Natamani dada yangu angekuwa ndio mke wangu

Natamani dada yangu angekuwa ndio mke wangu

POLE SANA MKUU ILA HUWEZI JUA KILICHO NYUMA YA PAZIA...
Mara nyingi watu huwa wanaficha mabaya mbele ya wageni wao
Kama shemeji yake dada yangu anamsifia shemejiye nadhani wako vizuri
 
Usione vya elea vimeundwa. Embu jichunguze madhaifu yako ujirekebishe ndio uje kwa mkeo halafu mfanye jinsi unavyotaka muishi
Hakuna asiyekuwa na madhaifu ila tumezidiana viwango,mwenzangu kanizidi mbali sana nilishajichunguza
 
Mtoa mada katamani tabia nzuri na mtindo wa maisha kiujumla anayoishi Dada yake na Mumewe wala si kumpindua shemeji yake.
Sio kweli hiyo. Inaonesha walikuwaga na kamchezo flan zamani kabla dada hajaolewa, Ndo maana akakurupuka kumpata mwenzi bila uchunguzi wa kina.
Ushauri;
Aondoke kwa dadake haraka kabla shem hajamgundua
 
watu ni mazumbukuku mnajua kumtamani vipi
Mnakazia incest kwa mtoa Mada.. Mna uelewa finyu


Blood great sinker mazafanta fakeni shiti asshole
Hahaa mlevi mmoja tayari ushabwia mitungi nini, hizo mazafanta vipi[emoji3] [emoji3] ,mambo lakini mlevi sugu 1!
 
Nimeoa mwanamke kimeo hatari,changamoto ninazozipitia kwenye ndoa yangu naamini hata shetani ananionea huruma.Nimemtembelea dada yangu nina wiki Sasa nipo hapa kwao,yeye na mumewe na watoto wao watatu,maisha ninayoyaona hapa daaaa najiona nina mkosi hawa watu wanaishi kwa upendo wa hali ya juu sana,na nilichogundua dada yangu anamheshimu na kumjali sana mumewe,na shemeji pia anampenda sana mkewe,

Shemeji ni mfanyabiashara mdogo mdogo na dada ni mtumishi serikalini,baada ya mumewe kuyumba kibiashara dada yangu ikabidi akavute mkopo benki(haya nimeambiwa na mdogo wake shemeji) dada yangu anakatwa mshahara,na dada yangu kila akitoa msaada wowote kwa wazazi kamwe hajawahi kusema Msaada katoa yeye ila mume wake,yote haya nimeyajua baada ya kufika hapa,

Je karne hii wangapi mnawafanyia haya waume zenu? Wangapi mnafanyiwa haya na wake zenu?mke anakujengea heshima kwao heshima ambayo alistahili yeye anakupa wewe mumewe,ndio maana nimejikuta ghafla nimetamani dada angekuwa ndio mke wangu,maana mke wangu mimi ni bingwa wa kunivunjia heshima kwao nk,mliooa wanawake wa namna hii hongereni Sana ,Wenzangu na mimi poleni ,tupambane na hali zetu.
Hujachelelewa,mrudishie bwashee mahari yake kisha umpose dada yako na umuoe!
 
Nna kisa kimoja kuna Dada my workment aliniomba nikamchukue kakaake anaumwa sana, kweli jamaa alikuwa kazidiwa sana hata kwenye gari kukaa hakuweza ilibidi nimlaze tu, nafikanae hospitali mkewe alikuwepo nakumbuka simu ya jamaa ikaita ile jamaa anajikokota kuongea na simu yule mwanamke alimnyang'anya na kumporomoshea maneno ya hovyo sana kiufupi jamaa alinyanyapaliwa sana na mkewe tena mbele yangu, ghafla dadaake alifika pale treatment aliopewa mgonjwa ni nzuri hata uso wa mgonjwa ulianza kuleta matumaini, nikajiuliza moyoni mwake anajutia kiasi gani kuwa na mwanamke aliena!!
Boss ndo maana kwanza nasemaje, ..kuoa nitaoa mwanamke sio kazi yake wala shepu wala sura wala elimu.


LAZIMA ANIKUTE na kwangu..


Siku akileta mbwembwe za kijinga jinga , anasepa yeye na mizigo yake .



TUOE WANAWAKE WENYE DINI NDANI YAO, WANAWAKE WENYE HOFU NA MUNGU.

DINI INSTAHARABISHA MWANADAMU
 
Mtoa mada katamani tabia nzuri na mtindo wa maisha kiujumla anayoishi Dada yake na Mumewe wala si kumpindua shemeji yake.
Watu tunatofautiana kuelewa, hata kusoma, sijui kwa nii? Bora ulivyoliweka vzr
Maudhui ya mada ni tofauti anayoiona kati ya familia yake na maisha ya familia ya dada yake yaani yeye anaona ni kama paradizo na kuzimu kwa hiyo yeye ameitamani paradizo yao tofauti na wengine walivyoelewa kwamba jamaa amemtamani dada yake
 
Mwenye nguvu sio dada yako ni huyo mume wako.
Nadhani umenielewa.

Acha hizi dhambi
Acha kutamani mke wa mtu
Acha kutamani kulala na umbu lako
Katamani TABIA sio MTU..

Mtu akikwambia "NATAMANI KUISHI MAREKANI"
Hamaanishi AHAME NCHI ila ANAHITAJI KUISHI MAZINGIRA YA UCHUMI YALIYO SAWA NA MAREKANI.

LUGHA YA FALSAFA

#ASANTE
#YNWA
 
Duh! Mbona sielewi namna ya kumtamani dadaako wa kuzaliwa! By the way, wiki nzima umejivundika alikoolewa dadaako, we mwanaume wa wapi wewe? Yamkini ni hizi tabia zako ndio zinamkera mkeo...toka hapo rudi nyumbani kwako
Katamani TABIA sio MTU..

Mtu akikwambia "NATAMANI KUISHI MAREKANI"
Hamaanishi AHAME NCHI ila ANAHITAJI KUISHI MAZINGIRA YA UCHUMI YALIYO SAWA NA MAREKANI.

LUGHA YA FALSAFA

#ASANTE
#YNWA
 
Katamani TABIA sio MTU..

Mtu akikwambia "NATAMANI KUISHI MAREKANI"
Hamaanishi AHAME NCHI ila ANAHITAJI KUISHI MAZINGIRA YA UCHUMI YALIYO SAWA NA MAREKANI.

LUGHA YA FALSAFA

#ASANTE
#YNWA
Kutamani mtu awe mke wako maana yake nini? Tukubaliane tu kuwa bango lake lina utata. Inawezekana hakuwa na nia hiyo ambayo sisi tunafikiria lkn lugha aliyotumia imefanya tuwaze huko.
 
Back
Top Bottom