Natamani kuona Serikali inaruhusu nishati ya umeme kutolewa na makampuni binafsi

Indoraptor

JF-Expert Member
Aug 30, 2019
248
504
Habari za Weekend wanaJF,

Suala la utoaji wa nishati ya umeme sasa limekuwa kero kwa wananchi. Na yote hii ni kwasbabu umeme unauzwa na shirika moja tu.

Kwa mfano, nimejaribu kuangalia nishati ya gesi jinsi makampuni yanavyoshindana utakuta Manjis anapambana kumpiku Oryx, Oryx nae hataki kupitwa na Lake, kule Orange anakomaa na Mihan, Meru nae anakazana kuja juu (hiyo ni mifano tu, simaanishi ushindani ndo upo hivyo).

Leo hii wananchi hawasumbuki sana na nishati ya gesi. Sana sana huwa kuna kipindi inapanda bei lakini gesi inapatika huwezi sikia gesi imeisha

Tukija mfano mwingine; kwa makampuni ya simu, mbona wameruhusu TTCL ipate washindani. Ona jinsi na wao wanavyohaha kuuza sim card mitaani ili nao wabaki kwenye soko. Tofauti na enzi hizo wakiendesha biashara wenyewe yaan ukitaka simu kwanza unaulizwa unataka simu ya kazi gani.

Lakini leo hii, mtu ukiona TTCL haifai unaweka pembeni, unahamia kwingine, ukiona nako hamna nafuu unakuwa huru kuhamia kwingine tena.

Narudi kwenye mada, siamini kama Tanesco angepata mshindani tungekuwa na kero yote hii. Kila kampuni ingejitahidi umeme upatikane. Hata kama ungeuzwa ghali lakini bado ungepatikana tu. Tusingesikia mambo ya mgao.

-Nani angekubali kampuni yake ikose wateja?
-Mteja gani angetaka kubaki kwenye kampuni yenye mgao? Kama tunavyolazimika sasa hivi kwa sababu tu hatuna chaguo lingine.
Lazima kila kampuni ingetafuta mbinu yoyote iendelee kubali kwenye soko

Natamani siku moja midomo yetu itamke makampuni ya umeme Tz

1.xxxxxx Power Supply
2. ......... Electrical Company
3.------ Home & Industrial Power
4. Ndo iwe hawa wachovu. TANESCO.

Jumamosi njema.
 
Nimeandika haya baada ya kuona umeme umekatika sasa hivi, na najua utarudi saa moja usiku.

Namfikiria kinyozi anayeenda kufungua kazi apate riziki yake ya leo
Namfikiria fundi welding ambaye ndo kwanza ametoa chuma zake nje aanze kazi ya kuchomelea
 
Habari za Weekend wanaJf

Unaamia mtandao gani wakati sa hivi wanashirikiana 🤔 wote wameambizana waweke 950mb kwa 2000tzs
 
Nimeandika haya baada ya kuona umeme umekatika sasa hivi, na najua utarudi saa moja usiku.

Namfikiria kinyozi anayeenda kufungua kazi apate riziki yake ya leo
Namfikiria fundi welding ambaye ndo kwanza ametoa chuma zake nje aanze kazi ya kuchomelea
Ratiba inajulikana leo umeme unashinda kesho haushindi ..sasa kama jana umenyoa umechomelea leo kinachofanya utoe vyuma nje nani
 
Unaamia mtandao gani wakati sa hivi wanashirikiana wote wameambizana waweke 950mb kwa 2000tzs
Ni kweli mkuu huduma imekuwa ghali lakini inapatikana.

Je, Umewahi kununua bando, mtandao ukakujibu ndugu mteja samahani hatuna MBs za kuuza kwa sasa? Au ndugu mteja leo tutauza MBs kwa watu waliopo maeneo fulani tu?
Hicho ndicho nnachomaanisha kwenye umeme. Hata kama kampuni itauza unit 1 kwa Tsh. 700 lakini cha msingi upatikane
 
Embu serikali ifanye kuruhusu hilo jambo, tuone wawekezaji wataweza au watashindwa?
Mkuu, kabla serikali haijaruhusu jaribu kutazama hata wewe. Kwa wingi wa nguzo za umeme zilizopo sasa ambapo supplier ni mmoja, itakuwaje kama wakiwa watatu?

By the way, ni nchi ipi ya dunia ya kwanza yenye power supplier zaidi ya mmoja ukiachana na kampuni za kuuza solar?
 
Habari za Weekend wanaJf

Suala la utoaji wa nishati ya umeme sasa limekuwa kero kwa wananchi. Na yote hii ni kwasbabu umeme unauzwa na shirika moja tu.

Kwa mfano, nimejaribu kuangalia nishati ya gesi jinsi makampuni yanavyoshindana utakuta Manjis anapambana kumpiku Oryx, Oryx nae hataki kupitwa na Lake, kule Orange anakomaa na Mihan, Meru nae anakazana kuja juu (hiyo ni mifano tu, simaanishi ushindani ndo upo hivyo).

Leo hii wananchi hawasumbuki sana na nishati ya gesi. Sana sana huwa kuna kipindi inapanda bei lakini gesi inapatika huwezi sikia gesi imeisha

Tukija mfano mwingine; kwa makampuni ya simu, mbona wameruhusu TTCL ipate washindani. Ona jinsi na wao wanavyohaha kuuza sim card mitaani ili nao wabaki kwenye soko. Tofauti na enzi hizo wakiendesha biashara wenyewe yaan ukitaka simu kwanza unaulizwa unataka simu ya kazi gani.
Lakini leo hii, mtu ukiona TTCL haifai unaweka pembeni, unahamia kwingine, ukiona nako hamna nafuu unakuwa huru kuhamia kwingine tena.

Narudi kwenye mada, siamini kama Tanesco angepata mshindani tungekuwa na kero yote hii. Kila kampuni ingejitahidi umeme upatikane. Hata kama ungeuzwa ghali lakini bado ungepatikana tu. Tusingesikia mambo ya mgao.
-Nani angekubali kampuni yake ikose wateja?
-Mteja gani angetaka kubaki kwenye kampuni yenye mgao? Kama tunavyolazimika sasa hivi kwa sababu tu hatuna chaguo lingine.
Lazima kila kampuni ingetafuta mbinu yoyote iendelee kubali kwenye soko

Natamani siku moja midomo yetu itamke makampuni ya umeme Tz

1.xxxxxx Power Supply
2. ......... Electrical Company
3.------ Home & Industrial Power
4. Ndo iwe hawa wachovu. TANESCO.

Jumamosi njema.
Shida ni kuwa kuna neno AUTHORITY ndo linaharibu sana..!! TTCL zamani walikuwa na authority ikaondolewa ndo wengine wakaja. Kabla ya hapo ukitaka kufanya biashara ya mawasiliano unawauzia wao, na wao ndo wauze kwa watumiaji. The same kwa TANESCO. Ikiondolewa hiyo, mbona itakuwa raha..!!

We kampuni inafanya biashara peke yake soko lote halafu eti wana SALES TEAM..!!
 
Ujinga na upumbavu wa Watanzania ndio unasababisha hayo yote,watu kila siku umeme unakatika-maji karibu mwezi,tumekaaa tu kama majunia ya mashudu tukilalamalika pasipo kuchukua hatua.

Kazia hivyo hivyo umeme katika kila siku-mpaka Siku tukipata akili.
 
Mkuu, kabla serikali haijaruhusu jaribu kutazama hata wewe. Kwa wingi wa nguzo za umeme zilizopo sasa ambapo supplier ni mmoja, itakuwaje kama wakiwa watatu?

By the way, ni nchi ipi ya dunia ya kwanza yenye power supplier zaidi ya mmoja ukiachana na kampuni za kuuza solar?
Hazina kwasababu supplier anatoa huduma ya uhakika, hizi nchi zetu zinahitaji ushindani ili kuleta reliability
 
Ujinga na upumbavu wa Watanzania ndio unasababisha hayo yote,watu kila siku umeme unakatika-maji karibu mwezi,tumekaaa tu kama majunia ya mashudu tukilalamalika pasipo kuchukua hatua.

Kazia hivyo hivyo umeme katika kila siku-mpaka Siku tukipata akili.
Safi sana shudu mwenzetu..!!
 
Miundombinu ya usambazaji wa umeme si rafiki katika biashara ya ushindani ndugu yangu, unless kama wanasayansi watakuja kuvumbua wireless power supplying technology siku za usoni.

Finland makampuni binafsi yanatumia miundombinu ya shirika la serikali kusambaza umeme kwa malipo maalum. Ila umeme unatoka kwa kampuni binafsi.

Wana makampuni binafsi nyingi tu za kusambaza umeme, mteja ana uhuru wa kuchagua na kuingia mkataba na kampuni anayoipenda.
 
Kampuni zipo ila zinauza umeme direct kwa Tanesco na sio kwa wananchi mfano kampuni ya Songas na ile kampuni ya mafisadi
 
Back
Top Bottom