PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
“Natarajia muda mfupi ujao, Inshaallah nitakuwa Rais wa Zanzibar" - Maalim Seif Sharif Hamad
MAALIM SEIF AJIPA MATUMAINI
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad bado anaamini atakuwa Rais wa Zanzibar akidai kwamba nchi alizopeleka malalamiko yake zimefikia katika hatua nzuri.
Maalim Seif ajipa matumaini
Toa maoni yako?
======
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Shariff Hamad amesema kwamba mpaka pale yeye atakaposhinda Urais wa Zanzibar na kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa chini ya chama chake ndio ataweza kuacha kugombea nafasi hiyo ya Urais katika chaguzi zitakazofata.
Ameyasema hayo jana alipokuwa kwenye mahojiano na Tido Mhando katika kipindi cha “Funguka” kinachorushwa na Azam Tv.
“Ngoja kwanza nipate haki yangu. Nikishapata haki yangu, CUF ikaongoza serikali ya Zanzibar, Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika uchaguzi unaokuja, hapo nitafikiria – lakini sasa ni lazima tupate haki yetu kwanza.” Alisema Maalim.
Alipoulizwa kwamba kung’ang’ania yeye tu kuwa mgombea urais katika chaguzi zote na kwamba kambo hili lina maslahi binafsi zaidi kwake tofauti na utaifa, alikana na kusema, “Mimi nimewaahidi Wazanzibari kwamba nitawatumikia, kwamba tutapata haki yetu. Tukishaipata haki yetu na mimi nikawa Rais wa kuongoza serikali ya umoja wa kitaifa, sasa uchaguzi mwengine utaona mambo yatakuwa vipi.
Alipoulizwa endapo ikifika mwaka 2020 atatangaza kugombea urais wa Zanzibar kwa mara ya sita, Maalim, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 73 alijibu kuwa inabidi jambo hilo lisubiri wakati wake kwanza kuona kama tumefanikiwa au hatukufanikiwa, baada ya hapo tunaweza kufanya maamuzi. Kugombea 2020 ni jambo ambalo inabidi tusubiri muda ufike na tuangalie hali halisi ya kisiasa ya wakati huo.