Natoa Mil. 2 Tshs,nilipwe pesa yangu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natoa Mil. 2 Tshs,nilipwe pesa yangu.

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Katabazi, Apr 21, 2010.

 1. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Salama wana JF!Niliuziwa kiwanja mbele ya adv. Kwa kupitia bank, kumbe hakina njia (sala2,DSM)nikatoa adv.20m,muuzaji amenizungusha,sasa sikitaki nataka mwanasheria atakaye recover hy pesa nimpe 2m.
   
 2. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mzee ulinunuaje mali pasi kutafiti eneo husika?? kurecovery inategemea na masharti ya makubaliano katika Mkataba wenu wa mauzo na iwapo taarifa za hali jhalisi ya kiwanja kulifichwa na kwa ufahamu wako hukuweza kuelewa (misrepresenation)..Nadhani huyo Adv aliyekusaidia angekuwa mzuri zaidi pia kukueleza sheria na kama kuna tatizo juu ya Makataba wenu ni vyema ungemjulisha shida ilipo ili kama anaweza akusaidie kwa kuzingatia na "facts" kamili ya issue yako.

  Kwa ushauri tu, kitaaluma, haishauriwi wala kuruhusiwa kwa Mwanasheria kupokea fedha ya Mteja katika suala linalohusu mabishano katika madai au kesi ya Mahakamani (contentious matters) kwa makubaliano kuwa atashinda. Vinginevyo utadanganywa tena. Hakuna Makubalina kama hayo kwani asipoweza ku recover hiyo hela yako, utamdai?? au ikiwa italazimika kufikishana Mahakamani, hiyo 2M itatosha kushughulikia kesi??..
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145

  Mkuu, mkataba unasemaje? Nani aliyeandaa huo mkataba? Je ulikagua hicho kiwanja kabla ya kusaini hati ya makubalino? Je, muuzaji alikuwa na wajibu wa kukupatia njia kulingana na makubaliano yenu? Je umenunua kiwanja pamoja na njia au umenunua kiwanja pekee? Mkataba unasemaje? Ukiyajibu haya maswali basi utaweza kujua umesimama wapi katika madai ya marejesho ya hiyo 20 milioni.
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Pole, kanunue eneo uweke njia, ukienda mahakamani ndugu ni soo, kama wewe sio kina Chenge au Marehemu Dito kesi itakaa miaka kibao utafikiri mtoto, mie na kesi ya design hiyo toka 2003 mpaka leo, kwa mwaka inatajwa mara 4 tu kati ya hizo 2 mawakili hawapo, 1 hakimu ana udhuru hiyo 1 ndiyo inasikilizwa na unakuta kuna PO. Yaani unaweza ukafungwa wewe kwa hasira
   
 5. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nawashukuru nyote:
  1.Kama hujauziwa kiwanja na mswahili mengi huwezi kuyajua,lakini nilichukukua tahadhari nyingi iwezekanayo na mojawapo lililonisikitosha na sijaelewa ni kwanini niliomba tuuziane kwa kupitia kwa advocate,maana nilitegemea pesa nyingi aliyodai,sasa ndio ilikuwa wakati wa yeye kuniokoa sasa amekaaa kimya wala hataki kujihusihsha as if kazi yake ilikuwa kwenye ku stamp muhuri na kuchukua pesa,anyway nitajibu kama ifuatavyo.
  1.Mkataba unaonyesha kuwa upande wa mbele kuna barabara ya mtaa na tulimpiga picha akionyesha barabara amabyo sasa mtu mwingine anadai kuwa hiyo ni part ya plot yake japo ni barabara na hataki itumiwe na mtu mwingine na anataka kuiwekea fence.
  Na walikuwa wana ugomvi muda mrefu na huyo bwana.
  2.Mkataba uliandaliwa na advocate na ukapitiwa na mimi na muuzaji
  3.Kukagua maana yake nini?Nilikikagua kwa maana ya kuwa kiko eneno lake.
  4/5.Muuzaji alinionyesha kuwa ile ni njia na la kushangaza hata huyo anayedai kuwa ni njia wakati tukileta watu wa ardhi kujua kama hicho kiwanja hakipitiwi na barabara au miundo mbinu hakuwahi kutuzuia tukipita na gari zaidi ya kutuambia kuwa ni kweli hicho kiwanja na cha huyo bwana.
  Mwisho mimi sihitaji kwenda mahakamani ila kwa wanaojua sheria nina imani wakitumia ujuzi wao wana nafikiri wanaweza kujua kama wataweza hiyo kazi au la na sihitaji kuua mtu kupata haki.
   
 6. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mh.Ngoshwe( a) nimeishalijibu wakati namjibu Ndugu Shadow,ni bahati mbaya kumbe ilibidi na Advocate niingie naye mkataba wa kujua hiyo pesa ninayomlipa ni ya shughuli gani,maana sasa ananionyesha kuwa kama hii si kazi yake-na sisi tusiojua sheria tunawaamini hawa wanasheria kama ma padri kuwa kila analokutendea analifanya kwa haki na kukutetea wewe,kumbe wakati mwingine inakuwa sivyo ( b)Hapa mimi fundi mchundo sikukuelewa kabisa,ila kwa lugha rahisi mimi nataka mtu amabaye nitaingia naye mkataba kuwa akikomboa hiyo pesa moja kwa moja nampa hiyo 2M,sidhani kama nahitaji kutoa 2M kabla sijapata hiyo haki,itakuwa kama nilivyotoa pesa nyingi kwa huyo mwanasheria wangu kabla ya ku own hiyo land.
   
 7. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu Katabazi,
  Je, hicho kiwanja kimepimwa? Master plan ya eneo hilo inasemaje?
   
 8. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #8
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwenye eneo(njia) anadai hata kama nikitoa 100M hatoniuzia hiyo njia wala kuniruhusu kuitumia ndio maana naona si vyema nikaishi na majirani wa hivyo. Kesi?unachosema ni kweli na sina subira maana pesa yenyewe nilikopa benki nikijua nimemaliza jambo moja kumbe ndio nimezua balaaa maishani,sasa nakatwa benki kila mwezi.
   
 9. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Pole inaonekana eneo lako halijapimwa, kama sikosei muuzaji aliongea na jirani aache wazi ili tu wewe ununue, au jirani alitaka kumuuzia njia akakataa, ilinikuta hii, ila badala ya makelele mfuate taratibu huyo jirani muombe akuuzie hiyo njia, then leta watu wa ardhi upimiwe na alama. Huko kwa advocate na mahakama naona kama unakosea kwa stage uliyopo muuzaji kakuachia soo tu, bembeleza upate njia, mie ilinichukua mwaka nimeuziwa 1.5m.
   
Loading...