Natamani Friendly Fire JWTZ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani Friendly Fire JWTZ

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Oct 7, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Kuna baadhi ya wanajeshi ni wapuuzi. Hawana uzalendo na hawana huruma na umasikini wa Watanzania walio wengi.

  Kuna baadhi ya wanajeshi (nina amini ni wengi) ni wazalendo na wanaona uchungu sana kuishi maisha ya peponi na kuendesha Range Rover wakati mamilioni ya Watanzania wanatekete kwa umasikini kwa sababu ya wanasiasa mafisadi na wala rushwa.

  Siku ya siku hawa jamaa watazichapa, upande mmoja ukijifanya kibarakwa kwa watawala, na upande mwingine ukifanya kazi yake - kulinda wananchi. Natamani sana hiyo siku ifike. Pengine ipo karibu.

  Hatimaye TBC1 ataonekana 'soja' akisoma taarifa ya habari.

  Mimi nitakuwa nakula gahawa tu na baby kitaa.

  JWTZ si ya Chadema wala CCM.

  Mlimg'oa nduli Idd Amini. Ni wakati wa kuung'oa utawala wa rushwa. Tunaomba mtulinde tuwang'oe mafisadi bila kumwaga damu.
   
 2. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,253
  Trophy Points: 280
  Kurara bure kuva bure waone uchungu wanini??
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,506
  Trophy Points: 280
  Kwa taarifa yako JWTZ limegawanyika maofisa wa ngazi ya juu wapo beneti na CCM kwa sababu wananufaika na ufisadi. Maafisa wa ngazi za chini ambao wanaathirika na ufisadi wa CCM wako beennti na Chadema. Huo ndiyo ukweli uliopo.
   
 4. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Nilibahatika kupitia JKT, nakwambia wanaofaidi ni maofisa tu, Kuanzia cheo cha Meja kwenda mbele, hawa wengine ni shida mtindo mmoja. kwa hiyo wanaokula kuku hasa ni wenye vitengo lakini walio man power ni mshahar kwa mshahara.

  Kwa hiyo usifikiri Jeshi nzima lipo na starehe, wengi wao ni matatizo na wanapenda sana mageuzi yatokee lakini ukiwa jeshini mzee umeapa na kuapa huwezi kusaliti kiapo chako hadi kifo. na chochote anachokwambia aliyekuzidi cheo ndicho hicho unafuata hakuna kuuliza why? how?

  Jibu ni "NDIYO AFANDE". Kwa hiyo usitegemee kauli yoyote toka kwa Jeshi kuhusu issue iliyotokea juzi - NEVER - Anayeweza toka kauli ni anayemzidi cheo - na yupo mmoja tu kama sikosei then Rais mwenyewe.

  Na hawa wakubwa wapo damu damu na watawala kumbuka JESHI pia lina riporti moja kwa moja IKULU.

  Sasa nafikiri unaona njisi vikwazo vilivyo vingi hapo, yaani safari ni ndefu ila hakuna kukata tamaa kama umma umeamua chochote kitafanyika - hatutaki mambo ya Zimbabwe ama Kenya, atakayeshindwa na aachie madaraka kwa amani na mshikamano.
   
 5. M

  Magezi JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mapinduzi ya kweli yataletwa na wapiganaji tu
   
 6. T

  Tata JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Hili ni tatizo la jeshi kukosa shughuli za kufanya mpaka wanatamani kuingilia kazi za polisi. Mimi naona Gen. Shimbo angejenga hoja wanajeshi wakapambane na Al-Shabaab Somalia ili wawe bize kidogo.
   
Loading...