kaligopelelo
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 2,766
- 3,940
😄😄😄 Wamewatesa Sana Babu zetu na athari zinaendelea kutesa kizazi na kizazi. Wameiba mali nyingi SanaNa hali ilivyo ngumu tulipwe tupate mitaji aiseee
Cha msingi watulipe kwanza hayo mengine yatafuata.Hata tukilipwa litakuwa suala la muda tu,tutarejea katika umaskini kwa kasi ya ajabu.Tatizo la Afrika ni uongozi mbovu.
Kama ingekubalika natamani mgao ugawiwe kulingana percentage ya athari za ukoloni katika taifa husikaHuo mgao wa malipo utatufikia kweli na sisi huku nanjilinji au ndiyo utapigwa juu kwa juu?
😄😄 Hatari sana,hili taifa linahitaji maombi sanaMi naona wawalipe hao wengine,sisi wasubirie kwanza,kwasababu hata zikija,sintafaidika nazo,zitaingia mifukoni mwa watu walewale wanaokula keki ya taifa,huku tukishuhudia,na bahasha zao zinazoandikwa SIRI.
Endelea kuagiza,waambie hela wataleta wakoloniNimeshaagiza zangu double kick nimekaa pale naendelea kunywa nikisubiria mgao wangu wa ukoloni nilipe bill
Inahitaji kujitambua na kuacha kuwa tegemeziAs if ukoloni umeshaisha Afrika? Nana Akufo angali ndotoni naoni. Waambieni kwanza Wakoloni waiachie kabisa Afrika itoke mikononi mwao.
Kabisa,yaani maisha yananipelekesha,nafanya kazi kwa bidii kutafuta mtaji lakini wapi,kwasababu dependants ni wengi na suwezi nikasema nisiwasaidie,maana ni ndugu zangu,naomba ajira TAMISEMI,wanachukua wa 2020,2021,wananiacha mimi,naomba sensa,wanapeana kimchongo,sasa hizo pesa eti zije,si zitaliwa tu.....?😄😄 Hatari sana,hili taifa linahitaji maombi sana
Naunga mkono hoja hii, ni muhimu Sana Afrika nchi za Ulaya kuilipa Afrika fidia walau kila mtu milioni 50 , kwa kuwafuta waafrika machozi ju ya uharibifu walio ufanya ndani ya Afrika.Ifike wakati Sasa Afrika tuungane Katika kutetea masilahi yetu. Linapokuja suala la Afrika lisiachwe liwe la mtu mmoja,au taifa moja.
Afrika tuoneshe kujitambua.View attachment 2325477
Mi nadhani lengo sio kutajirika,kikubwa hapo ni kurejesha fidia ya uharibifu na wizi walioufanya. Haiwezi kulipia machungu na maumivu waliuopitia waafrika ila ni inasaidia kuwajulisha watesi wetu kuwa walichokifanya hakikuwa sawa.... katika vyote ameona kulipwa "fidia" ndiko kutaikwamua Afrika? Kwa zaidi ya miaka 60 ya uhuru wa Afrika, bara hili limepokea mabilioni mangapi ya dola? Yameifikisha Afrika wapi? Badala ya ku-hit kiini cha tatizo, anajizungushazungusha tu kama kawaida ya viongozi wa Afrika.
Mwl. Nyerere alituasa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne tu - ardhi, watu, siasa safi, na uongozi bora - fedha (fidia) sio miongoni mwa mahitaji hayo. By the way, wasingekuja wazungu (na waarabu) Afrika ingekuwa na hali mbaya sana kuliko iliyo nayo sasa.
Tutalipwa tu,muda ukifika wahuni wote wanaotutesa Sasa hivi tutawaburuza mahakamani,na ndio maana hawaitaki katiba mpya.