Pata ufahamu na elimu dhidi ya ugonjwa wa Mafindofindo (Tonsils) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pata ufahamu na elimu dhidi ya ugonjwa wa Mafindofindo (Tonsils)

Discussion in 'JF Doctor' started by Mahesabu, Jan 27, 2010.

 1. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Ugonjwa huu ambao kwa kiswahili zoelefu unajulikana kama "MAFINDOFINDO"hivi sasa umevamia watu wengi nikiwemo na mimi mwenyewe.

  Dalili nilizoanza nazo ni HOMA,KICHWA KUUMA,MWILI KUUMA,UCHOVU MKUBWA NA USINGIZI USIOISHA,KOO KUUMA(madonda kooni) mi nilidhani ni dalili za MALARIA.

  Nikaja kuta si mimi tu niliyekuwa naugua ugonjwa huu.Kila nimfahamuye anaponambia anaumwa ukimuuliza anakwambia ni "TONSES"

  Mpaka sasa ni zaidi ya watu 7(saba) wakiwa sehemu tofauti wanaugua ugonjwa huu.

  Japo onyo nililopokea ni kwamba USINYWE VITU VYA BARIDI lakini siku zote nimekuwa nikinywa kwa miaka sasa bila kupata dalili hizo.

  Hapa ndio nafikia kujiuliza na kuuliza umma, Je ugonjwa huu ni maambukizi?

  ======

  ============

  Swali kutoka kwa Emecka na majibu kutoka kwa Riwa


  Heshima mbele wana JF.

  Naomba kuuliza swali:

  Hivi mtu anapofanyiwa upasuaji "operation" ya tonsils halafu akang'olewa je kuna uwezekano wa ugonjwa kurudi tena? make kuna rafiki yangu alifanyiwa upasuaji mwezi wa nne kufika mwezi wa 7 zikarudi ikabidi akafanyiwe upasuaji tena.

  Je, inawezekana hiyo?
  ========== Baadhi ya majibu ==========


   

  Attached Files:

 2. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mahesabu, NDIO,MAFINDOFINDO NI AMBUKIZI

  HOW?

  Tonsilitis usually spread from person to person by contact with throat or nasal fluid of someone already infected

  HOW TO AVOID?
  1.make sure to keep your sick person's drinking glasses and eating utensils separate ans wash them in hot,soapy water
  2.All family members should wash their hands frequently.

  ============

  Tonsil husababishwa na sababu nyingi tu . Pia husababishwa na upungufu wa white blood cells katika mwili ambazo cells hizi ndio hupigana na vidudu vyote venye kuleta maradhi ndani ya mwili sasa vinaposhindwa kufanya kazi lymph zinavimba na husababisha Tonsils.

  Kila mtu na ukuwaji wake wa mwili, wapo ambao wanapata tonsils kwa kunywa maji ya baridi ambayo maji ya baridi huwa ni moja katika chanzo cha kupata tonsils, mavumbi huchangia vile vile pilipili na vitu vikali kama vile embe mbichi limau pia huwa ni sababu kuu ya kupata tonsil.

  Wakati unapokuwa na tonsils muhimu zaidi kuacha maji ya baridi na vitu vyote vikali, zaidi utumie maji ya moto

  Dawa za tonsils ni : kama ni mtumiaji wa dawa za chemicals basi epincilin inasaidia sana kuondosha tonsils.

  Dawa nyengine
  ambayo mimi binafsi naipendelea hii zaidi kwani inafanya kazi mara moja : Kamua ndimu moja katika glass yako kisha tia maji ya Uvuguvugu (warm water) na baadae tia vijiko vinne vidogo vya asali na kijiko robo cha chumvi kuroga uzuri na unywe pole pole

  Au Dawa hii Jaribu pia Dawa ya TONSILS ni kusukutuwa maji yaliokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala Tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto.

  Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia.

  Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako.

  Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafanya kazi na mdomo uko wazi basi pia unaweza kuumwa na Tonsils.

  Vile vile kutoka nje kwenye joto kisha ukaingia pahala baridi huwa inasababisha Tonsils na maradhi mengine kama flu na kuumwa na kichwa..n.k

   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,568
  Likes Received: 18,313
  Trophy Points: 280
  Nao hilo ni jibu la kidaktari.Mimi sio daktari, ila naweza sema ugonjwa huo ni ambukizi kwa watu wanaoambukizika kutokana na mambo ya kigenetiki. Nina watoto 5, wawili wa mama mmoja na watatu wengine wa mama mwingine. Hawa wawili mama mmoja ndio ambao hupata tonses na wala hawaambukizi hawa watatu wengine na wakiumwa hatuchukui tahadhari zozote.

  Hawa ambao hawapati ndio kiboko kwa kula barafu, tena mmoja anatafuna kama peremende na kumeza mabonge lakini hapati.... utafiti binafsi, sio wa kidakitari, nikagundua hawa wanaoumwa kwa mama yao ugonjwa huu upo, na hawa wasioupata kwao haupo kabisa. Ni sawa na magonjwa kama ulcers, pressure, mvi na upara, yatatokana na ukoo.

  Nimegundua kumbe hata uzee pia ni kuoo, ukiangalia kuna koo hawazeeki, na kuna koo just at 60 ni mzee wakutupa. Ila pia in every case, there is exceptionals.
   
 4. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Pasco

  kama ulivyosema kuwa wewe sio daktari,lakini kauli yako kuwa mafindofindo uweza ambukiza watu ambao wanafanana vinasaba ni sahihi,zipo reseach zilifanywa na kuthibitisha hilo,lakini hali hiyo haimanishi kwamba wale wenye vinasaba tofauti kama vya wale wanaougua hawawezi ambukizwa.Kama nilivyoeleza hapo juu,tunatakiwa tuchukue hizo taadhari ili kuepukana na maambukizi ya mafindofindo.
   
 5. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ndio unaambukiza na zipo njia nying za maambukizi moja ni busu la kubadilishan mate kwa wapenzi aka denda kama mmoja wapo ana umwa anaumwa mafundofundo basi mwenzi wake ni rahisi kuupata
   
 6. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na dawa yake?
   
 7. Willy

  Willy Member

  #7
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 78
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Tonsilitis ni ugonjwa kuvimba kwa tezi za shingo (tonsils) ambao unaletwa na bacteria pamoja na virusi. Asilimia kubwa inaletwa na bacteria wanaoitwa Streptococcus pyogenes. Bacteria hawa hushambulia tezi ambazo huvimba , kuwa nyekunde na kuwa na usaha. Kwa sababu unaletwa na vijidudu basi huambukizwa kwa njia ya droplets ( vimajimaji) vilivyo na hawa bacteria. Kwa kawaida ni ugonjwa wa watoto lakini inaweza kuwapata watu wazima.
  Willy
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbona hamsemi dawa nyie.....?
   
 9. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Dawa yake ni kunywa warm tea au unaweza tengeneza lemon juice na kunywa..........mafindo findo hata mie huwa napata mara kwa mara.Kama unasikia maumivu sana unaweza kunywa panadol kwa kutuliza maumivu.
   
 10. Willy

  Willy Member

  #10
  Jan 27, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 78
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 15
  Matibabu za tonsilitis inategemea the cause. The best iption ni kumwona daktari, hii ni kwasababu it is caused by many organisms including bacteria. Ni daktari ambayeanaweza kutofautisha. Pia inategema kama ni mara ya kwanza au ni chronic. Nikiwa kama daktari wa magonjwa I dont advice ule to dawa tu au unyem maji moto. Kama yalivyo magonjwa ya njia za juu ya hewa ni vizuri kuavoid vitu baridi. Tonsilitis inazo complication zake pamoja na kuaffect moyo (Rheumatic fever) ndiyo maana unahitaji kumwona daktari. Naona nikomee hapa.
  Willy
   
 11. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Hapa WILLY umenena. kwa mbali najisikia MOYO UNAUMAna mara chache KULIPUKA......!
  dawa niliyopewa mimi ni AZYWOK CAPSULES(azythromicin)

  ASANTENI WACHANGIAJI KWA DARASA NILILOLIPATA JUU YA UGONJWA HUU!
  JE UGONJWA HUU NI MLIPUKO(kama kipindupindu)?
   
 12. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  taska barrrrrrrrrrrriiiiiiiiiiiiiiiiiiidiiii!
   
 13. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Zimekusaidia?
   
 14. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ....he!he!he!he!he!....haya bana na bega kwa bega yako.....! ungesema Ulanzi mkangafu......!
   
 15. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  ZIMENISAIDIA...lakini dozi mbili, kwani ya kwanza baada ya kuisha zikaanza kurudi tena....ikabidi niji-prescribe dozi ya pili!
   
 16. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2011
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Dr. Heshima Mbele na wana JF

  Dokta tonses(mafindofindo) yakizidi yana madhara gani??

  kwa upande wangu ninayo hayo mafindofindo sasa yananisumbua sana muda na kila asubuhi nikipiga mswaki natema damu, na nikiwa nakula nashindwa kumeza napaliwa sana na msosi mpaka niweke maji pembeni. bado sijaenda hospital na nikiangalia yamevuimba sana.

  msaada wakuu nijue madhara niwahi kutibu ila nilishawahi kujaribu PEN V ikadunda hii inaponesha kwa muda. na kazini ni AC sasa sijui ni hii AC
   
 17. f

  fkstetes New Member

  #17
  Apr 1, 2011
  Joined: Feb 10, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wahi kikombe kwa babu Loliondo, matatizo yako yatakwisha
   
 18. BLISS

  BLISS Member

  #18
  Apr 3, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana.
  jaribu kusukutua na maji ya chumvi angalau mara 3 kwa siku yanasaidia sana.
  pia epuka kula vitu vya baridi kama maji yabaridi, na vyakula vinayowekwa kwenye jokofu,


  maumivu yakizidi pata ushauri kwa dakitari
   
 19. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  First Aid = Lamba asali mbichi kwa wingi tu, isizidi nusu kikombe cha chai.

  Halafu kamuone Dokta haraka sana.
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,059
  Trophy Points: 280
  Maneno hayo. Nimeshasikia wengine hufanyiwa operesheni ya kuyaondoa kabisa, lakini usithubutu kufanya hivyo maana nimeshasikia matukio machache ambapo wagonjwa waliokubali kufanyiwa operesheni kufariki.
   
Loading...