Natamani kuwe na ligi moja ya soka Tanzania

SammagaTZ

Member
Oct 24, 2021
48
52
Habari zenu wanajukwaa pendwa la michezo JF,

Katika kipindi hiking ambacho team ya taifa ipo kambini kujiaandaa na mechi za kufuzu kombe la dunia nimepata wazo kama timu ya taifa inajumuisha wachezaji kutoka Tanganyika Na Zanzibar Kwa nini kusiwe Na ligi moja ya Tanzania?

Natamani kitokee Kwa kuwa kitakuwa na maslahi ya kusogeza soka letu Na kupunguza manung'uniko kutoka upande mmoja na Nina imani itakuwa ligi Bora

Ahsante.
 
Hakutakuwa na shida kama viongozi wa team watakuwa serious na timu na kuwa na watu wa masoko Kwa ajili ya kutafuta wadhamini
 
Hilo jambo linawezekana kabisa shida ni utata uliopo katika masuala ya Muungao, suala michezo halipo katika masuala ya muungao, ila milango ipo wazi kwenye ushirikiano!

ndio mana kwenye mashindano kama ya CAF au Challenge cup tunashiriki individually!
 
Suala la michezo Ni la muungano ndiyo maana Zanzibar haina kiti FIFA Na team ya taifa Ni moja tatizo Ni pale kunapokuwa Na ligi mbili mechi moja
 
Hawa wazanzibari walivyolegea mbona watashuka daraja wote tutabaki wenyewe..... Sijaona Bado Fowadi ya Zanzibar ya kumpita BENJAMIN ASUKILE , KELVIN YONDANI au JUMA NYOSSO
 
Zanzibar wala urojo tulikuwa tunacheza nao zaman kombe LA Muungano yan team tatu zilizoshika nafasi ya juu bara na visiwan zilikuwa zinakutana nakucheza ligi yao halafu bingwa anawakilisha nchi CAF nafasi ya pili anashiriki shirikisho... Wala urojo wazanzibar walikuwa wanapigwa kila mwaka mpaka wakagomea huo mfumoo
 
Habari zenu wanajukwaa pendwa la michezo JF,

Katika kipindi hiking ambacho team ya taifa ipo kambini kujiaandaa na mechi za kufuzu kombe la dunia nimepata wazo kama timu ya taifa inajumuisha wachezaji kutoka Tanganyika Na Zanzibar Kwa nini kusiwe Na ligi moja ya Tanzania?

Natamani kitokee Kwa kuwa kitakuwa na maslahi ya kusogeza soka letu Na kupunguza manung'uniko kutoka upande mmoja na Nina imani itakuwa ligi Bora

Ahsante.
Zenji Ni nchi huru mkuu. Mazuzu tumebaki sisi Wadanganyika.
 
Back
Top Bottom