Natamani kujiunga na TISS, Nifanyeje?

Natamani kujiunga na TISS, Nifanyeje?

Mimi natamani kuwa na cheo cha kulindwa na hao watu, aisee kumbe binadamu tumetofautiana sana
Hahahah ata mm nataka niwe raisi wawe wananilinda kila mara wanizunguke kama 30 iv wananilinda tu!!
 
Habari wakuu,

Kwa muda mrefu nimekuwa naipenda sana kazi ya Usalama wa Taifa. Ingawa najua kila mtanzania mzalendo ni Usalama wa Taifa lakini mimi naitaka kazi hii kwa urasmi kabisa.

Awali nilihisi kuna chuo cha mafunzo ya kusomea Usalama wa Taifa lakini baada ya kufanya utafiti na kuendelea kuwa na kiu kwa kazi hii, nimegindua hakuna chuo cha namna hiyo. Ndio maana leo nimeona nilete hoja hii ili nipatiwe msaada na maelekezo.

Naomba kuwasilisha!

Kwa ku-post hili swali jamii forum umeshafeli. Tafuta kazi nyingine
 
Mimi natamani niwe Bashite niwatumie navyotaka
 
Kwann mnapenda kutuchunguza sana sisi watu wa TISS?

Kuwa na adabu, usije kuja kulia hapa.

Ishia hapohapo.Kukutafuta ni kazi ndogo sana.
 
Usalama wa taifa wanachukuliwa vijana wa ccm green guard ,hiyo ndio siri ,hawachukui watu wasioamini katka ccm
 
Sasa kumbe unajua hadi Makazi yao sasa unatusumbua nini kutuuliza humu kuhusu kupata Ajira huko Kwao? Kwanini tu usiombe kuingia humo wanakoishi ili uyaeleze haya yote ili uweze kusaidiwa kiharaka na ufanikishe unachokitaka kuliko kuja na huu Upupu / Upuuzi wako humu JF? Unafiki ni kitu kibaya mno kwa Binadamu.
Mkuu ukiona hivyo ujue kuna mtu/watu ana/wana/lotafuta hapa JF,hasa ukizingitia kuwa mada nyingi uchambuliwa/uanzishwa JF baadae magazetini (and Vise vesra).
Anyway tuwape sikio labda kuna chochote ata/wata-choambulia/kujifunza.
 
Huwa hatuchukui watu wa aina yako! Usirudie kusema hatuna chuo cha mafunzo! Huwezi ukajua mpaka siku tutakayokuteka ndiyo utaamini kama tuna chuo cha mafunzo!
Nimeipenda, heri mie sijasema.
 
Huwa hatuchukui watu wa aina yako! Usirudie kusema hatuna chuo cha mafunzo! Huwezi ukajua mpaka siku tutakayokuteka ndiyo utaamini kama tuna chuo cha mafunzo!
Na mimi naomba kuwa mmoja wa mateka yenu mniingize kwenye kazi yenu.
 
Kazi ile inafaa kwa wasio muamini Mungu ... kama unaimani na Mungu wako kwa kufuata matendo mema ... hasa msimamao wa amri 10 za Mungu hiyo sio kazi ya kufanya itakupeleka motoni ...

Achana nayo sio kazi nzuri wala haifai ... haina uhuru ... kuna kazi nzuri sana za kizalendo zenye manufaa mpaka kwenye maisha yako baada ya kifo ...
Km vile kazi gani?
 
Back
Top Bottom