Natamani dada yangu angekuwa ndio mke wangu

Jabakeke

JF-Expert Member
Apr 18, 2019
386
355
Nimeoa mwanamke kimeo hatari,changamoto ninazozipitia kwenye ndoa yangu naamini hata shetani ananionea huruma.Nimemtembelea dada yangu nina wiki Sasa nipo hapa kwao,yeye na mumewe na watoto wao watatu,maisha ninayoyaona hapa daaaa najiona nina mkosi hawa watu wanaishi kwa upendo wa hali ya juu sana,na nilichogundua dada yangu anamheshimu na kumjali sana mumewe,na shemeji pia anampenda sana mkewe,

Shemeji ni mfanyabiashara mdogo mdogo na dada ni mtumishi serikalini,baada ya mumewe kuyumba kibiashara dada yangu ikabidi akavute mkopo benki(haya nimeambiwa na mdogo wake shemeji) dada yangu anakatwa mshahara,na dada yangu kila akitoa msaada wowote kwa wazazi kamwe hajawahi kusema Msaada katoa yeye ila mume wake,yote haya nimeyajua baada ya kufika hapa,

Je karne hii wangapi mnawafanyia haya waume zenu? Wangapi mnafanyiwa haya na wake zenu?mke anakujengea heshima kwao heshima ambayo alistahili yeye anakupa wewe mumewe,ndio maana nimejikuta ghafla nimetamani dada angekuwa ndio mke wangu,maana mke wangu mimi ni bingwa wa kunivunjia heshima kwao nk,mliooa wanawake wa namna hii hongereni Sana ,Wenzangu na mimi poleni ,tupambane na hali zetu.
 
Pole mweshimiwa,ni kawaida sana kutamani mkeo awe kama ndugu zako hii ni kwa sababu ndiyo uliowazoea. Kila mwanamume anatamani mke kama mama yake kwani ndiyo mwanamke bora uliyemjua kwanza.
Huwa haiwezekani lakini. Hivyo jaribu kumuelekeza huyo uliyenaye ili awe vile unavyotaka. Unahitajika hekima sana lakini inawezekana...kuwa mvumilivu pia.
 
Nimeoa mwanamke kimeo hatari,changamoto ninazozipitia kwenye ndoa yangu naamini hata shetani ananionea huruma.
Nimemtembelea dada yangu nina wiki Sasa nipo hapa kwao,yeye na mumewe na watoto wao watatu,maisha ninayoyaona hapa daaaa najiona nina mkosi hawa watu wanaishi kwa upendo wa hali ya juu sana,na nilichogundua dada yangu anamheshimu na kumjali sana mumewe,na shemeji pia anampenda sana mkewe,
Shemeji ni mfanyabiashara mdogo mdogo na dada ni mtumishi serikalini,baada ya mumewe kuyumba kibiashara dada yangu ikabidi akavute mkopo benki(haya nimeambiwa na mdogo wake shemeji) dada yangu anakatwa mshahara,na dada yangu kila akitoa msaada wowote kwa wazazi kamwe hajawahi kusema Msaada katoa yeye ila mume wake,yote haya nimeyajua baada ya kufika hapa,je karne hii wangapi mnawafanyia haya waume zenu? Wangapi mnafanyiwa haya na wake zenu?mke anakujengea heshima kwao heshima ambayo alistahili yeye anakupa wewe mumewe,ndio maana nimejikuta ghafla nimetamani dada angekuwa ndio mke wangu,maana mke wangu mimi ni bingwa wa kunivunjia heshima kwao nk,mliooa wanawake wa namna hii hongereni Sana ,Wenzangu na mimi poleni ,tupambane na hali zetu.
Asante kwa taarifa,, ngoja tuwe makini ktk kusaka jiko
 
Umemtamani hadi dada yako angekua mkeo we kweli hamnazo, sema nini usije ukaanza kukorofisha ndoa ya dada yako maana kuna kila dalili ...unamuonea wivu shemeji yako kupewa pesa kesho utamwambia dada yako achana na huyu jamaa ...na matatizo ya ndugu huwa ni moja tu wakija kukutembelea huwa kazi yao ni kutibua tu
 
Si uachane tu na Hugo mke wako.
by the way picha ya Dada basi kama hutojali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom