Natamani sakata la Lissu kupigwa risasi liwe declassified

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Mwaka 1994 mwanasiasa machachari huko nchini Kenya Dr Fredrick Masinde alipata ajali mbaya sana ambayo ilisababisha kifo chake. Ajali ambayo baadae ilikuja kujulikana kuwa ilitengenezwa na kisha yeye kuja kuwekewa kitambaa chenye sumu ili afe kwa kuvuta hewa ya sumu na huku wananchi wakiwa wamedanganywa kuwa amefariki kwa ajali ya gari.

Ilichukua muda mrefu kuja kufahamu kuwa aliwekewa sumu eneo la ajali ili afe na hii ilijulikana baada ya information juu ya kifo cha Dr Fredrik Masinde kuwa declassified.

Kwa hivyo ni wazi kuwa ili raia wa kawaida tuweze kujua ukweli juu ya matukio kama yaliyompata Tundu Lissu basi ni wazi kuwa lazima taarifa za matukio haya zisiwe siri tena.

Je, ni lini taarifa za kushambuliwa Lissu zitakuwa declassified na vyombo vya usalama vya nchi yetu? Tuna kiu kujua ukweli, kama dereva alihusika? Tunataka kujua ni nani alitumia Machine gun kufyatua risasi nyingi namna hiyo huku asifanikishe lengo lake. Na kikubwa zaidi tunataka kujua nani ni mhusika ali-mastermind mpango mzima.
 
Umetoa hoja nzuri mkuu ila mwamuzi wa haki yaani muda atakuja kuamua na watanzania watakuja kujua ukweli na hii ni pamoja na kupotea kwa saanane kutekwa na kuuliwa kwa Azory, nini hasa kilitokea na kusababisha kuuliwa kwa Akwilina na nini hasa kilipelekea kwa police wetu waliokula kiapo cha kulinda raia kuamua kutumia deadly force kwenye yale maandamano pale Pemba (to make things worse hata nyayo zao hazijafutika hapa duniani wamesalitiwa na politician's njaa ambao wao wamejitoa na kulipa the max penalty yaani kifo)hapo SA ukweli kuhusu SSA sawa na TISS yetu unajitokeza jinsi walivyotumia maelfu ya pesa vibaya na tuhuma zote zinaelekezwa kwa aliyekuwa president, ukweli unatoka na MUDA unaamua.
 
Back
Top Bottom