Natoa pole kwa mapacha walioungana, Consolatha na Maria

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,198
Mapacha walioungana, Consolata na Maria bado wanaendelea kutibiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam.

Pichani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofika hospitalini hapo kuwajulia hali na kuwatakia uponyaji wa haraka.

Namuomba Mungu ili Consolata na Maria wakapate kupona na kurejea chuoni kuendelea na masomo yao.
FB_IMG_1518289894574.jpg


Wakuu hivi Consolata na Maria akiumwa mmoja wanaumwa wote?
Ndugu wana JF tuwaombee ndugu zetu wapone.
 
Mapacha walioungana, Consolata na Maria bado wanaendelea kutibiwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es salaam.

Pichani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofika hospitalini hapo kuwajulia hali na kuwatakia uponyaji wa haraka.

Nasi Jamii forum tunamwomba Mungu ili Consolata na Maria wakapate kupona na kurejea chuoni kuendelea na masomo yao.
View attachment 693672

Wakuu hivi consolata na maria akiumwa mmoja wanaumwa wote?
Ndugu wana jf tuwaombee ndugu zetu wapone.
Nilishawaza sana hichi kitu sasa akifariki mmoja itakuwaje jaman?? Mitihani ya dunia hiii achen tu
 
Kwani anaumwa mmoja au wote?
Na moyo wanachangia mmoja au?

Anawaza akifariki mmoja itakuwaje. Anaumwa mmoja na kila mmoja ana moyo wake ila kwa kuwa hawawezi kutengana imebidi walazwe wote. Akifa mmoja ndo swali linalomwazisha mwenzangu. Nami linaniwazisha maana sijui sayansi. Moyo na ubongo kila mmoja anajitegemea ila kwenye kiwiliwili kuna viungo wanashea. Ikitokea huyo mgonjwa akafariki halafu viungo vilivyoungana vinaendeshwa na ubongo wa aliye hai itakuwaje? Nawaza yule hai atajisikiaje kuona maiti ya mwenzie? Madaktari watamharakishia kifo au watamchelewesha marehemu kuoza? Nawaombea uzima hawa mabinti.
 
Back
Top Bottom