Nateswa sana na jini mahaba

stori yako hakueleweka umebaki kulalamika sana pili jini hafungi riziki ya mtu riziki hutoa mungu hakuna kiumbe wa kuizuia
 
Pole sana ndugu kwa changamoto hiyo. Suluhisho la kudumu la tatizo lako ni moja tu, Yesu Kristo.
Yesu Kristo ndiye mwokozi na hakuna linaloweza kumshinda. Yesu Kristo alikuja duniani kuwaokoa wanadamu kutoka kwenye utumwa wa dhambi pamoja na kazi zote za shetani, ikiwa ni pamoja na hayo majini.
Unachotakiwa kufanya ili kufunguliwa kabisa sio tu kwenda kwenye maombi, bali unatakiwa ukubali kumpa maisha yako Yesu. Umruhusu Yesu Kristo awe mwokozi na mtawala wako. Yeye akiingia ndani ya moyo wako atakufanya kuwa kiumbe kipya na kukutoa katika utumwa wote wa ibilisi na hayo majini.
Unaweza kunipigia kupitia 0754288391 kwa maelezo zaidi na msaada wa maombi
 
Yaani nakuelewa sana km kweli wahitaji msaada nitafute nkusaidie niliteseka for 25 good years na hilo dubwana mpk last year...nimepona km uko serious ntakusaidia hakuna ndumba,wala kuvaa hirizi utapona hutaamini kwa uwezo wa Mungu.

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
 
Naliona tatzo la ugonjwa wa akil hapa

Nenda muhimbil kuna kitengo maalu. Watakusaidia
HII NDIO TIBA SAHIHI, 90% Ya wadau humu wana imani hizo za ajabu, na ni sababu ya mazingira ya jamii yetu, upungufu wa uwelewa ikiwemo elimu, maisha duni

Na Imani hizi zimeshamiri sana maeneo ya Pwani, na baadhi ya kusini

Kuendelea kuamini ugonjwa unakomaa, NI MAGONJWA YA AKILI NA UNAUSABABISHA MWENYEWE

Sorry mm sina taaluma yeyote, NI IMANI YANGU TU na kama ni vinginevyo Mwenyezi MUNGU ANISAMEHE
 
Jini mahaba, chuma ulete, limbwata, kurogwa ni matatizo ya watu masikini tu. THINK


BTW hizo ni image umezitengeneza mwenyewe kichwani MATATIZO/ CHALLENGES zipo kutufunza ni formula you cant grow if you dont face challenges usifikirie zimeletwa na mtu au kiumbe.
 
Rafiki,nitakuuliza swali,umewahi kuwa na uhusiano na mtu sababu ya kuunganishwa na mtu mwingine wa tatu?!lets say una mke lakini ulimpata kwa kuunganishwa na kaka yako,na kila mnapokuwa na jambo huyo kaka yako husikilizwa zaidi na mkeo so unajikuta unamtumia kakio kusolve kila jambo sensitive kati yako na mkeo?uhusiano wenu unaimarika katika uwepo wa third party lakini mkiwa wenyewe wawili hivi inakuwa shida,umewahi kuona aina hizi za relationship?!huwa zinadumu?The answer is NO.
Wewe unakuwa hujaoa mkeo bali umeoa kakaako.
Au hata ofisini,boss hapendi kudeal nawe moja kwa moja,humtumia mmoja wenu ambaye anaelewana nae zaidi kuliko mliobaki?aina hizi za relationship huwa zinadumu kwa amani mda mrefu?NO!

Now the same applies spiritually.
There is something going on btw you and that spiritual being!
Zingatia post za wadau namba 88 na 91.Wameeleza vitu vya msingi ambavyo ukivizingatia ukombozi wako unapatikana hakika.
Kuna kitu ambacho kilikuwa hakimpendezi Mungu na kinampendeza huyo jini.Kitu hicho ndio kinampa mamlaka ya kuwa nawe na kukusumbua.
Utahangaika hadi kuzimu kama hujagundua ni kitu gani ulikifanya kwa consent yako kisichompendeza Mungu na kumpa huyo jini njia na uhalali kuyacontrol maisha yako,hautomtoa huyo jini.
Lazima mkataba kati yako na yeye uvunjwe,halafu uingie mkataba na Mungu.
Mkataba unadumu muda wote baada ya kuwekwa.Ina maana jambo ulilofanya likamleta inawezekana bado unalifanya au hujalivunja kwa kunuia na kutamka.Kuna kitu kipo kwako kimemleta.Its between you and her.So you are the only one to break it.Hakuna third party atakayeweza kukusaidia na msaada wake ukadumu.No,lazima wewe binafsi uhusike 100%.
Yapo mengi sana tunayafanya haswa ujanani ambayo ni very dangerous spiritually ila hatujui.

Mambo matatu binafsi naona mara nyingi ndio hufungua mlango wa mapepo kumuingia mtu ni uzinzi,kutokusali, na emotional stress( hasira,uchungu,unyonge,majuto, na vitu kama hivyo) hufungua mlango wa roho kwa mapepo sababu vitu hivyo vitatu vinampunguzia mtu nguvu za kiroho alizo nazo.

Na kama ni mzoefu utagundua silaha hizo tatu za shetani hushirikiana kumuathiri mtu.
Unaletewa jambo,linakutia stress,muda unavyokuwa mrefu ukiwa na hizo stress,unakata tamaa na kuanza mambo mengine kama uzinzi,ulevi etc na ibada inaondoka kichwani.
Ikifikia mahali una habits ambazo unaona kabisa huwezi kuziacha hata ufanyeje,ujue ushaingia mkataba na kiumbe fulani yuko nawe anaoperate.
So ukitaka kumtoa vunja kile kilichomwingiza kwanza.Utapambana kukivunja kama ulivyopambana kukijenga.
Silaha yako kuu ni maombi tu,hakuna dawa nyingine.Ni maombi na kuvunja mkataba full stop.
 
Kuna special case.
Inawezekana ukawa mtu mtulivu sana,na HUJAWAHI KUFANYA ZINAA(kama wewe ni bikra hakikisha unasali sana,hawa viumbe hupenda sana mtu msafi wa aina hiyo sababu ya kuwapa material fulani ya kichawi muhimu kwao).Lakini kukawa na jambo fulani umelifanya kuondoa ulinzi wa kiungu,labda hufanyi ibada,au una stress sana etc.Ghafla haya maviumbe yakaanza kukuandama.
Ujue hapo kinachotafutwa ni nguvu zako za uhai kupitia sperms(unavyolala na kuota unafanya navyo mapenzi actually ni njia ya kukufanya uwape material hiyo muhimu sana katika ulimwengu wao wa roho na uchawi.
Na kwa case hii inawezekana pia pakawa na mkono wa mtu,yaani wachawi na wanapendelea kuiba nguvu hizo toka kwa watu wasafi wasiofanya uasherati,ulevi etc

Principle ni ile ile tu.Tafuta pale ulipopungua mbele za Mungu,fix it,then fanya ibada endelevu.Yatakwisha.
Huwezi kutibu kitu endelevu kwa kutumia tiba ya mara moja.
Kama majini na wachawi hawachoki,wanakutaka kila siku,then you need to be a man of prayers daily all your life.
Pengine kuna swali unajiuliza,why me?The answer is very simple..BECAUSE IT'S YOU.
Sisi binadamu tulivyo tofauti sura zetu na muonekano basi mpaka kiroho ni hivyo hivyo.
Wapo wenye mvuto wa kiroho kuliko wengine na hawa kama wasipojitambua na kujua waishije,huishia kuwa na tabu sana hapa duniani.
Utakuta kijana mzuri,ana akili na kila sababu ya kuwa namna fulani,lakini hayuko hivyo.
So usije ukajifananisha na watu why wao wako na amani,wanafanya maovu na wanasonga mbele,lakini wewe ni vita tuu hadi uishi mfumo fulani wa maisha.
Ujue una namna yako katika ulimwengu wa roho kinachovutia wanaoendesha ulimwengu huo so unapaswa kujitambua.
 
Kula Sana kitu Moto na sali kwa Imani,ukiamini kuwa Yesu anaweza tayari roho mtakatifu anakuwa ndani yako,pia epuka maisha ya kinafiki,mfn kufanya uasherati ukiamini hakuna anaekuona,wakati roho mt.anakuona na shetani wako Yuko pembeni anasubiri utende uovu akurudie,maana unapotenda uovu kwa kujau hasa gizani,roho mt.anakutoka shetani anaingia.
Zaidi ya yote tiba sahihi ni Yesu kristo.waganga hawawezi.
 
Kwanin unaimani za hovyo namna hio mkuu...

Mimi naishi nikiamin..

No shetan
No majin
Nikifeli lazima nijue tatizo na Mara nyingi inakuwa kutokuwa makini..

Kukataliwa na watu I don't care kwan huwez pendwa na kila MTU hapa duniani ..

Acha kuwa na mawazo ya kigiza giza
Nimeandika na kufuta mara kadhaa.

Maisha yana mambo mengi sana, omba yasikukute.
 
Pole sana kwa mitihani ya maisha na dunia
Wengi wanateseka na mashetani wabaya kama hao
Ushauri wang kwanza kabsa weka nia alaf omba msamaha kwa mungu
Funga siku 3 mfurulizo amka usiku muombe mungu sana
Naamin kwa hayo machache yatakusadia
 
Nimezunguka katika madhabahu za kiganga tofauti na jibu ni hilo hilo, ata kanisani nikiombewa mtumishi akitaja neno mahaba jini katika maombi mwili lazma utetemeke kama hali ya kupatwa na ubaridi
Huwezi changanya nuru na giza ukategemea matokeo chanya. Sikuhukumu mkuu, najua matatizo hupelekea mtu kutafuta suluhu kwa njia yoyote ile inayowezekana. Mambo ya waganga na imani ya kikistro ni vitu viwili tofauti.

Weka mkazo kwenye maombi, usijichanganye na mambo mengine.
 
stori yako hakueleweka umebaki kulalamika sana pili jini hafungi riziki ya mtu riziki hutoa mungu hakuna kiumbe wa kuizuia
Mzee kiimani tunasema Mungu ndie mpaji wa riziki na kila kitu ila tukija field nikuhakikishie sio jini tu hata binadamu mwenzako anaweza zuia usitoboe kwenye haya maisha...na achilia mbali kupata ugali wakula ila binadamu anaweza katisha hata maisha yako hapa duniani
 
Katika kusaidiana kupata msaada wa Mungu,mimi nina jambo ninalolifahamu ambalo ningependa kukupa naamini linasaidia sana,ni very powerful weapon katika vita hizi.
Nalo ni moja tu...JINA LA MWENYEZI MUNGU.
Jaribu kila usalipo utamke Jina halisi la Mwenyezi Mungu kumuomba msaada.
Na uwe unarudiarudia sala hiyo(iwe fupi) mara kwa mara hata utembeapo,uwapo ofisini etc.
Sijui wewe ni dini gani,ila mimi nafahamu Jina la YAHWEH mkuu,Muumba mbingu na nchi.
Sisi wakristo tunapomaliza kusali huwa tunasema KWA JINA LA BABA,MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
Sasa hapo mimi hutamka majina halisi,yaani YAHWEH,YAHSHUA na RUACH ELOHIM.
YAHWEH ni Jina kuu la Mwenyezi Mungu,maana yake MIMI NIKO(and bring everything into existence).Halafu YAHSHUA(YESU) maana yake ni YAHWEH NINAYEOKOA na RUACH ELOHIM maana yake ni Roho/pumzi/upepo wa Mungu wenye nguvu na uelekeo according to his purpose.
Ni upepo huu hutumika kupuliza pumzi ya uhai ambayo Mungu humpa kila mtu anapozaliwa.Ile pumzi inakuwa kama signature,yaani kusudi la Mungu juu ya mtu au kiumbe huyo,kusudio lake la kupewa uhai,kusudi hilo ndio wanajimu na wachawi huita nyota ya mtu.
Sasa hebu tafsiri hili unakuwa unamuita Mungu anayeishi(aliyepo),ambaye amekufanya uwepo,na anaweza kukutendea neno unalomuomba akalifanya likatokea(likawepo),akuokoe kwa kutumia nguvu yake ya kiungu (roho) ije kutenda kile ulichoomba but according to his will.(Huu upepo/Roho ndio tool ambayo Mungu anaitumia kufanya analotaka liwepo likawepo its a certain divine power,force.)
Matamshi haya pekee tayari ni mkataba kati yako na Mungu na sala itakayofuatia lazima itende kazi katika maisha yako kwa namna ya kipekee sana.Nazungumza kitu nilichokiexperience in real life.
Angalizo tu,huwezi kufikia kumuita Mungu kwa kiwango hiki halafu usiwe serious na ulichoomba.Ni jambo lenye uwajibikaji ndani yake.Imeandikwa Kila alitajaye Jina la Mungu na auache uovu.Na pia imeandikwa "Usilitaje BURE jina la Mungu".
Kama umeamua kufikia hatua hii basi uwe na shida yenye uzito wa kufanya hivyo, uwe rohoni umeamua kwa dhati ndipo umuite Mungu kwa staili hii.Vyovyote iwavyo majibu utayapata.Kama uko serious utapata majibu na pia kama hauko serious utayapata majibu yatakayokufanya uwe serious!
Sometimes tukiwa tumeelemewa sana hatuwezi hata kujiamini kutunga sala ili umfikishie Muumba wako.
Kama uko katika hali hiyo,unaweza tu kuchukua biblia,tafuta kitabu cha Zaburi,Soma Zaburi sura ya 10;1-17 kwa ajili ya kupambana vita na roho yoyote chafu.Unaposoma Zaburi hii kila penye neno BWANA sema "El Meez" maana yake "Mungu mtetezi wa wanyonge" na moyoni mwako ukimwona hivyo.Ukimaliza mwambie El Meez nisaidie mimi fulani mwana wa..(tamka jina la kwanza la mama yako).
Atakuja Ruach Elohim kukusaidia kwa nia ya Yahweh akiwa kama El Meez msaada wako.
Zaburi hii ya "kivita" iendane na Zaburi za toba (Zaburi 6 na Zaburi 25).Unaweza usiku kusoma zaburi hizi za toba na asubuhi kabla ya kuanza shughuli zako unasoma ile ya mapambano.Ufanye hivyo mpaka pale utakapoona nafsini mwako kwamba umeomba vya kutosha kilichobaki ni Mungu mwenyewe kujibu,then switch to Zaburi sura ya 8.Ni ya kushukuru,kusifu na kuabudu na kutambua mamlaka ya kibinadamu ambayo Mungu amekupa juu ya nchi na hakuna wa kukuondolea mamlaka hiyo.
Unairudisha mamlaka yako na akili zako kwa Muumba wako na wewe mwenyewe,badala ya kuhofu na kuwaza viumbe wengine walioumbwa kama wewe tu,na hawana cha kukufanya ukisimama na Mungu wako.

God bless you,na ushinde,ukaishi kwa Jina lake.
 
Back
Top Bottom