Mkuu mimi pia ni mwalimu, wa secondari, kwa ngazi ya A level nina mwaka moja tu kazini ila nilichokigundua kwa waalimu wenzangu nikuwa waalimu wengi hawawezi kujiamini katika madai yao kwa sabasu zifuatazo;-
- asilimia 75 ya waalimu wamepata kazi hiyo kwa njia sizizo halali yaani ni unqualified teachers since wameungaunga tu kielimu na kusaidiwa na ndugu najamaa kupata nafasi hizo.
- nikweli wengi wetu wanamatokeo mabovu hasa form four na form six wengi utakuta walipata division 4 za point 26,27,28 , wakaaanzia certificate wakasoma vidiploma vya kuunga unga mpaka degree. so hii ina wa fanya wa na kuwa na lack of confidence.
- Waalimu wengi ni wavivu wasiopenda kujituma kutambua kuwa maisha ni zaidi ya mshahara na hakuna tajiri aliye ajiriwa bali matajiri halali wote duniani wame jiajiri wenyewe kwa kuanza na idea ndogo ya kibiashara iliyo tiliwa mkazo na kuwa kubwa. ndomaana wallimu wengi ni masikini wakutupwa, kwakutokujua umuhimu wa kuwa wajasiliamali
- waalimu wengi ni wanafiki, wenye majungu na watu wakujipendekeza pendekeza wanaopenda kukaa staffroom na kusemana wao kwa wao bila kufikiri muda ni pesa hivyo kupoteza muda wao mwingi kujadili yasiyo yamsingi
nikweli kuwa waalimu tunamazingira magumu lakini ugumu mwingine tunao wenyewe ni wakujitambua. tutambue kuwa kidogo unachokipata ukikitumia vizuri waweza fanya makubwa, uta shangaa mwalimu ngazi ya degree ana lipwa kiasi cha shilingi 435000/= take home, nikweli kwako ni kidogo kwani wapo watumishi wanaolipwa zaidi ya hapo na malupu lupu juu, wakiwa elimu yao ni ndogo na ni wewe uliye wafundisha na kuwafanya wafike hapo, na wewe jiongeze fanya kazi kulingana na malipo yako, jifanyie miradi midogomidogo mingi mwisho wasiku utaona faida yake, cwt ni tawi la hao hao sirikali, ukitegemea msaada wao na wewe utajenga nyumba kwa hela za kustaafu kwani waalimu wengi ndo mtindo wetu, kama nikijana jitume fundisha kadri ya uwezo wako, fikiri nje ya mshahara, tafuta pesa, watanzania wenyewe bado usingizi mnene matoto yetu yenyewe huku shuleni hata ulifundisheje lenyewe ni facebook, twitter, whatsup, club kwa sana, mabinti ndo usiseme yaani ni kujiachia.
ukiwagusa watoto labda kuwanyang'anya sim au kuwapa adhabu, wazazi wanakuja wana kuchimba mkwara diwani nae anakufata na kukupiga mkwara eti atakufukuza kazi, matoto hayaji na madaftari sikuhizi ni headphones kwa kwenda mbele, wazai wao wana waona wana waacha. mwalimu acha kuji chosha do what you have to do, na rudia tena kwa hali hii ha kuna wito fanya kazi kulingana na bei unayo lipwa.