#COVID19 Natamani mdahalo 'live' kati ya wanaokubali na kukataa chanjo ya COVID-19

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,636
2,000
Timu "chanjo Yes" iongozwe na Dr Gwajima na timu "chanjo No" iongozwe na Askofu Gwajima!

Huo mdahalo mtoto hatumwi dukani. Kuna timu moja naiona haiwezi kuthubutu kutia mguu kwenye mdahalo huo, naiona ina hali mbaya.

Wamiliki wa luninga jaribuni kuzikutanisha timu hizo mbili ili watu wote waweze kutenganisha.

Pumba na mbegu ili wafanye maamuzi sahihi. Huku kwenye mitandao ya kijamii timu moja iko hoi sana.

Kwa bahati mbaya kwenye mitandao ya kijamii si watu wote wanapita huku. Lakini kwenye luninga mamilioni watatazama.

Naiomba serikali yetu sikivu wakubali mdahalo huo watakapoombwa na wamiliki wa luninga.
 

jumashaban

New Member
Nov 15, 2018
3
45
Mdahalo juu ya suala la Chanjo inahtaj zaid madaktari, n kwa bahat mbaya madaktar wetu ktk hili sio waongeaji sana, wanasiasa ndo wanaoongea sana ktk hili. madaktar wanatakiw wafanye analysis ya content iliyopo kwenye chanjo wahusianishe na DNA kisha watuthibitishee kuw tutakuw salama au la.
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,239
2,000
Timu chanjo lazima itoke nduki,maana mpaka Sasa haijamjibu Gwajima chochote,Ina kimbilia kumwita mpotoshaji.
 

Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
6,899
2,000
Timu chanjo No hawana majibu ya kisayansi watakwambia tumeoteshwa kwa unabii ,😂😂

2863330_3C944EC2-BCB0-4CC6-8681-15A945BEC8B1.jpeg
 

Attachments

  • File size
    15.7 MB
    Views
    0

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,276
2,000
Mkuu Mbingunikwetu hayo ni maono makubwa sana umeyapata, waje wote kwenye uwanja wa hoja ili tujue mantiki zipi zimebeba madini ya nguvu ndani ya uhiyari wa kuchagua ama mbuga au chanjo. Hapo ni uamuzi tu ya nani wa wakumfuata, Baali ama Mungu wa kweli, tiba ya kisayansi ama ile tiba ya kiroho.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom