Natamani kuoa, lakini

Natamani kuoa, lakini

Kichwa Ndio Mtu

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2014
Posts
3,079
Reaction score
1,719
Natamani sana kuoa lakini sioi kwa sababu aina ya wanawake naotaka hawapo au wote wameolewa.

Ukiacha sifa za kwanza za mke mfano awe na upendo, mzuri, mvumilivu, mtafutaji, muelewa nk.

Mimi nataka mwanamke mwenye sifa za ziada kidogo maana sifa hizo hapo juu sehemu kubwa ya wanawake wanazo.

Nataka mwanamke mwenye ufaham wa wastani au zaidi wa mambo mengi mfano uchumi, sheria, tekinolojia, sayansi, siasa, dini, falsafa.

Mwanamke anaeweza kujenga hoja, kupambanua mambo mengi vizuri.

Mwanamke anaejua muziki, filamu na mapenzi tu simtaki, hanifai.

Mabinti wengi wa siku hizi wanajua mapenzi, filamu na muziki, mambo mengine hawajui na hawataki kujua, ukileta hoja nje ya hayo anayoyajua atabakia kuitikia tu "ndio mzee" maana hajui.

Wanawake wa ndio mzee mimi siwataki.

Hicho ndio kinasababisha nashindwa kuoa ingawa natamani. Wewe kwa nini huoi, huolewi. (najua kuoa au kuolewa sio lazima)
 
hicho ulichoongea ni kwa mujibu wa nafsi yako ila sasa hivi huwez kupata mwanamke ana sifa zote unazotaka hata nyie boys hatuwez wapata wote wenye vigezo stahiki tunavyovihitaji ukitaka umpate wa hivyo maybe uumbe wako mwenyewe
 
unatakiwa umuoe mwenye baadhi ya sifa na zingine utamwongezea sio kwamba atajua yote
 
hicho ulichoongea ni kwa mujibu wa nafsi yako ila sasa hivi huwez kupata mwanamke ana sifa zote unazotaka hata nyie boys hatuwez wapata wote wenye vigezo stahiki tunavyovihitaji ukitaka umpate wa hivyo maybe uumbe wako mwenyewe

vigezo stahiki mnavyovitaka ndio vipi
 
kweli wewe kichwa ndio mtu, aya, subiria hizo sifa za ziada, cha kukusaidia nenda afrika magharibi wapo wanaojua kuchambua mambo hasa ebola.
 
ha ha ha uuuupsi umba wako mkuu uweke new file na program unazotaka pia antvirus strong watu wasije kutia virus

kumbuk kila mtu ana tabia zake na kila mtu kalelewa familia tofauti ...tafuta general tabia njema kwa KUMUOMBA MUNGU...baada ya hapo kaa nae mfudishane hizo za unique unazotaka..

jaribu kupanda ndo uvune mkuu..unapenda kutumia kilicho chema bila kujua msemo wa no sweety without sweat
 
Chonga wa kwako. Lol! Oa ambaye angalau anakaribiana na utakacho kisha unamuongezea maarifa hayo. Cha msingi awe tayari kufunzwa hayo mambo. Wengine wabishi. Ila utampata tu, panua wigo wa maeneo unayotafuta. Kila mtu ana wake hapa duniani. Ila pia nawaonea huruma kina dada, vigezo vya kupata mke vinaongezeka na kuwa vigumu zaidi kila siku.
 
Unajiwekea standard za juu sana ambazo hutaweza kuzipata kirahisi. Kifupi unajitengenezea matatizo mwenyewe.

Fikiria kuoa kwa msingi wa kuoa sio kupata forums za kisiasa, kichumi, sayansi, saikolojia, technolojia n.k. Interests are never universal bro. Mwanamke ana priorities zake na mwanaume ana priorities zake..

unaweza kupata mwenye vyote hivyo vya kisiasa lakini akawa na mengine ambayo yanakunyima hata hamu ya kukaa nyumbani au hata kumsemesha kwa lolote.

Jitafakari upya mkuu, pungua matarajio yako
 
Mature woman umri unaanzia 30...hao unaona wenye upeo wa kila kitu mostly wako in their 30s...wewe oa ambae atakuwa na muelekeo wa kuwa smart later...below 30 music..movies ndo wakati wao....watakomaa taratibu..
 
Wanawake kweli tuna kazi....yani anatakiwa ajue yote hayo plus kupika,kufua,kukata mauno.....pamoja na mishemishe zote hizo plus zile za kazini bado unataka akirudi nyumbani jioni au wikiend mjadili siasa,teknolojia na sheria...!! Samahani kwa kweli
 
unatakiwa umuoe mwenye baadhi ya sifa na zingine utamwongezea sio kwamba atajua yote

Sawa mkuu. Sema unakutana na binti akademikale yuko vizuri,aliscore single digit level zote za sekondari,chuo ana gpa nzuri tatizo linakuja hajui kingine chochote zaidi ya taaluma yake. Ni kazi kwa kweli.
 
Mature woman umri unaanzia 30...hao unaona wenye upeo wa kila kitu mostly wako in their 30s...wewe oa ambae atakuwa na muelekeo wa kuwa smart later...below 30 music..movies ndo wakati wao....watakomaa taratibu..

Point taken mkuu.
 
Back
Top Bottom