Natamani sana kuolewa. Ni tatizo au?

Natamani sana kuolewa. Ni tatizo au?

Pole sana. Ila kwanini uliachana na huyo mtu?
 
Hakuna haja ya kukata tamaa ingawa sijui umri wako kaa ufurahie maisha kwanza mume atakuja tu jiweke busy tafuta fursa ujiweke juu zaidi kiuchumi mume atakuja hata na miaka arobaini utaolewa tu muhimu waepuke mabazazi wasije kukuachia kibendi uhangaike nacho
 
Usikate tamaa, kuna nuru gizani bidada.
 
Hahaaaa!!
Mwanaume kutokuwa na kazi si dhambi ila ndio huwezi hata kujishughulisha!?
Mtu kuanzia panakucha mpaka kiza kinaingia unahama viti tu na remote mkononi,hujigusi hata!!!
Kuna wanaume wengine hawana kipaji cha kuchacharika ( hasa wale ambao hawajapita kwenye mishemishe ya kiume ambayo mnatafuta mkipata wote poa akipata mmoja anam-support mwenzake kwa siku hiyo)
 
Next year unaolewa..............document my words please
 
Wakati mwingine tunapitishwa kwenye mahusiano kwa lengo la kujifunza hivyo basi wa kwako yupo, kaa chini tulia na yale mabaya aliyokufanyia yachukulie kama changamoto na funzo ili siku nyingine yakutokee. Wakati mwingine tunaletewa matatizo ili tuweze kutafakari na kutambua haya mambo yapo hivyo hata siku nyingine ukipata mwingine tayari umekuwa strong. (embu takari kidogo "kama ingetokea amekuoa alafu matatizo yanatokea kwenye ndoa ungekuwa katika nafasi gani"​. TAKE IT EASY
 
Je, we ni wakike au wakiume?

Kama ni wakike sidhani kama hilo ulilonalo ni tatizo, ila kama ni wakiume hebu fika reherb

Duuuu!!!!!kweli bado tuna safari ndefu, tatizo kusoma heading tu, ingawa hata heading inaeleza jinsia ya mtoa mada, hatuna ukameron nchini ili kusema ni dume linalotamani kuolewa.
 
Kuolewa kweli kwa wamama ni issue,jana rais wa korea kusini nae ni mmama,hana mme wala mtoto,basi korea ya kasikazini wamempaka mabango eti anahonga uchi kwa pimp Obama ili obama aishambulie northkorea.udhalilishaji mkubwa just because bado yuko single na umri ushaenda.
 
Je, we ni wakike au wakiume?

Kama ni wakike sidhani kama hilo ulilonalo ni tatizo, ila kama ni wakiume hebu fika reherb

Anasema anatamani kuolewa unauliza kama ni KE au ME. Au ndoa za jinsi moja zimeishaingia Bongo? Mungu apishie mbali
 
Hahaaaa!!
Mwanaume kutokuwa na kazi si dhambi ila ndio huwezi hata kujishughulisha!?
Mtu kuanzia panakucha mpaka kiza kinaingia unahama viti tu na remote mkononi,hujigusi hata!!!
Haya, unaona sasa....????? Na haya umeyaongea wakati umecheka kidogo, je ukikasirika hadi chozi linakutoka, utatamka nini..??? Wanawake...!!
Na ukiwa unafanya kazi nayo shida... utasikia... haya uchague moja kazi au familia... YAAANI..mhnn

 
Nakupa pole sana Dada lakini kaa ukijua lolote gumu linalomkabili mwanadamu jibu lipo cha msingi usikate tamaa...ebu jiulize ungeenda kwa Doctor kucheki afya majibu yakaja umeathirika kipi bora kuwa mzima alafu uko single au ni mwathirika alafu upo na mwenzako kwenye ndoa...jipe moyo ktk Bwana usiogope Majibu yako yanakuja.
 
Kuna wanaume wengine hawana kipaji cha kuchacharika ( hasa wale ambao hawajapita kwenye mishemishe ya kiume ambayo mnatafuta mkipata wote poa akipata mmoja anam-support mwenzake kwa siku hiyo)

Wa hivyo ni kuzichanga nimnunulie hata gunia moja la mkaa auze kwa kupima!!!!
 
Wa hivyo ni kuzichanga nimnunulie hata gunia moja la mkaa auze kwa kupima!!!!
Tatizo lingine tena watu wa design hiyo wapo selective na kazi, mtu hana hela lakini anajiweka katika pozi la ukurugenzi wakati kazi za kusomea ramani zipo kibao wakati unatafuta ile unayoitaka "mtu anashindwa kutafuta hata ka-laptop kimeo na kupiga mishemishe ya kuingiza nyimbo kwenye simu au hata kuwa dalali tu ambapo mtaji ni suruali 4 na mashati 4 mazuri na nadhifu ya kuanzia ili ku-build trust kwa wateja"
 
Haya, unaona sasa....????? Na haya umeyaongea wakati umecheka kidogo, je ukikasirika hadi chozi linakutoka, utatamka nini..??? Wanawake...!!
Na ukiwa unafanya kazi nayo shida... utasikia... haya uchague moja kazi au familia... YAAANI..mhnn

Imebidi nicheke sasa!!!
Namhimiza ajiongeze kiroho safi tu ili twende sawa,wanaume wasio na kazi wala pa kujishikiza wana gubu kama ndugu wa mume na lawama kama watoto wanaolelewa na ndugu!!! Akikosea usiongee kisa atalalamika ananyanyaswa. Ukikutana na issue juu kwa juu inataka maamuzi ya haraka ukaifanya then ndio uje kumwambia atakwambia umemdharau,ukimpa maagizo msichana ya nini kipikwe atadai analishwa makapi kisa hanunui ukimuuliza atakula nini mchana anakwambia tunakoelekea utamtuma sokoni!!!
Ni shidaa!!!
 
hehehehehe kantangaze, mwanaume anahama na kivuli cha mpapai saa moja kilikuwa hapa na yeye yupo saa saba kipa kule na yeye kaenda!
 
Tatizo lingine tena watu wa design hiyo wapo selective na kazi, mtu hana hela lakini anajiweka katika pozi la ukurugenzi wakati kazi za kusomea ramani zipo kibao wakati unatafuta ile unayoitaka "mtu anashindwa kutafuta hata ka-laptop kimeo na kupiga mishemishe ya kuingiza nyimbo kwenye simu au hata kuwa dalali tu ambapo mtaji ni suruali 4 na mashati 4 mazuri na nadhifu ya kuanzia ili ku-build trust kwa wateja"
Sasa huyu mkurugenzi wa remote ukimtia masingi utaambiwa unamnyanyasa?
CC Ngalikihinja
 
Last edited by a moderator:
endelea kumuomba Mungu sana, nadhani hakuna mtu aliyewahi kuumia kama mimi, nilichumbiwa na kijana mpole sana na kabila ni muhaya na kila alichokuwa nafanya nilijua ni kweli, kumbe alikuwa anaigiza tuu, baada ya uchumba akabadilika hata wale ndugu aliowaleta siku ya uchumba hawakuwa ndugu zake pia hata kabila halikuwa lake na kila nikienda kwa ndugu zake hawakuwa ndugu zake yaani ulikuwa kama mchezo wa kuigiza tuu, baadae nikajua ukweli na hapo alikuwa ameshanifanyia ukatioli wa kila aina, huyo kaka alikuwa mkurya wa majimoto kiukweli sitasahau yale maisha, wazazi wakaniambia niolewe tuu kwa kuwa mambo yalikuwa yameshakamilika nikajificha kwenyew lodge moja peke yangu siku nzima nikafikiria sana tena sana kuwa haya maisha ni yangu mimi na siyo wazazi hivyo nikaibuka na kusema sitaki kuolewa na zilikuwa zimebaki week mbili niingie kanisani kufunga ndoa.
nilipata wakati mgumu sana tena nilikuwa chuo mwaka wa mwisho ila nilimuomba Mungu anipe mume ambaye hataprenda kuona natoa chozi la uchungu bali chozi la furaha kwa kuwa nimeshateseka sana, Mungu amesikia kilio changu nimeolewa sasa na ni mume niliyemuomba kwa Mungu nina raha na amani tele. HVY USIKATE TAMAA HATA KIDOGO MUNGU ANAJUA WEWE LINI UTAPATA HITAJI LAKO MTUMAINIE NA UTAONA MIUJIZA YAKE, ALIYEPITA MUACHE AENDE OMBA MWINGINE
 
Back
Top Bottom