S.N.Jilala
JF-Expert Member
- Jan 26, 2012
- 540
- 507
Prof.Lumumba kutoka Kenya,nilimsikiliza kwenye Kigoda cha MWL.Nyerere na leo nimemsilikiza vizuri. Jamaa naona anastahili kabisa kuitwa Prof.
Tuna maprofesa hapa lakini walio wengi wametekwa nyara kifikra na wanasiasa. Hawako huru kabisa,wanaogopa kusema ukweli.
Wakiongea baadhi yao mpaka unawaza kuwa kuitwa Profesa kaitwa kama sifa wanavyojiita wakina Prof.Jay,Majimarefu au?. Wako wapi magwiji kama wakina Prof. Chachage?.
Prof. Lumumba ukimsikiliza mpaka unavutiwa maana anaonyesha ukomavu wa hali ya juu kabisa katika changamoto za Bara la Afrika na utatuzi wake.
Mapungufu najua anayo, kama binadamu huwezi kuwa perfect,lakini nataka Ma-Prof. wetu watuonyeshe njia kwenye mambo magumu ya kitaifa. Wanatakiwa waseme ukweli hata kama watachukiwa na watawala kwani ndiyo kazi yao.