Indoraptor
JF-Expert Member
- Aug 30, 2019
- 248
- 504
Habari za Weekend wanaJF,
Suala la utoaji wa nishati ya umeme sasa limekuwa kero kwa wananchi. Na yote hii ni kwasbabu umeme unauzwa na shirika moja tu.
Kwa mfano, nimejaribu kuangalia nishati ya gesi jinsi makampuni yanavyoshindana utakuta Manjis anapambana kumpiku Oryx, Oryx nae hataki kupitwa na Lake, kule Orange anakomaa na Mihan, Meru nae anakazana kuja juu (hiyo ni mifano tu, simaanishi ushindani ndo upo hivyo).
Leo hii wananchi hawasumbuki sana na nishati ya gesi. Sana sana huwa kuna kipindi inapanda bei lakini gesi inapatika huwezi sikia gesi imeisha
Tukija mfano mwingine; kwa makampuni ya simu, mbona wameruhusu TTCL ipate washindani. Ona jinsi na wao wanavyohaha kuuza sim card mitaani ili nao wabaki kwenye soko. Tofauti na enzi hizo wakiendesha biashara wenyewe yaan ukitaka simu kwanza unaulizwa unataka simu ya kazi gani.
Lakini leo hii, mtu ukiona TTCL haifai unaweka pembeni, unahamia kwingine, ukiona nako hamna nafuu unakuwa huru kuhamia kwingine tena.
Narudi kwenye mada, siamini kama Tanesco angepata mshindani tungekuwa na kero yote hii. Kila kampuni ingejitahidi umeme upatikane. Hata kama ungeuzwa ghali lakini bado ungepatikana tu. Tusingesikia mambo ya mgao.
-Nani angekubali kampuni yake ikose wateja?
-Mteja gani angetaka kubaki kwenye kampuni yenye mgao? Kama tunavyolazimika sasa hivi kwa sababu tu hatuna chaguo lingine.
Lazima kila kampuni ingetafuta mbinu yoyote iendelee kubali kwenye soko
Natamani siku moja midomo yetu itamke makampuni ya umeme Tz
1.xxxxxx Power Supply
2. ......... Electrical Company
3.------ Home & Industrial Power
4. Ndo iwe hawa wachovu. TANESCO.
Jumamosi njema.