Cruel mpole
JF-Expert Member
- Jul 3, 2013
- 282
- 106
Nashukuru Mungu kuzaliwa tarehe hii na mwezi kama huu,najiona ni mtu mwenye bahati sana,namshukuru mama yangu mzazi kwakuvumilia nakunitunza kwa miezi 9 tumboni mwake nakunileta ulimwengu huu mnamo tarehe 1.1.1991.vilevile namshukuru baba yangu mzazi kwa kutambua umuhimu wa malezi kwa mtoto na kutambua umuhimu wa elimu.Kanisomesha kwa hali na mali na kuvumilia usumbufu wa hapa na pale uliojitokeza,mpaka sasa nina kazi yangu,ninaishi vizuri na nina afya njema.Vilevile nawashukuru wana jf kwa kunipa kampani ya hapa na pale,hasa pale ninapotoa thread kuhusu jambo flani linalohitaji ushauri,hamkusita kunishauri.Mungu awabariki sana,na awajalie heri na fanaka kwa mwaka mpya 2014.AMEN.