Ndebile
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 7,237
- 9,871
Nipo kibaruani mchana wa leo (nimerudi kazini awamu ya sita baada kama nilivyohaidi), nimempokea mama na kichanga chake ambaye amejifungulia kazini kwenye kiwanda cha Mchina (sehemu sitaitaja) ila ni mazingira mabaya kujifungulia binadamu, mama hana kadi ya kliniki na bahati nzuri alikuja kuanza kliniki ijumaa saa kumi akakuta huduma zimeishafungwa (jiulize ilikuwaje mama aanze kliniki na mimba kubwa karibia na kujifungua, hii haihitaji akili kubwa bila shaka hakuna ruhusa kazini) kwahiyo zile huduma kama vipimo vya wingi wadamu, magonjwa ya zinaa na ukimwi nk. na hivyo maisha ya huyu mtoto yapo hatarini!
Jamaa waliomsindikiza kwenye tax huyu mama ni wanaume watatu hakuna jisia ya kike! Walipofika wakahudumiwa wakataka kulipia staff aliyekuwepo akasema huduma za mama na mtoto ni bure, na hapo waksema wanazo 200,000/ mchina kawapa kwa ajili ya matibabu ya huyu mama na wakasema anahitaji risiti, wakauliza kama tunaweza kufanya mbinu ili risiti ipatikane .....kwa ufupi hatukuwapa risiti na badala yake yule mama alipewa sh.40,000 hela iliyobaki wasema wanaenda kutafta namna ya kupata risiti...tuachane na mambo ya pesa maana mimi sio lengo langu la kuleta uzi hapa JF,
Kitendo cha huyu mama kutohudhulia kliniki, kujifungulia kazini, nk kinaleta picha ya kuwepo na manyanyaso kwenye hiki kiwanda, nilitamani huyu mama awe mfano kwa akina mama na watu wote wanaoteswa na kunyimwa haki zao makazini...nilitamani kuripoti unyama huu ila....HII NCHI WAPENDA HAKI HAWATAKIWI KABISA, ukiangalia kesi za wenye pesa kama wale wezi wa mafuta Kigamboni ambapo serikali wapo kimya, nk nikijifanya kuingia anga za hawa wachina wanaoshirikiana na watanzania wenzangu yanaweza kunikuta ya kunikuta na kubaki peke yangu na historia isinikumbuke!
Tuendelee kuangalia pingamizi lililowekwa kwa Diamond Platnumz aondolewe kwenye tuzo za BET maana hiki ndicho waliowengi miongoni mwetu tunaweza sana!