habari zenu wanajamvi,
kweli, natamani sana kuwa na mwanaume mwema, mwenye upendo wa kweli, anaejali, na mwenye utu. lakini kulingana na hali halisi ya wakati huu, mawazo hayo ni hadithi. kumpata mwanaume wa staili niitakayo inakuwa ni bahati ya kuzaliwa.
hivyo nimeamua kutazama kama vile natazama mpira uwanjani...! nimewashirikisha tu mawazo na hisia zangu, si lazima kuchangia.
Kwa ujumla hakuna mwanadamu mtimilifu,kila mmoja wetu ana mapungufu yake kwa hali hiyo ujikane na ujitwishe mzigo wako. Kumbuka mchagua nazi mwishwe huchagua koloma