Natamani kujiua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani kujiua

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kimada, Jun 10, 2011.

 1. k

  kimada Member

  #1
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana Jamii Forum. Mimi ni mgeni humu. Ila si mgeni ki hivyo nimekuwa natembelea bila kuwa member. Nimeamua kujiunga ili nipate kushauriwa kwani shida niliyonayo siwezi kushare na mtu ninaye mjua.

  Mimi ni mdada wa miaka 32. Ni mrembo sana yaani wale mnaoita 8 figure. Sijisifii ila hilo nimeona nilitamke ili muweze kuielewa vizuri mada yangu.

  Nilitokea kumpenda sana kijana mmoja na kuja kugundua baada ya miezi miwili kuwa ni mume wa mtu. Kaka ni muislamu hivyo havai pete na kwa kuwa ni kijana sikuweza kudhania kuwa ni mume wa mtu na kwa kweli ningejua nisinge mpa moyo wangu.

  Tatizo niligundua kuwa kaoa wakati nimeshampenda. Na ni yeye mwenyewe alinitamkia kuwa nina mke baada ya kujua sitaweza kumwacha kwani nilikuwa nimekolea.

  Tumekaa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka na nusu sasa mpaka pale mkewe alipokuja kugundua. Mimi mkewe nilikuwa nimeshamjua. Ni mdada msomi na ana kazi nzuri sana ila ni wa kawaida na aniingii hata nusu kwa uzuri kwa hiyo nilijua tu kuwa mumewe atakuwa ananipenda mimi zaidi na labda kuna siku nitakuwa mke wa pili kwani ni muislamu.

  Tatizo limeanza miezi miwili iliyopita. Jamaa alinipigia simu akanambia mkewe amejua kuwa tuna uhusiano, kwa hiyo mimi na yeye basi kwani hataki kuvunja ndoa yake. Nimeumia sana imagine mwaka na nusu na nimeshampenda sana. Nimejitahidi kumfuata ofisini kwao secretary wake ananambia jamaa kasafiri wakati gari naliona nje ya ofisi. Nimempigia simu simpati naona amebadili namba.

  Hivi kweli wanaume mnaweza kuwa wakatili hivi? Kibaya zaidi mkewe kutwa ananipigia simu na kunitisha kuwa atanifukuzisha kazi. Mimi sijali kufukuzwa kazi kwani ninampenda sana huyo mwanaume.

  Nishaurini nifanyeje kwa wale wenye uzoefu wa kuwa vimada na wale wenye nyumba ndogo.

  Msinitukane jamani. Mimi sijawahi maishani mwangu kutembea na mume wa mtu zaidi ya huyu na sikuwahi kuwaza kuwa yatanikuta. Hivi nyie wanawake wa kwenye ndoa uwa mnawaroga wame zenu? Iweje mtu niliyekuwa nampagawisha the other day leo aseme sitaki kukuona tena kisa tu mkewe kajua?


  Na huyu mkewe nimfanyeje aache kunifuata fuata. Maana amekuwa ananipa vitisho kila kukicha mpaka nahofia uhai wangu. Mumewe mwenyewe kesha niacha na yeye bado analeta mikwara wakati nikimwangalia hata ngumi moja namuua.
   
 2. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mnhhhhhhhhhhhhhhhhhh........
  pole sana time is the best healer...
  with time utamsahau tu......

  jichanganye kama wewe sio mtu wa kutoka anza sasa kutembelea sehemu zile social kama pub/club...sehemu za michezo nk utapata tu wa ubavu wako...pole sana....
   
 3. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  oops badilisha number huyo mkewe atakuwa hakupati,kwa kifupi anza maisha yako upya kama vile hujawahi kukutana nao....
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  aljunuuni funuuuni

  kila mwendawazimu ana fani yake lol
   
 5. Big Lady

  Big Lady JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi ipo hapa
   
 6. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Jitahidi kuni PM leo leo. Mambo yako yatakunyookea haraka sana. Usikawie
   
 7. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 80
  Kimada:
  - First of all no man is worth your life! Let alone a married man aliyekutamkia hakutaki with words and actions!!

  - Secondly kuhusu urembo na kumpagawisha, you can never relay on that for sure .While you may have been blessed with the looks , labda huyo mkewe has been blessed with cash na ndiye anayemhifadhi huyo jamaa?? Mind you love and/or sex never pays the bills!!

  -Lastly, hebu jiulize if this guy really wanted you, kwanini akuache wakati you were willing to be his second wife na yeye imani yake inamruhusu to have more than one missus??
   
 8. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Tatizo umelikuza wewe polepole na kwa mda mrefu. Pale ulipojua baada ya yeye kukuambia ilibidi uwe alerted, na si uchawi bali jamaa anaipenda ndoa yake.
  Jipe muda utapona, na utapenda mwingine kuliko huyo. Huyo jamaa mpotezee kama hajawahi kuwa nawe katika maisha, ukiacha huyo utampa nafasi aliye single.
  Best wishes.
   
 9. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  1. mwanadada uzuri pekee si kigezo cha kupendwa zaidi. So futa kabisa akilini mwako eti kisa we ni figure no 8 ndio utapendwa sana.2. Huo ukatili wa wanaume unauovutia upande wako eti!! Vp kuhusu ukatili alioufanya huyo jamaa kwa mke wake? Dont be selfish just stay away from them.3. Naona umeanza hadi kufikiria kumroga mme halali wa mwanamke mwenzako eti. Kwa nini usitulie na kumsubiri wako? Hakuna uchawi mzuri kma kumheshimu mumewe, kumjali na kuongea naye vizuri. Hivyo ndivyo wanawake wengi ambao ndoa zao zinadumu hufanya.4. Acha kumsumbua na kumfuata fuata mme wake hapo ndio huyo mke wake ataacha kukusumbua. Just live ur life and let them live their lives.
   
 10. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mungu anakupenda Dada yangu.Ameruhusu haya yatokee sasa ili upone sasa kabla hujafika mbali.Unajua ulichokuwa unafanya sio sawa.Maana hata wewe ungekuwa huyu mke wa huyo bwana usingefurahi kusikia habari hizi.Hakuna ushauri mzuri ambao naweza kukupa zaidi ya kwenda kwa Mungu aliyemfinyanzi na kutubu na kumwomba akuponye na jeraha hilo.Baada ya hapo Mwambie Mungu afanye njia uweze kutoka hapo.Kwa Bwana Yesu yote yanawezekana.Yeye aliyeruhusu yote yakutokee, yeye aweza kukuponya.Mtwishe Bwana Yesu fadhaa zako atakusaidia.Usifikirie kulipa kisasi wala kufanya vita maana haitasaidia.
  Wanaume wako wengu sema ulijifunga sana kwa huyu bwana na kufunga ufahamu wako usiangalie wengine.Kiri umekosea, omba msamaha mbele za Mungu halafu mwambie Mungu akusaidie maana huu mzigo sio mwepese hutaweza kuubeba peke yako.Ukicheza utazidisha uovu kwa kumaliza waganga au kujimaliza mwenyewe au kumaliza mtu.
  "Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; " (Isaya 1:18-19).
   
 11. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0

  Fanya hivi mi najitolea siku tujumuike pamoja na wewe ili akikupiga simu huyo mkewe naongea naye mimi .nitakachomueleza kama atarudia kuupigia atakupigia itakuwa ni kukuomba na yaishe.

  So nasubiri pm yako kimada.
   
 12. s

  shosti JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Dada unaonekana umzuri lakini mambo adimu huna hahahahahahhhha,pole kula uzuri huo....umetumiwa kama pedi kwisha khabar yako
   
 13. Y

  Yakuonea JF-Expert Member

  #13
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 601
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwanza nimelipenda jina lako 'kimada' , naona umejisifia sana kwa uzuri ulio jaaliwa nao (fig no. 8). Utakuwa unakosea sana ukifikiri unaweza kutumia umbo lako kama silaha ya kusambaratisha ndoa ya watu, ndoa ina mambo mengi nafikiri ni tofauti na wewe unavyodhania, usivuruge ndoa ya watu , jipange upya na endelea kivyako
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Jun 10, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Jamani yaani wewe mrembo unataka kujiua kisa mme wa mtu ..leo umenipa kali ya mwaka

  Pole sana lakini maana moyo wa kupenda hauna subira ..cha msingi hebu tuliza moyo mama..nashukuru mungu mahusiano na huyo mme wa mtu yameisha ili uanze maisha yako mapya kabisa.

  kaa utulie na kama unatamani sana kuolewa piga goti na uombe mungu atimize haja ya moyo wako.
  Omba kwa imani bila kukoma .
  Kumbuka mungu hachelewi wala hawai yeye anatoa kwa wakati wake anaopanga mwenyewe
  ..mungu akusaidie katika jambo hili
   
 15. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #15
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Pole sana ndio inavokuaga kwani hujui? mke akigundua huwa uhusiano unakufa labda kwa vichwa ngumu, Ndio maana vimada wenye akili huwakumbusha wanaume zao kurudi nyumbani mapema kumheshimu mke, kutoonyesha kama ana uhusiano mwingine ili wadumu kwenye dhambi yao hiyo......Ushauri wangu hivi huoni raha kutafuta wako na wewe ummiliki mwenyewe na wewe akienda huko nje ana refer kwamba ana mke yaaani wewe? Unaweza ona umri umeenda ila hujachelewa bado jipe moyo na anza upya
   
 16. M

  Marytina JF-Expert Member

  #16
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  na wewe huna maneno mengine ya kumwambia mpaka umuumize au kwa kuwa ana mpango wa kufa?
   
 17. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #17
  Jun 10, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mi sikupi pole hata kidogo.ulipogundua ni mume wa m2 ulipaswa kuachana nae asap,lakini kwa kutumia kigezo cha uzuri uliona uliendelea kujipa moyo ati utakuwa second wife.kwani jamaa aliwai kukutamkia kuwa anataka kuoa tena? Nakushauri futa kabisa iyo mentality ya uzuri kwani ndo inakudanganya.nani alikwambia mwanaume anapenda kwa kuangalia uzuri na figure
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Jun 10, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  pauline..............abadilishe namba na amuachie mumewe!
   
 19. M

  Marytina JF-Expert Member

  #19
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  u hv spoken ma mind
  kumpa pole ni kuendekea uhawara mode of living
  Akatafute wa kwake mwenyewe na si apore wa wenzie koma kabisa
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Jun 10, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sijui wanawake sometimes mnakuwa na akili za namna gani mtu unaambiwa pale kuna shimo utadumbukia lakini bado hausikii unazidi kwenda tu cha ajabu zaidi kwa vile umejijua wewe ni KIMADA umeamua kujipa na ID ya KIMADA hivi unataka tukushauri nini? Unataka tukushauri uendelee kumegana na mume wa mtu kwa vile unajifanya umekufa sana juu? Kama unasema ulikuwa unampagawisha iweje leo kakuacha na karudi kwa mkewe?

  Wakisema wanawake hamjithamini mnaona mnaonewa hivi unataka kuniambia haujaona wanaume wengine kwa umri huo ulionao au ndio kusema sikio la kufa halisikii dawa au ndio kichwa cha mwendawazimu saa zingine mnakuwa mnajitafutia mikosi tu maana kutembea na mke/mme wa mtu ni kujiletea nuksi na mikosi, haya labda ni kitu gani ambacho unaweza kujivunia kwa kutembea na mume wa mtu nachoona hapo ni kwamba kakutumia kama vile chupa maji baada ya kukata kiu unatupa kwenye dustbin. Saa zingine fungua macho vitu vingine mnalaumu wanaume wakati viko ndani ya uwezo wako sasa hapo utamlaumu nini mwanaume wakati wewe aliishakwambia kuwa ana mke na wewe bado ukaendelea kujenga msingi. Tafuta maisha yako mwenyewe wanaume wako chungu nzima unajitia najisi kung'ang'ania mume wa mtu.

  NB: Halafu wanaotaka kujiua huwa hawasemi you just do it. Halafu ukijua unakuwa umempunguzia mume wa mtu matatizo.
   
Loading...