mdoe
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 433
- 103
Mimi ni Kijana wa miaka 30. Nimezaliwa katika familia masikini, mkoani Kilimanjaro. Nimeanza kujitambua nikiwa na umri wa miaka mitano nikiwa mikononi mwa bibi wa mama yangu. Sikujua ni kwanini niliishi na bibi wa Mama lakini Baada ya muda, Mama alikuja kunichukua na Nikaenda kuishi nae wilaya nyingine mkoa wa Kilimanjaro ambapo nilianzishwa masomo ya elimu ya chekechea na msingi. Mama yangu ana watoto wane, mimi nikiwa wa pili.
Mtoto wa mwisho ni mtoto wa baba yetu mlezi, ambae nilikuja kubaini kuwa Yule sio baba yangu mzazi, ila ni mlezi kufuatia vijimaneno vya mjomba na Mama yangu mdogo aishie kijijini. ( Wewe mu-uru, . Wewe mkibosho, nk. Wakati Baba tuliekua nae ni Mzigua) Nilikuja kubaini hilo nikiwa kidato cha nne.
Nikaanza kupata Kiu ya kumjua baba yangu mzazi.
Baada ya kumaliza kidato cha sita, hamu ya kumjua baba yangu mzazi ilizidi. Nikamfuata mama yangu mdogo (R.I.P. mama mdogo), ambae alikua akiishi moshi maeneo ya Pasua.
Sikutaka kumbughudhi Mama yangu kwasababu niliona tabu zote alizopitia katika kutulea na kutusomesha. Nilijua wazi Mama mdogo atakua anamjua vizuri dada yake (Mama yangu), na anaweza kuwa na clues muhimu kumpata baba yangu. Alikataa sana, ila mama ni mama.
Nilijua niseme nini na nimshawishi vipi na hatimae alinipa details za baba yangu japo hakujua alikoishi. Kutokana na details nilizopata, ikiwa ni pamoja na sehemu alizofanya kazi, nilifanikiwa kumpata mtu ambae alinipeleka moja kwa moja mpaka nyumbani kwake.
Nilimuona na nikajitambulisha. Niliposema tu nilipotokea alinijua mimi ni nani. Akanitaja jina. By then I was around 16. Nilikaa kidogo na akanipa namba za ndugu zangu kibao niwatafute. Niliwatafuta baadhi na nikajenga nao ukaribu. Nilidhani baba, pamoja na kutokua na uwezo (Amestaafu), angetambua uwepo wangu.
Ila zaidi ya mimi kwenda kumsalimia na kuwa kama mgeni yeyote tu wa kawaida anaekuja na kuondoka, hapakua na la ziada. Hakutaka kujua naishije, niliishije, nini malengo yangu, … no dad to son talk at all. Mategemeo yangu ya kumuona na kuongea na Baba yalipotea kabisa. Nilimtembelea kama mara tatu na baada ya hapo nikakaa kimya kuona kama atanikumbuka japo kwa ku beep.
Baada ya muda, niliamua kumchunguza mama taratibu kujua kulikoni. Nilianza kwa kumuambia kuwa namjua Baba yangu mzee …(Nikamtaja jina). Alishtuka kidogo hatimae akaniambia kua ni kweli, huyo ndie baba yako. Baada ya siku kadhaa, Mama aniliita faragha.
Akaanza kunisimulia mambo ambayo baba alimtendea, iliniuma sana. Ilifika kipindi mama anaomba ridhaa kwa barua kwa baba kuwa tupelekwe jando (Ikumbukwe kuwa walishaachana miaka mingi nyuma), baba anajibu kwa barua kuwa "Hao watoto ni zawadi yako nimekupa. Fanya chochote unachotaka".
Sijui nini chanzo cha ugomvi wao, sijui nini kilipelekea wao kuachana, sijui ni kwa nini tuliishi maisha ya shida sana na mama aliteseka sana peke yake kutulea na wakati baba alikua na uwezo, ila kwa vyovyote vile, baba alitakiwa kuonyesha kuwa altujali wanae.
Ameniona mimi tu, Mdogo wangu alienifata nae ni mwanae, ila wala kumuulizia hamuulizii. Niliwahi kumuuliza kuwa anamtambua mdogo wangu kuwa ni mwanae akajibu kuwa Anamtambua.
Mada ambayo wana Jamiiforums nataka wani shauri ni uamuzi ninaotaka kuuchukua sasa.
Nimemchukia baba yangu ever since nimemuona. Ila inawezekana kuna mengi mengine ambayo siyajui kati yake na mama yangu. Nafikiria kwenda kuongea nae aniambie mambo mengi sana kati yao na kwanini ametususa kiasi hicho.
Japo sidhani kuwa ni uamuzi sahihi kwani niko na baba mlezi ambae kwangu mimi amebeba thamani yote ya neno Baba. Natamani nimsamehe ila sina pa kuanzia. Namuona kama womanizer kwasababu ana watoto sita nje ya ndoa yake, mimi na mdogo wangu tukiwa wamoja wapo.
(Hakuwa amemwoa mama, inavyosemekana alimdanganya, akamzalisha kumbe ameoa). Je, ni uamuzi sahihi kwa mtoto kum face baba yake na kuhoji ukweli wa yaliyojiri kati ya baba na mama?
Kwanini he was irresponsible kwetu tukiwa wadogo? Lengo ni kupata sababu yakumsamehe ili nafsi iwe na Amani kila nikimkumbuka, Badala ya chuki na hasira.
Niwieni radhi kwa uzi mrefu na mchanganyiko wa lugha.