishaji. Kilo 10 za mchele na 2000@ mwanafunzi + ndoo ya mkaa au mzigo wa kuni! Nikuta wazazi walishe familia za walimu.

Kama wangekuwa nania njema wangewapereka watoto makambini km alivyofanya mkuu wa mkoa wa Simiyu. Lakini michango hii hii ndio itangizwa kuhalalisha matumizi ya fedha za serikari kuwa zilinunua vyakula na mahitaji mengine

Hii nayo nirushwa kam rushwa zingine! Lakini ni matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya walimu wanaojinufaisha kupitia mchezo huu (si wote)

Bado nikosa lakutumia taaruma kwa lengo la kujinufaisha.

Nawasilisha tafadhari.
Enzi na Enzi
 

Ndachuwa

JF-Expert Member
Mar 8, 2006
6,004
2,000
Chagua moja uchange hayo makande na maharage mtoto apate mlo wa mchana au mwanao ataabike siku nzima bila chakula.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom