Natamani kumwona tena

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,130
918
Ni miaka mingi hatujaonana, leo maazimisho ya Kifo cha Mwalimu, nipo katika usafiri wa umma (daladala) nikiwa kituoni, watanzania wenzangu wakiteremka, natizama dirishani, namwona jamaa ninae mfahamu,yeye ni Mmachinga anafanya biashara ya CDs..natamani kumsalimu kumbe nae ameniona anapaza sauti "wee bro, wapi??" Mbele ya huyo rafiki yangu mmachinga kuna mwanamume na mwanake wameongozana, mwanaume anageuka kutizama nilipo, ananiona nikipunga mkono, nae ananipungia, hajui kwa nini nami sijui (hatufahamiani), huyu mwanaume amemkumbatia mtoto mchanga kifuani, ghafla mwanamke aliyeongozana nae nae anageuka, tunagongana macho...anatoa tabasamu dogo na kufumba mdomo kutumia kiganja cha mkono wake, lakini naona kama kakwazika, kama amegusa waya wa umeme, akaduwaa kwa muda, akashindwa kuvuta hatua mbele...ni kama kitu kilikuwa kimemwingia, akajilazimisha kujongea mbele, na akijifanya kama kiatu alichovaa kinamvuka, akainama na kutizama kule nilipo na kutikisa kichwa kwa dalili zote za kuonyesha ana huzuni fulani moyoni baada ya kuniona...hana jinsi, ana hofu fulani!!

Nami nilihisi kitu kimekikamata kooni..nikaachama, nikatamani kuteremka kwenye gari lakini sikuwa na maamuzi ya haraka.. nikahisi sauti ikiniambi
a "yule aliyekuwa nae ni mumewe na mtoto wao''...mara dereva wa daladala akawa tayari ameondoa gari kwa kasi....akili ikanirejea, nikakumbuka.....duh..huyu mwanamke alikuwa rafiki yangu zamani, tukapotezana..sasa nimemwona lakini sijui anapoishi..nitamwonaje, natamani kumwona tena, nisikie tu hata sauti yake nyororo, inikumbushe zamani .

 

Magoo

JF-Expert Member
Sep 4, 2011
445
72
Jana tu kuna mmoja tulipotezana miaka kama 5 nyuma nikiwa kwenye corrola katika foleni Ubungo mara mbele anakatiza mrembo nikamkumbuka na kumuita ile anakimbia kuja kwenye gari trafiki akaruhusu magari nikabaki sina jinsi zaidi ya kuondoka ndo imetoka hiyo
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,802
24,505
hivi ile huduma ya radio free africa wasukuma walikua wanaitumia kuwataarifu ndugu zao wakiwa na safari za kwenda mjini kahama,geita na mwanza bado ipo? lol!

QUOTE=Husninyo;2645010]bandika matangazo.[/QUOTE]
 

hayaka

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
474
100
jitahidi kumsahau la sivyo utaishia kunawa na kula hutakula sasa point ya kumtafuta ni ipi?
 

AMINATA 9

JF-Expert Member
Aug 6, 2011
2,128
640
duh! we lazima ni mwandishi mana si bure uko deep kinoma............any way back to ze point pole mnooo loh!
 

samito

JF-Expert Member
May 16, 2011
631
175
nategemea kufanya movie wakat wa x-mas, nitafute uniandikie script, tutalipana vizur usijal
 

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,130
918
si mlishamalizana unamtakia nini mwenzio ana ndoa yake tayari?

Hatukumalizana mkuu, pengine mazingira na wakati vinaweza kututenganisha na baadae kujikuta ikishindwa kuwa na wachaguo lako..bado nahisi ndimi zangu zanivuta kwake...kwa sasa si tena kwa yale tuliyokuwa tukifanya zamani, bali kwa urafiki mpya, nakumbuka sana kauli zake za kutia moyo, najihisi ningekuwa mbali kama tungejaliwa kuwa pamoja...nilipomwaona japo sasa si wangu ila nimeingiwa na wivu mkuu juu ya mwanaume mwenzangu aliye nae kwa sasa..kwa lile tabasamu la woga alilonitolea, nahisi nae bado atakuwa ana fikira zinazofanana na za kwangu...angependa tuonane tena..
 

MAGISAC

Member
Sep 6, 2011
97
26
Una dalili zote za kuchakachua mke wa mtu, Mungu aepushe msionane tena, ulishachelewa bwana ungetangaza nia mapema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom