National Insurance Corporation(NIC) Limefungwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

National Insurance Corporation(NIC) Limefungwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gembe, Feb 5, 2009.

 1. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Heshima Mbele,

  Kwa taarifa nilizonazo ambazo nimepewa toka kwa mkulu mmoja wa shirika la Bima ni Kwamba Serikali imeagiza shirika hilo lifungwe wakati serikali ikiamua ni nini kifanyike kulinusuru shirika hilo.

  Habariz a ndani kabisa zinasema kuna baadhi ya watu wanataka kulichukua shirika hilo kama wawekezaji kwa bei ya kutupwa(Majina ninayo nasubiri kwanza) .Watu hao ni baadhi ya viongozi wenye sauti kubwa katika serikali.

  Habari hizi zinasema kufa kwa shirika hilo kumechangiwa sana na Mkurugenzi Mkuu Mama Ikongo na baadhi ya maafisa wa juu wa shirika hilo akiwamo Mkurugenzi wa Fedha na Utawala
   
 2. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Haya wakuu,Nani alilifiisha shirika hili hapa
   
 3. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  NIC restructuring takes off
  PIUS RUGONZIBWA
  Daily News; Thursday,February 05, 2009 @07:31

   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Historia ya watawala wetu "points to nothing else" isipokuwa ufisadi hata katika hili.Kuna wingu zito la ujinga wa kutupwa lililotanda juu ya watawala hawa."They do not think of anything else" isipokuwa kujipatia fedha ya aibu hata katika kipindi hiki ambapo wanajua fika kwamba ujinga wao uko wazi kwa wananchi wote.
  Mungu aisaidie Tanzania jamani, "it's too much to bear."Mmm.

   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Bima ya Taifa yawafuta kazi wafanyakazi wake wote


  SHIRIKA la Bima la Taifa (NIC), ambalo ni kongwe na kubwa kuliko taasisi zote zinazotoa huduma hiyo nchini, jana lilianza kutekeleza mchakato wa kuachisha kazi wafanyakazi wake wote na kuwaajiri upya ili liweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.


  Shirika hilo, lililokuwa na haki peke za kuendesha shughuli za bima nchini tangu mwaka 1967 wakati serikali ilipotaifisha mashirika binafsi, lilianza kuyumba mwaka 2000, miaka miwili baada ya serikali kulegeza masharti ya biashara na likatimua zaidi ya wafanyakazi 700 ili kupunguza gharama za uendeshaji, lakini tatizo la ufanisi linaonekana kuendelea.


  Katika taarifa yake, mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NIC, Hamisi Kibola anaeleza kuwa zoezi la kuachisha kazi wafanyakazi wote linafanyika kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya wafanyakazi, serikali na kampuni ya Consolidated Holding Corporation.


  Dk. Kibola alieleza kuwa wafanyakazi wote wa shirika hilo lililoanzishwa mwaka 1963 wameachishwa kazi na walitarajiwa kulipwa mafao yao kuanzia jana.


  "Aidha, taratibu za kuajiri upya wafanyakazi tayari zimefanyika kulingana na mahitaji ya shirika," alisema Dk. Kibola.


  Dk. Kibola alisema katika taarifa yake jana kuwa kutokana na zoezi hilo, shirika litasitisha huduma zake kwa siku mbili mfululizo, kuanzia leo na kurejeshwa upya Jumatatu ijayo.


  "Wakati wa zoezi hili huduma, huduma za NIC zitaendelea kutolewa na madalali na wakala wa bima wa NIC waliopo nchini kama kawaida," alisema Dk. Kibola akizungumzia huduma za shirika hilo ambazo ni pamoja na bima ya maisha na nyingine.


  "Marekebisho hayo yanahusisha kuachishwa kazi kwa baadhi ya wafanyakazi kuanzia Februari 4 mwaka huu na kuwalipa mafao yao kulingana na mikataba yao. Utaratibu wa kuajiri wafanyakazi wapya tayari umeandaliwa kwa mujibu wa mahitaji ya shirika," alisema Dk. Kibola.


  Hata hivyo, hadi jana jioni wafanyakazi wengi walikuwa hawajalipwa stahili zao na wengi walikuwa wamekusanyika mitaa ya katikati ya jiji wakisubiri hundi zao.


  "Hakuna kitu," alisema mfanyakazi mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alipozungumza na Mwananchi majira ya saa 11:00 jioni. "Nilikuwa likizo na nikasikia kuwa tutalipwa leo. Nimekuja hapa tangu asubuhi, lakini hakuna kitu tulicholipwa hadi sasa. Labda sasa tusubiri kesho."


  Mwaka 2006, kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi ilipinga mpango wa serikali wa kuliuza shirika hilo liuzwe kwa Sh3 bilioni na kuwaita viongozi wa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) ili kuwahoji kuhusu mpango huo.
   
Loading...