Natamani kuoa, lakini

Natamani kuoa, lakini

We unataka mwenye sifa zote hizo unataka kuanzisha chama cha siasa au lengo ni nini hasa.
 
Natamani sana kuoa lakini sioi kwa sababu aina ya wanawake naotaka hawapo au wote wameolewa.

Ukiacha sifa za kwanza za mke mfano awe na upendo, mzuri, mvumilivu, mtafutaji, muelewa nk.

Mimi nataka mwanamke mwenye sifa za ziada kidogo maana sifa hizo hapo juu sehemu kubwa ya wanawake wanazo.

Nataka mwanamke mwenye ufaham wa wastani au zaidi wa mambo mengi mfano uchumi, sheria, tekinolojia, sayansi, siasa, dini, falsafa.

Mwanamke anaeweza kujenga hoja, kupambanua mambo mengi vizuri.

Mwanamke anaejua muziki, filamu na mapenzi tu simtaki, hanifai.

Mabinti wengi wa siku hizi wanajua mapenzi, filamu na muziki, mambo mengine hawajui na hawataki kujua, ukileta hoja nje ya hayo anayoyajua atabakia kuitikia tu "ndio mzee" maana hajui.

Wanawake wa ndio mzee mimi siwataki.

Hicho ndio kinasababisha nashindwa kuoa ingawa natamani. Wewe kwa nini huoi, huolewi. (najua kuoa au kuolewa sio lazima)

Mi nashindwa kwa sababu natafuta shabiki wa mpira wa miguu haswa anayeipenda CHELSEA FC
 
that's great thread for me, mkuu mawazo yako na yangu yako sawa kabisa,
sio una owa mtu stors zake ni mapenz, muzik, kusema watu, stors za kina Wema na kusoma pagazeti ya udaku,
licha ya uwaminifu na usomi, kuna vitu vingi sana vya ziada mwanamke ana takiwa kuwa navyo.

kwa upande wangu mwanamke anarekebishika na ana badilika, unaweza ukawa na asie juwa hivyo vitu na ukamfanya avijuwe tena kwa mda mfu tu...

mfano Salma kikwete hakuwa mwana ccm wala hakuwa mwana siasa, hata Mama maria Nyerere hakuwa mwanaharakati, lakini wameweza kubadilishwa.
Hata wake za wachungaji wakubwa kama Gamanywa, Gwajima hawakuwa wapendwa ila sasa niwapendwa.

Mfano binabsi, Mm ni shabiki wa Man u, huwa naendaga kuwatch au huwa nawatch sana game za Man U na mchuchu wangu, nae amejikuta anaipenda Man u.
 
Jitazame kwanza wewe mwenyewe unasifa hizo usitake vizuri wakati wewe ni muozo na sifa za mwanamke huwezi kuzijua kabla ya kumuweka ndani mke mwema hupata mume mwema mshirikishe mungu jambo la ndoa halina uprofesa hata maprofesa huingia chakani pia na elimu yao mapenzi kitu kingine subiri sana
 
bac uolewe wew,
izo sifa zote izo wew mwenyewe unazo????
alafu umeona wapi, mke pia awe mtafutaji???? ili iweje?? akusaidie??
 
Jitazame kwanza wewe mwenyewe unasifa hizo usitake vizuri wakati wewe ni muozo na sifa za mwanamke huwezi kuzijua kabla ya kumuweka ndani mke mwema hupata mume mwema mshirikishe mungu jambo la ndoa halina uprofesa hata maprofesa huingia chakani pia na elimu yao mapenzi kitu kingine subiri sana

Rudia kusoma mada uielewe usikurupuke tu kujibu.
 
that's great thread for me, mkuu mawazo yako na yangu yako sawa kabisa,
sio una owa mtu stors zake ni mapenz, muzik, kusema watu, stors za kina Wema na kusoma pagazeti ya udaku,
licha ya uwaminifu na usomi, kuna vitu vingi sana vya ziada mwanamke ana takiwa kuwa navyo.

kwa upande wangu mwanamke anarekebishika na ana badilika, unaweza ukawa na asie juwa hivyo vitu na ukamfanya avijuwe tena kwa mda mfu tu...

mfano Salma kikwete hakuwa mwana ccm wala hakuwa mwana siasa, hata Mama maria Nyerere hakuwa mwanaharakati, lakini wameweza kubadilishwa.
Hata wake za wachungaji wakubwa kama Gamanywa, Gwajima hawakuwa wapendwa ila sasa niwapendwa.

Mfano binabsi, Mm ni shabiki wa Man u, huwa naendaga kuwatch au huwa nawatch sana game za Man U na mchuchu wangu, nae amejikuta anaipenda Man u.

Asante bro,nashukuru kwa ushauri wako mkuu. Itanibidi nibadili mtazamo wangu kidogo.
 
Ndiyo maana nikasema itakuwa vigumu kama unafikiri unaweza kumpata mwenye vigezo vyote unavyotaka. Hata waliooa huwa wanaangalia vigezo viwili au vitatu ambavyo huwezi kuvifumbia macho na vingine ni either kurekebishana na ikishindikana ni kutafuta jinsi ya kuishi na udhaifu wa mwenzio. Mbali na hapo itakuwa vigumu na ukimwambia mtu ulishindwa kuoa kwa vigezo hivyo huwezu kueleweka. Hii ni sawa na tunavoishi na ndugu zetu, wafanyakazi wenzetu ambao kwa njia moja au nyingine wanakukwaza kutekeleza majukumu yako. Hali haliweza kukufanya uache kazi eti unakwazika. Watu wote tu kwenye sayari moja. Kwa maana ni kwamba ni vigumu kukweoa madhaifu ya wenzio. Hii inaanzia kwa mke kwamba hana vigezo vyote na haishii hapo itaenda kwa wafanyakazi wenzio hawako au hawafanyi unavotaka. Jaribu kutafakari..

Shukrani sana mkuu. Point taken. Mawazo kama haya ndio nataka.
 
Wille ni jina la kiume, nina mchumba nitaoa sio mda..
Tuwapende hivihivi taratibu wanafaa, kikubwa watatuletea na watoto na ni wasaidizi wetu tuu, they cant be like us, they are women.. Is that understood!!

understood sir. Thanks mkuu nimeelewa point yako,asante sana.
 
Sioni ubaya kwa sifa hizo upendazo, ingawa tunasema viwango ni ubora na muda, tafuta mwanamke bora tumia muda then set your own standard.

Kila kitu kinawezekana ingawa vingine utakuja vifikia kwenye umri wa uajuza.

Muombe Mungu utafanikiwa mkuu.
 
Wanawake kweli tuna kazi....yani anatakiwa ajue yote hayo plus kupika,kufua,kukata mauno.....pamoja na mishemishe zote hizo plus zile za kazini bado unataka akirudi nyumbani jioni au wikiend mjadili siasa,teknolojia na sheria...!! Samahani kwa kweli

Usisahau kujifunza ufundi gari, bomba, vitasa na kila kitu! Bado uzae na ulee!
 
Natamani sana kuoa lakini sioi kwa sababu aina ya wanawake naotaka hawapo au wote wameolewa.

Ukiacha sifa za kwanza za mke mfano awe na upendo, mzuri, mvumilivu, mtafutaji, muelewa nk.

Mimi nataka mwanamke mwenye sifa za ziada kidogo maana sifa hizo hapo juu sehemu kubwa ya wanawake wanazo.

Nataka mwanamke mwenye ufaham wa wastani au zaidi wa mambo mengi mfano uchumi, sheria, tekinolojia, sayansi, siasa, dini, falsafa.

Mwanamke anaeweza kujenga hoja, kupambanua mambo mengi vizuri.

Mwanamke anaejua muziki, filamu na mapenzi tu simtaki, hanifai.

Mabinti wengi wa siku hizi wanajua mapenzi, filamu na muziki, mambo mengine hawajui na hawataki kujua, ukileta hoja nje ya hayo anayoyajua atabakia kuitikia tu "ndio mzee" maana hajui.

Wanawake wa ndio mzee mimi siwataki.

Hicho ndio kinasababisha nashindwa kuoa ingawa natamani. Wewe kwa nini huoi, huolewi. (najua kuoa au kuolewa sio lazima)

wewe mwenyewe unajua falsafa ya kitu gani kati ya hayo uliyoyaorodhesha na kwa kiwango gani?

mnaotaka kulelewa mna matatizo sana
 
Back
Top Bottom