National Parking(NPS) Wizi mtupu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

National Parking(NPS) Wizi mtupu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Obhusegwe, Jan 26, 2009.

 1. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jamani habari za mvua?

  Leo wakazi wa dsm tumepata mvua, nadhani wengi wamefurahi, mbali na kuwa kuna kero mbalimbali associated with it.

  Leo nilikuwa mjini mapema sana asbh, nikapaki gari ''somewhere" nikaenda kwny shughuli zangu. Nilivyorudi nikakuta gari zima limezungukwa na dimbwi la maji yaani hakuna jinsi ya kuingia mpaka nikanyage kwenye maji!! Jamani imenipa mtihani, mwisho nikajitoa muhanga nikayakanyaga maji ndo nikaweza kuingia kwny gari.

  Sasa la kutia hasira!! Kabla sijawasha gari, akaja dada amevaa koti la NPS, akakinga mkono anataka pesa, nikamuuliza pesa ya nini, akasema ''ya parking'', nikamwuliza parking gani kwny dimbwi? akasema yeye hajali alimradi gari limesimama, anachotaka ni pesa!! Du!! nikashangaa!!

  Nililoamua ni kuwasha gari na kuondoka bila kulipa kwani bado nilikuwa na hasira jinsi nilivyochafuka kutokana na hilo dimbwi!! sasa sijui watanitafuta au la!! Najua naweza kuwa nimevunja sheria, lakini tujiulize yafuatayo;

  Je NPS kazi yake ni kukusanya pesa za parking tuuuu au inao wajibu pia wa kuhakikisha parking zinapatikana kirahisi na zinakuwa na hadhi ya kutosha?
  Je ni haki kulipia huduma ambayo ubora wake ni almost zero? Au watanzania tumeshazoea kutoa hela tu(hata kama ni ndogo) bila kuuliza alimradi mtu amesema lete hela?
  Ni maeneo mangapi hapa mjini NPS au tuseme halmashauri za manispaa zetu zimeyadesign mahususi kwa ajili ya parking(nimeona la pale karibu na PPF house ambalo nalo ni matope matupu!!) au wanasubiri tu watu wakishajenga majengo then wao wanaweka P kuubwaa!! mbele ya jengo na kusubiri watu waegeshe nao wadai 300?

  Jamani huu si wizi????? Tunaibiwa tukiwa macho!! Watch out!!!
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Nililoamua ni kuwasha gari na kuondoka bila kulipa kwani bado nilikuwa na hasira jinsi nilivyochafuka kutokana na hilo dimbwi!! sasa sijui watanitafuta au la!! Najua naweza kuwa nimevunja sheria, lakini tujiulize yafuatayo;

  MKUU hapo ukumtendea haki,,anaeshuglika na mambo ya barabara ni wizara ya miundombinu na TANROAD,yeye hana mamlaka ya kuongeza hata mchanga hapo,,,so swala la mvua kujaza madimbwi na je mvua isingenyesha,,nafikiri walaumiwe halmashauri ya kinondni ilala temeke ambazo zinachukua pesa nyingi tu kwa hawa mabwana na kwenda kugawana kwenye bara badala ya kuzifanyia kazi,,,ombi langu kama unamkumbuka vyema ukaenda kumrudishia ama kama vipi nipatie namba yake nitamrejeshea ,,ulikaa muda gani,,kumbuka yule kakulipia siku hiyo maana asipolipwa inakula kwake,,,,kuna supervisor wanahesabu magari so usipolipa wewe huyo mtu anakutolea huoni dhambi...............
  TENDA WEMA UENDE ZAKO
   
 3. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Thanks, mawazo mazuri

  Lakini nadhani yeye ndo anaweza kuwa karibu na hao na kuwajulisha yanayoendelea kwny street. Kwa nini nilipie huduma mbovu? Kuhusu wema, hapo tutaonana wabaya kwani hiyo ni business hakuna swala la wema hata chembe, akija kwangu glass ya maji nitampa, huo ndo wema. Habari za kutoa hela kwa huruma tu sizifagilii kabisa, hao ndo street scammers na hao mabosi wao, kama hawawezi kuwaconvice wanaohusika warekebishe hali, then wajue itakuwa inakula kwao kila mara mpaka labda waache hiyo kazi.
  Thats the way i see it mama, na nawahimiza na wengine wenye magari ''PLZ USILIPIE PARKING MBOFUMBOFU!!''
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Talking about parking in Dar? wapi kuna parking? Ni wizi mtupu!

  Hivi ni nani mwenye huo mradi vile?
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  The same problem kila kukicha...management of our resources. Wanakusanya hela lakini sidhani kama zinatumika kule zinakokusudiwa...Pengine kiasi kikubwa kinatumika kwenye posho za mikutano ya manispaa. Za kujengea barabara nzuri zitapatikana wapi?? Namuonea huruma huyo dada mana kutolipwa imekula kwake
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mama mia sound like una interest na NPS

  Mimi naungana mkono na wewe uliyekataa kulipa kwa kuwa hawa jamaa wanachojua ni kukusanya tu na si kuboresha miundo mbinu. Unaposema hiyo ni kazi ya Wizara ya miundombinu, Mama sikuelewi hapo. Kama ni kazi Miundombinu kwa nini wao ndiyo wasikusanye hiyo hela ya parking wakatengezea mifereji na badala kuwaacha hawa NPS wakichukua hela na kupeleka kusikojulikana?

  Parking ni service na service lazima uihudumie au uiboreshe ili kuipa value. Sasa kwa style hiyo ya madimbwi hiyo parking kwa leo ilikuwa valueless. Tena ningekuwa na uwezo ningehamasisha watu wote wasilipe wakipaki kwenye madimbwi ili hawa jamaa wajue kuwa siku mvua ikinyesha hakuna hela ya parking na wakae nyumbani, au wamweleze huyo anayewatuma kuwa waboeresha parking.

  Hii sasa inakuwa na tupo Somalia yaani watu wanakusanya ushuru amabao hawautumii kuboresha huduma bali ni kujilipa mishahara tu basi. One objecive of tax is provision of public goods including these parking spaces.
   
 7. M

  Mkora JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwenye mradi ni mkomunist na mjamaa maarufu yaani mpinga ubepari number moja nchini
  Dini yake yeye ni ujamaa
   
 8. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wizi mtupu. Kama kweli angekuwa mjamaa hasingewaibia watu mchana kweupe. Ni bora ukalipia huduma unayopata na sio kama hawa wezi wa NPS. Hili wazo lako mkuu la kuhamasisha watu walisipie hii kadhia naiunga mkono asilimia 101.
   
 9. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  You run from Kingunge's NPS and succumb to Kivela' Yono or or the majembe's, they will tow your car wherever you will be parking and you will pay for the breakdown and fine big time.

  The lady has just taken your car number and reported to her bosses as the exchange for the payment she deserved!

  .....ndiyohiyo
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ha ha ha..

  Huyo muzee ni 'mjamaa' na sio MJAMAA (without ''.). Jinsi nchi inavyofanywa masikini chini ya uangalizi wa 'wajamaa' hawahawa ingekuwa Uchinani huyo kichwa chake halali ya serikali zamaaaani..
   
 11. Obhusegwe

  Obhusegwe JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 232
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ha ha haaaa!!

  Hiyo labda si TZ, hiyo sehemu nilipark sikku moja na sijui kama nitarudi hapo within six months, and by the way do you want to tell me ana proof tosha ya kunikamata? Hata akienda kisutu, nitamwacha huko!!!

  Nawashukuru sana akina Hofstede kwa kuona na kukemea ufisadi huu wa miatatumiatatu. Watanzania tumefikia sehemu inabidi tulipie huduma tunayopata, siyo unalipa kwa sababu tuu serikali imesema ulipe!! Inamaana kama serikali leo itasema ''kila ukilala na mkeo unalipa kodi'', wewe utakubali????? Watch out bro, pigana vita na adui aliyeko mbele yako, yule unayemuona macho kwa macho, hayo mambo ya mafisadi wa BoT waachie akina Zito huko bungeni wanatuwakilisha, sisi vita yetu juu ya mafisadi ianzie huku mitaani kwenye miradi yao waliyojiwekea kwa manufaa yao(kama huo wa parking). Watanzania tukiwa na umoja ktk mambo madogomadogo kama hayo, ndo tutaweza kujenga nguvu ya kupambana na sangara.

  Samahani kama nimegusa maslahi yako, lakini habari ndo hiyo!!!

  ALUTA CONTINUA!!
   
 12. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #12
  Feb 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  NPS interst yao ni hela, lakini sijui kama kuna maegesho yoyote ambayo wametengeza au wananyoweza kuyaita maegesho. Ni wizi tu hakuna lolote la maana linalofanyika mbali na kutumia vyombo vya dola kuwanufaisha watu. Kukiwa na Uongozi makni hii kero itaondoka tu.
   
Loading...