Natamani dada yangu angekuwa ndio mke wangu

Natamani dada yangu angekuwa ndio mke wangu

Nimeoa mwanamke kimeo hatari,changamoto ninazozipitia kwenye ndoa yangu naamini hata shetani ananionea huruma.Nimemtembelea dada yangu nina wiki Sasa nipo hapa kwao,yeye na mumewe na watoto wao watatu,maisha ninayoyaona hapa daaaa najiona nina mkosi hawa watu wanaishi kwa upendo wa hali ya juu sana,na nilichogundua dada yangu anamheshimu na kumjali sana mumewe,na shemeji pia anampenda sana mkewe,

Shemeji ni mfanyabiashara mdogo mdogo na dada ni mtumishi serikalini,baada ya mumewe kuyumba kibiashara dada yangu ikabidi akavute mkopo benki(haya nimeambiwa na mdogo wake shemeji) dada yangu anakatwa mshahara,na dada yangu kila akitoa msaada wowote kwa wazazi kamwe hajawahi kusema Msaada katoa yeye ila mume wake,yote haya nimeyajua baada ya kufika hapa,

Je karne hii wangapi mnawafanyia haya waume zenu? Wangapi mnafanyiwa haya na wake zenu?mke anakujengea heshima kwao heshima ambayo alistahili yeye anakupa wewe mumewe,ndio maana nimejikuta ghafla nimetamani dada angekuwa ndio mke wangu,maana mke wangu mimi ni bingwa wa kunivunjia heshima kwao nk,mliooa wanawake wa namna hii hongereni Sana ,Wenzangu na mimi poleni ,tupambane na hali zetu.

Huyu mkeo yupo sahihi!

Yaelekea wewe ni tatizo mno zaidi ya hata unvyoandika hapa!

Yaani mtu mwenye mke na watoto na mji wake unaenda kukaa kwa dada yako alieolewa na mwanaume mwengine ili iweje?
 
Huyu mkeo yupo sahihi!

Yaelekea wewe ni tatizo mno zaidi ya hata unvyoandika hapa!

Yaani mtu mwenye mke na watoto na mji wake unaenda kukaa kwa dada yako alieolewa na mwanaume mwengine ili iweje?
Unaposema dada aliyeolewa na mwanaume mwingine unamaanisha nini?tuanzie hapo
 
By the way yeye katamani tabia ya utii na heshima aliyonayo dada yake kwa mumewe hivyo anaona kama kwa mkewe kunapungua vitu vingi kiasi cha kujuta rohoni mwake. Lakini ndugu mtoa hoja lazima utambue hili, mwamke kumfanya aishi utakavyo yahitaji muda wakutosha na si ubabe uta fail.
Miaka mitano sasa mkuu
 
Hawa wanawake wanaolelewa shule za boarding unategemea watakuwa wake wa kueleweka?
Yeye anachodhani kuwa mke ni kuoffer sex tu!
 
Mkeo anakuvunjiaje Heshima kwao??? Wewe unajua huyo shemeji yako pamoja na kidgo anachopata huwa anatoa sh ngapi kusaidia kwa mkeo??? Ndoa za watu ndugu ona tu watu wanaishi kwa raha sijui wanasaidiana Hela ya Mwanamke haitoki bila Manyanyaso na mateso pamoja na masimango wewe unaweza hisi Dada ko hamfanyii hayo shemeji yako ila ukweli ni kuw shemeji yako amemaua kuwa mvumilivu maana ni hali ambayo anajua ni ya mpito..!! Nae siku akichoka utajua ukweli wote.
 
Hawa wanawake wanaolelewa shule za boarding unategemea watakuwa wake wa kueleweka?
Yeye anachodhani kuwa mke ni kuoffer sex tu!
Wengi wanaangalia Matacco aisee ndoa sio mchezo walahi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Mkeo anakuvunjiaje Heshima kwao??? Wewe unajua huyo shemeji yako pamoja na kidgo anachopata huwa anatoa sh ngapi kusaidia kwa mkeo??? Ndoa za watu ndugu ona tu watu wanaishi kwa raha sijui wanasaidiana Hela ya Mwanamke haitoki bila Manyanyaso na mateso pamoja na masimango wewe unaweza hisi Dada ko hamfanyii hayo shemeji yako ila ukweli ni kuw shemeji yako amemaua kuwa mvumilivu maana ni hali ambayo anajua ni ya mpito..!! Nae siku akichoka utajua ukweli wote.
Sifa zote nimezisikia kutoka kwa mdogo wake shemeji yangu,pamoja na yote changamoto katika ndoa yoyote hazikosekani
 
Sifa zote nimezisikia kutoka kwa mdogo wake shemeji yangu,pamoja na yote changamoto katika ndoa yoyote hazikosekani
Mdogo wake??? Nkajua shemeji mwenyewe[emoji23][emoji23][emoji23] haya mkuu sema usitamani kiatu cha mwenzio ukikivaa unaweza usitembee kabisa
 
Back
Top Bottom