1.Kutamani ni dhambi.
2.Sifa za mwanamke wa kuoa hazitafutwi kama pesa,
bali zinatengenezwa pole pole.
3.Yawezekana labda wewe ndio tatizo,rejea neno "lakini" kwenye uzi wako na si lazima
sana kuoa au kuolewa ingawa ni jambo lililo jema na la kupendeza na lenye baraka.
4.Wakati mwingine usipende kuchagua chagua na kubagua bagua wanawake
kwani muda ndio hivyo unazidi unakwenda.
5.Ni vyema ukafumba macho na kufanya uamuzi sahihi sasa na kama ukishindwa
ni bora ukawa mvumilivu kwani ndoa ni mpango wa Mungu.
6.Jitahidi sana kuwa mcha Mungu na ipo siku utampata aliye kwenye ndoto zako,vivyo
hivyo ndivyo ilivyo kwa upande wa mwenzi wako mtarajiwa.
7.Na ukisha mpata ni wajibu wako kumtunza kwa hali na mali ili hatimaye kizazi na kizazi
kipate kuiga mfano ulio bora na wenye maadili mema yasiyo bagua au kuchagua chagua
wanawake au wanaume.
Ni hayo tu rafiki.
Nakutakia usiku mwema.
Asante.