Natamani hata kuondoa uhai wangu

Natamani hata kuondoa uhai wangu

Mkuu pole na sijui uliwaza nini huna pesa halafu ukawa mlevi.
Ila kumbuka maisha yako yana thamani kuliko laki 5. Kuna mtu humu yeye alihustle akapata pesa akaibet mils sijui 3 ikaliwa na hakuwahi kujiua.
Ni hali ya kawaida ya mtu inaweza kumkuta, anakata tamaa, mbele giza nyuma giza, unasema ngoja nimalize tu na hii iliyopo. Kumbuka story ya Mama Mjane kwenye Biblia, akasema ngoja nikatengeneze chakula cha mwisho nile na mwanangu kisha tusubiri kifo.....kwahio wala tusimlaumu. Tumsaidie kama tutaweza
 
Humu ataambulia ushauri akihitaji msaada wa kifedha.
La msingi akumbuke kuwa hata hiyo laki 5 aliitafuta kwa jasho lake hivyo kama aliweza basi hana haja ya kujiua anaweza akatafuta na kupata zaidi ya hiyo.
 
Weka hapa qualifications zako tafadhali, huenda akajitokeza mtu/watu wakataka kukusaidia.
 
Pole saana mkuu ila na wasiwasi umeamka na hangover inakupelekesha hadi unapata mawazo ya kujiua
 
Weka hapa qualifications zako tafadhali, huenda akajitokeza mtu/watu wakataka kukusaidia.
Qualification zangu mkuu mimi nilisoma diploma chuo fulani(Public administration and management)na sikupata ajira kwa zaidi ya miaka 5 sasa ndio nikaamua kujichanganya kwenye kampuni ndio ikawa hivyo
 
Wadau habari zenu,

Wadau mimi nikijana (28) nilikuwa nafanya kazi kampuni fulani ila ikafika muda tukapunguzwa kazini, lakini pia nilikuwa nimesave kiasi cha kama laki 7 kwenye account yangu benki, ikumbukwe pia kipindi chote hicho sikuwa na hata pakuishi hata simu niliyokuwa natumia ilikuwa ya batani maana nilikuwa na katecno.

Ila katika harakati za kutafuta kazi basi ilibidi nikauze ili kupata nauli ya kufatilia michongo ya kazi, maana nilikuwa jobless tu kitaa na pia wazazi nao hawakuwa vizuri kiuchumi hivyo nilikuwa napiga tu mishe kwa kujitegemea.

Sasa baada yakupunguzwa kazini kutokana na ukata wa kampuni huku nikiwa na mawazo mengi kichwani nikafatilia pesa yangu benki huku nikijua ndio mwisho wa kazi. Nikasema wacha ninunue hata ka smartphone ka laki 2, ikabaki laki 5 ili zingine zinisaidie kwenye michongo yangu, hapa ndipo balaa lilipoanzia

Nikajikuta nimekuwa mlevi kupindukia ndani ya siku 5 kwenye account nikicheki salio ni elfu 10 tu ndio imebaki. Sijui pakuanzia tena na pesa imeisha, yaani nimetumia almost laki 5 kwa siku 5 duh! Hapa nilipo nimechanganyikiwa, kazi sina pesa zimeisha mpaka natamani kujimaliza tu maana mawazo tele kichwani.

Ndugu zangu, huku JF sijaingia muda nikasema mkinikosa jua nimeshafanya maamuzi magumu tu ya kujitoa uhai

NB: Sina uandishi mzuri na nimepaniki mno hapa nilipo maana mawazo hayaishi.
Nahisi hapa hata ukipewa ushauri unaweza ukaenda kulewea.
 
Kama una chakula ndani, jitahidi uwe una amka asubuhi unapika unakula kisha unalala tena.

Circle iwe hivi: Amka, Pika, kula, Lala

Fanya hivyo hivyo mpaka utakapo anza kuona badiliko kwenye kichwa chako.
Wakati unalala jitahidi kutokuwaza chochote ashumu kila kitu kipo sawa kabisa kama inavyopaswa kiwe, Kisha baada ya muda utaghairi kujiua mwenyewe.
 
Qualification zangu mkuu mimi nilisoma diploma chuo fulani(Public administration and management)na sikupata ajira kwa zaidi ya miaka 5 sasa ndio nikaamua kujichanganya kwenye kampuni ndio ikawa hivyo
Hapana, qualifications haziandikwi kwa style hii, hebu andika kama mtu ambaye yuko serious. Chuo gani, mwaka gani? Kibarua ulifanya kwenye department gani? Kwa muda gani? nadhani inasaidia kutoa picha fulani. Pasaka Njema
 
Huyo analeta masikhara, ni kwenda naye kimasikhara hivyohivyo
 
Back
Top Bottom