Ugonjwa wa Ngiri(Hernia), Dalili na tiba yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ugonjwa wa Ngiri(Hernia), Dalili na tiba yake

Discussion in 'JF Doctor' started by Polisi, Jun 27, 2011.

 1. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,090
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Wakuu,

  Habari ya kazi. Nilikuwa Bugando kwa ajili ya kufanyiwa kipimo kinachoitwa endoscopy. Matokeo yalikuwa kama ifuatavyo

  Esophagus – MILD DISTAL OESOPHAGISI 2”/HIATAL HERNIA
  Stomach - HIATAL HERNIA
  Duodenum – NORMAL
  Final Diagnosis - GERD 2” HIATAL HERNIA

  Sasa WIKI IJAYO nakwenda kuonana na daktari bingwa nimpe majibu haya. Kama mjuavyo watu ni wengi na hivyo kupata muda wa kujieleza na kudodosa vizuri kwa daktari inakuwa ni ngumu. Ndiyo maana nikaona ni bora nianzie hapa nipate mawili matatu mfano:

  - Kwa matokeo haya ya vipimo nitegemee nini kutoka kwa daktari
  - Baada ya kupitia humu jf nikagundua hiatal hernia ni ngiri, je inaweza pia kusababisha haya maumivu ya MIGUU na MIKONO?

  HALI YANGU KWA SASA
  Maumivu sehemu ya juu ya tumbo kama kuna kidonda ambayo yanapelekea maumivu hadi miguuni kwenye nyayo na mikononi. Maumivu yakipungua kifuani na miguu wala mikono haiumi. MAUMIVU PIA HUWA NAHISI MGONGONI

  HISTORIA YA TATIZO
  Ilianza mwaka 1998 baaada ya kupata stress sana. Ilitokea baada ya kuhisi kuwa msichana niliyetembea naye alikuwa ameathirika baada ya kumkuta amelazwa hospitalini na akadai anaumwa TB. Kwa kweli alikuwa amekonda sana. Kuanzia hapo mauza uza yakaanza kwa kukosa amani na mawazo tele. Mara tumbo, mara kifua mara miguu kuwaka moto nk. Hayo yote yalipelekea mimi kuconclude kwamba nimeathirika na sikutaka hata kujisumbua kupima

  Niliishi na hali hiyo kwa miaka karibu 4 yaani hadi katikati ya 2002 ndipo nilipopata ujasiri wa kwenda kupima. Nilianzia CBBRT negative, the same day nikarush ANGAZA negative. Nikamshukuru mungu. Maumivu makali yaliendelea yaani tumbo, kifua, miguu na mikono kuwaka moto n.k. Nikaenda Muhimbili na kufanyiwa kipimo cha BARIUM na kukuta nina ULCERS. Nikaanza masharti ya ulcers na dawa mbalimbali za kitalaam na zile za asili but changes zilikuwa kidogo sana. Nakumbuka nilikuja humu jf na kueleza tatizo langu na mchangiaji mmoja nadhani ni Riwa (sijui kama yupo huyu ndugu, sijamwona siku nyingi) alionesha wasiwasi wake kama kweli ilikuwa bado ULCERS kwa jinsi nilivyotumia dawa mbalimbali

  Mwaka 2011 nikarudi tena Muhimbili na kufanyiwa kipimo cha endoscopy na majibu yakawa nina oesophagistis fungus. X ray – normal na HIV negative. Nikapewa dawa awamu ya kwanza nikamaliza na dawa awamu ya pili kama aina nne hivi nikamaliza. Maumivu yakapungua kwa asilimia 50. Daktari mmoja aka-recommend tena nirudie endoscopy kwa kuwa ni HIV negative (Assumption kwamba hizo fungus huwapata walioathirika). Ndiyo maana nikaenda tena hosptali


  =========

  [​IMG]

  Kuna magonjwa ya hernia ya aina nyingi kama zile ziitwazo kitaalamu inguinal, umbilical, femoral, epigastric, incisional, inguinal hernia na diaphragmatic hernia.

  Lakini watu wengi hukumbwa na hernia iitwayo inguinal hernia ambayo hutokeza karibu kabisa na sehemu ya siri ambako hapa kimrija kinachochukua mbegu za kiume kutoka kwenye korodani na kuingia kwenye tumbo na kuingia kwenye kiungo cha kiume.

  Hapa panaweza kuwa na uwazi na uwazi huo ukaingia utumbo mdogo na kusababisha hernia hii. Aina hii ya hernia kama nilivyosema hapo juu ndiyo inayosumbua sana watu wengi duniani. Kuna aina nyingine ya hernia inayoweza kutokea kwenye kitovu, sehemu ambayo kunakuwa na mshipa unaopitisha damu yenye chakula na hewasafi ya oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni.

  Sehemu hiyo mtoto anapozaliwa panaweza pasijifunge vizuri, hivyo mtoto huyo kupata hernia hii baadaye kwani utumbo mdogo huingia katika kijinafasi hicho kisichojifunga vizuri, hivyo kusababisha uvimbe wa hernia hii. Lakini tatizo hili ikiwa mtoto amezaliwa na akaishi zaidi ya miaka miwili bila kujitokeza tena, basi atakuwa salama kwa sababu kwa muda huo sehemu hiyo huwa imejifunga kabisa.

  TIBA
  Ikitokea sehemu hiyo ikaacha kujifunga kwa kipindi hicho cha miaka miwili, basi daktari huamua kumfanyia upasuaji mtoto huyo. Kwa watu wazima hernia kwenye kitovu ambayo kitaalamu huitwa umbilical hernia inaweza ikatokea kwa akina mama wenye mimba au kwa wale ambao ni wanene kupita kiasi kwani presha kwenye tumbo inakuwa kubwa na kufunga sehemu hii ya kitovu ambayo inawezekana awali ilikuwa wazi.

  Hernia nyingine huweza kutokea kwenye kiungo cha njia ya kumezea chakula kinapoungana na tumbo. Kama sehemu hii haikufunga vizuri utumbo unaingia kwenye kinafasi hicho na kujitokeza kwenye kimfuko kilichopo kifuani kinachoitwa kitaalamu diaphragm.

  Ndiyo maana hernia hii huitwa diaphragm hernia.
  Hernia nyingine iitwayo femoral hernia hutokea pale mishipa ya damu iendayo kwenye mguu inapopita kwenye tumbo na ikiwa kwenye maungio pana nafasi basi hernia hii hutokea kwenye paja karibu na kiunoni.

  Kuna hernia ingine inayotokea kwenye chembe ya moyo ambapo misuli inaachia na kusababisha kingozi cha tumbo na utumbo kuingia katika sehemu hiyo hivyo kuvimba na kusababisha hernia.

  Tiba za uhakika za hernia ni kufanyiwa upasuaji kama tulivyofafanua hapo juu.

  ======

  UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE)
  Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

  Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji. Ugonjwa huu wa ngiri unawapata wanaume na wanawake wa rika zote. Mshipa wa ngili ni jina linalokusanya magonjwa kama Ngiri kavu (Hernia), Ngiri maji (Hydrocele) na Ngiri nyinginezo kama vile kuvimba kokwa au mfereji unaopitisha manii unaojulikana kitaalamu kama Epididmorchitis.

  Ngiri Kavu (Hernia), aina hii ya ngiri huwapata wanawake na wanaume wote kwa ujumla. Ngiri kavu inapompata Mwanamke huitwa Fermoral Hernia, na pindi inapompata mwanaume inaitwa Scrotal hernia. Kwa maana halisi ya ngiri au mshipa wa ngiri ni hali inayotokea katika mwili wa binadamu ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili. Sehemu hiyo inayoathiriwa mara nyingi huwa ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

  Pamoja na hivyo mshipa wa ngili hujitokeza sehemu mbalimbali za mwili na hupewa majina tofauti kutokana na sehemu ulipojitokeza, kwa mfano ngiri ya tumbo inajulikana kitaalamu kama Abdominal Hernia, pia watoto wanaozaliwa na vitovu vikubwa inaitwa Umbilical Hernia, na pale ngiri inapojitokeza katika sehemu ya haja kubwa inaitwa Anal Herni. Dalili zake hazitofautiani sana hata hivyo ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote isipokuwa kuna baadhi ya ngili hujitokeza na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza.

  Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa wa mwili wa kupitiliza au kuongezeka uzito kwa ghafla, pia kua na kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.

  Mojawapo ya dalili za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
  • Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
  • Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.

  • Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
  • Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.
  Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

  ======

  Ugonjwa wa ngiri ya kitovu (Umbilical Hernia)

  Hili ni tatizo la kiafya ambalo huathiri ukuta wa tumbo na kitovu. Tatizo hili husababishwa na mambo makubwa matatu; kwanza ni kasoro ya kuzaliwa. Hapa ni kwamba kitovu kinakuwa na kasoro tangu pale mtoto anapokuwa tumboni kabla hajazaliwa.

  Tatizo hili kwa watu wazima lipo mara tatu zaidi kwa wanawake ukilinganisha na wanaume ambapo lipo kwa kiasi kidogo sana. Kwa watoto kiwango cha tatizo hili vinalingana kwa wote wa kike na wa kiume na tafiti zinaonesha kwamba, tatizo ni kubwa kwa watoto wa Kiafrika ukilinganisha na mataifa mengine.

  Aina ya pili ya tatizo hili ni ngiri ya kitovu. Hii inatokea tu pasipo na kasoro za kuzaliwa nazo. Hili linatokea kutokana na shinikizo la mgandamizo wa hewa na nguvu ndani ya tumbo kunakosababishwa na unene kupita kiasi, kunyanyua mizigo mizito au vitu vizito mara kwa mara, kikohozi cha muda mrefu na ujauzito wa mimba ya mapacha kwa mwanamke.

  Aina ya tatu ya ngiri ya kitovu inaitwa ‘Paraumbilical hernia’. Aina hii ya ngiri hutokea zaidi kwa watu wazima na husababishwa na kasoro upande wa juu wa kitovu kuelekea kwa juu kufuata mstari wa kati wa tumbo.

  DALILI ZA UGONJWA
  Ngiri hutokea katika eneo la kitovu ambacho kwa lugha nyingine huitwa ‘Umbilicus’, ‘navel’ au ‘Belly button’. Kwa watoto wachanga wanapozaliwa kitovu huwa kirefu sana na huungana na kondo la nyuma la mama ili kupeleka lishe na hewa ya oksijeni kwa mtoto anapokuwa tumboni.

  Baada tu ya kuzaliwa, mtoto hujitegemea hivyo kitovu hukatwa katika eneo maalum ili kipungue urefu. Baada tu ya kitovu cha mtoto kupona, mtoto anaweza kupatwa na tatizo hili la ngiri ya kitovu tangu anapokuwa mtoto mchanga ambapo akilia kitovu kinatokeza juu na anaponyamaza kinarudi ndani.

  Hali hii wakati mwingine humsababisha mtoto apatwe na maumivu makali huku akilia kila wakati.

  Aina hii ya ngiri huwa haipasuliwi kwani huisha yenyewe baada ya miaka miwili hadi mitatu, lakini baada ya umri huo kama haikuisha basi mtoto atafanyiwa upasuaji kurekebisha.

  Endapo mtoto ngiri hiyo itakuwa inamsumbua kabla ya umri wa miaka mitatu, basi hatapasuliwa bali itafanyiwa utaratibu wa kuirudisha kitaalam ili isiendelee kutokeza na kuleta maumivu. Ngiri inapokuwa kubwa, tundu lake huwa haliongezeki hivyo husababisha matumbo na kila kitu kitachomoza na kubana nje kushindwa kurudi ndani na kusababisha hali iitwayo ‘Strangulation’.

  Kama hali hii haitatibiwa mapema basi italazimika upasuaji wa dharura na ikichelewa huweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa. Tatizo hili hutokea hata kwa ngiri nyingine ambazo tutakuja kuziona katika matoleo mengine.

  UCHUNGUZI
  Ngiri ya kitovu huonekana kwa macho pale inapochomoza ambapo dhahiri itaonesha imechomoza, wakati mwingine mgonjwa atalalamika maumivu na kama ni mtoto atakuwa analia mara kwa mara.

  Vipimo vingine vitategemea na daktari kadiri atakavyoona inafaa.

  MATIBABU
  Matibabu ya ngiri ni kupasuliwa, haishauriwi kufungia sarafu kwani inaweza kukosewa na kusababisha sehemu ya utumbo kubanwa au kuleta maambukizi ya ngozi kwenye kitovu. Kwa mtoto huisha yenyewe taratibu na ikibidi hupasuliwa baada ya umri wa miaka mitatu.

  Wakubwa ni lazima ipasuliwe kama inaleta shida. Wahi hospitali ya mkoa kwa uchunguzi na tiba

  ======

  Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

  Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).


  Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

  Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

  Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni).

  Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

   
 2. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana JF niko serious na wala ctanii, na naombeni mnipe ushauri utakaonisaidia mwenzenu. Imetokea kuwa nasumbuliwa na ugonjwa wa ngiri na hapa nilipo nackia maumiv c kawaida. Imepelekea mpaka sehemu 1 ya yai la kushoto kwenye uume ina mishipa yenye uvimbe najihic ni utumbo umezama huko nikishika. Nilienda hsptl doctor akanipa 2 vidonge ambavyo havikunisaidia. NAOMBENI USHAURI KWA ANAEJUA DAWA YAKE NIWEZE KUPONA MANAKE NIMEKATA TAMAA YA KUPONA. Nakaribia mwaka nikiwa na haya maumiv.
   
 3. s

  stan b Member

  #3
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hiyo ndugu yangu dawa yake ni opreshen, hlo ni tatizo ambalo wanaume wengi huzaliwa nalo, gharama yake si chin ya elfu 50, baada ya opreshen huitajik kufanya tendo la ndoa miezi 6 wala kaz ngum. uckubal kudanganyika na dawa za kienyeji onana na madaktar hospital kubwa za serkal.
   
 4. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Asante sana mkuu kwa ushauri.
   
 5. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,043
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Pole sana,wengi hupona kwa upasuaji so nenda hospitari.
   
 6. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,838
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  jitahidi kuzingatia hapo kwenye red
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Sep 30, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,934
  Likes Received: 6,577
  Trophy Points: 280
  Ndugu God bell,
  Pole kwa maumivu.

  Kwanza niseme kuwa kwa kiswahili bado kuna mkanganyiko wa neno Ngiri. Wapo wanoiita ngiri kwa maana ya busha (hydrocele), na wengine huita ngiri (Hernia) ambayo ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwasababu ya kuwa l'oose'

  Kwa maelezo yako nadhani unaongelea abdomen hernia ambayo sehemu ya utumbo hutumbukia katika hasua. Hii ni kwasababu sehemu inayozuia (kiwambo) inakuwa imeachia. Utumbo huingia huko na kukuletea maumivu. Siyo maradhi yanayosababishwa na wadudu, hutokea hata kwa watoto wadogo au watu wazima ambao hufanya kazi za nguvu n.k.

  Hakuna dawa inayotibu bali zinazopunguza maumivu. Mara nyingi ukilala na taratibu kusukuma hicho unachokihisi kurudi juu, basi hali inaweza kutulia. Itajirudia tena tena kwasababu umesogeza tu lakini hujazuia.

  Matibabu yake ni operesheni ya kufunga sehemu hiyo. Matibabu hayo ni muhimu sana kwasababu inaweza kutokea kuwa utumbo umeingia ukajikunja na kushindwa kupitisha damu (strangulated hernia) hivyo sehemu hiyo itaoza na kuweza kuleta madhara makubwa zaidi tusiyotarajia.
  Hutokea nadra lakini inapotokea hujui utakuwa sehemu gani ya huduma muhimu na za haraka hapo unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana kimaumivu na pengine kimaisha.

  Tafadhali kawaone madaktari katika hospitali kubwa kwa ushauri zaidi.
   
 8. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Ubarikiwe mkuu kwa ushauri wako mzuri.
   
 9. Chrizo

  Chrizo JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 80
  Samahani wana jf nilikuwa napenda kujua hernia ni ugonjwa gani na husababishwa na nini,pia dalili na matibabu yake ni yapi. Nawasilisha
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,143
  Likes Received: 577
  Trophy Points: 280
  kwa kiswahili wanaita NGIRI


  nadhani hukukwepa umande


  [h=3]Hernia Causes[/h]Although abdominal hernias can be present at birth, others develop later in life. Some involve pathways formed during fetal development, existing openings in the abdominal cavity, or areas of abdominal-wall weakness.
  • Any condition that increases the pressure of the abdominal cavity may contribute to the formation or worsening of a hernia. Examples include
   • obesity,
   • heavy lifting,
   • coughing,
   • straining during a bowel movement or urination,
   • chronic lung disease, and
   • fluid in the abdominal cavity.
  • A family history of hernias can make you more likely to develop a hernia

  [h=3]Hernia Symptoms and Signs[/h]The signs and symptoms of a hernia can range from noticing a painless lump to the severely painful, tender, swollen protrusion of tissue that you are unable to push back into the abdomen (an incarcerated strangulated hernia).
  • Reducible hernia
   • It may appear as a new lump in the groin or other abdominal area.
   • It may ache but is not tender when touched.
   • Sometimes pain precedes the discovery of the lump.
   • The lump increases in size when standing or when abdominal pressure is increased (such as coughing).
   • It may be reduced (pushed back into the abdomen) unless very large.
  • Irreducible hernia
   • It may be an occasionally painful enlargement of a previously reducible hernia that cannot be returned into the abdominal cavity on its own or when you push it.
   • Some may be chronic (occur over a long term) without pain.
   • An irreducible hernia is also known as an incarcerated hernia.
   • It can lead to strangulation (blood supply being cut off to tissue in the hernia).
   • Signs and symptoms of bowel obstruction may occur, such as nausea and vomiting.
  • Strangulated hernia
   • This is an irreducible hernia in which the entrapped intestine has its blood supply cut off.
   • Pain is always present, followed quickly by tenderness and sometimes symptoms of bowel obstruction (nausea and vomiting).
   • The affected person may appear ill with or without fever.
   • This condition is a surgical emergency.
   
 11. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  umetusaidia na sisi pia! eimen!!
   
 12. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,597
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Well summarized Edson...
   
 13. Chrizo

  Chrizo JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 470
  Likes Received: 317
  Trophy Points: 80
  ahsante mkubwa ubarikiwe
   
 14. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Could u summarize is kiswahili so we can understand all of us. Thankx mkuu.
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,229
  Likes Received: 4,019
  Trophy Points: 280
  Kwanza niseme kuwa kwa kiswahili bado kuna mkanganyiko wa neno Ngiri. Wapo wanoiita ngiri kwa maana ya busha (hydrocele), na wengine huita ngiri (Hernia) ambayo ni sehemu ya viungo kuingia sehemu nyingine kwasababu ya kuwa l'oose'

  Kwa maelezo yako nadhani unaongelea abdomen hernia ambayo sehemu ya utumbo hutumbukia katika hasua. Hii ni kwasababu sehemu inayozuia (kiwambo) inakuwa imeachia. Utumbo huingia huko na kukuletea maumivu. Siyo maradhi yanayosababishwa na wadudu, hutokea hata kwa watoto wadogo au watu wazima ambao hufanya kazi za nguvu n.k.

  Hakuna dawa inayotibu bali zinazopunguza maumivu. Mara nyingi ukilala na taratibu kusukuma hicho unachokihisi kurudi juu, basi hali inaweza kutulia. Itajirudia tena tena kwasababu umesogeza tu lakini hujazuia.

  Matibabu yake ni operesheni ya kufunga sehemu hiyo. Matibabu hayo ni muhimu sana kwasababu inaweza kutokea kuwa utumbo umeingia ukajikunja na kushindwa kupitisha damu (strangulated hernia) hivyo sehemu hiyo itaoza na kuweza kuleta madhara makubwa zaidi tusiyotarajia.
  Hutokea nadra lakini inapotokea hujui utakuwa sehemu gani ya huduma muhimu na za haraka hapo unaweza kujikuta katika wakati mgumu sana kimaumivu na pengine kimaisha.

  Tafadhali kawaone madaktari katika hospitali kubwa kwa ushauri zaidi.
  source:
  https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/177748-ugonjwa-wa-ngiri.html
   
 16. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mkuu nashukuru kwanza kwa kukubali kubadilisha hiyo lugha ya kingereza kuwa kiswahili kwa faida ya wengi. Nakumbuka mwezi ulopita niliweka thread kama hii nikiwa nasumbuliwa na huu ugonjwa wa ngiri. Nimeshaonana na doctor na ameniambia nahitaji upasuaji. Hivyo ndo najiandaa kwa operation. Asanteni kwa wale walotoa mchango wao wa kunishauri.
   
 17. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #17
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,454
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Wakuu nina tatizo la kutopata choo(Nikifika chooni mzee anafika mpaka dirishani lakini hatoki ng'o) wakati wa baridi au nikipigwa na baridi kama ya ac, sometime nikinywa maji ya baridi. Ukienda hospitali wanakupa dawa za constipation. Daktari huwa wananiambia niwe nakunywa maji na kula matunda sana. Ukweli ni mlaji sana wa matunda na kunywa maji yasipongua lita 3 kwa siku.

  Katika uchunguzi wangu nimegundua kwamba tatizo hili hutokea wakati nikihisi hali ya ubaridi kama nilivyoelza hapo juu, nimegundua kwamba hii itakuwa ngiri tu ingawa sihisi chochote kuvimba kwenye mwili wangu.

  Nani anajua dawa ya tatizo hili. Kama ni ngiri je ipi ni tiba yake ya kudumu acha hizi za muda

  Nawasilisha
   
 18. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #18
  Mar 22, 2012
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nenda Pale Eneo la Temeke Vetenary kuna kituo cha Mafuta OIL COM, next building ni msikiti, unaitwa Masjid Iman. Ukifika hapo utaona kuna kibanda kidogo geti la kuingia msikitini. Hapo kuna jamaa anauza dawa za miti shamba. Kuna dawa ya mchanganyiko wa miti mbalimbali inaitwa MIDDLE FILDER. Ukiitumia dawa hiyo naamin tatizo lako litaisha. Naomba usidharau kama kweli unatatizo hilo.
   
 19. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,454
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Mkuu nashukuru sana. Tatizo lipo.Nitalifanyi akazi mkuu. Nikirudi nitakubrief
   
 20. ldd

  ldd JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 791
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Dawa yake ndgo husinywe maji na vingine vya baridi!
   
Loading...