Nataka Rais Magufuli ashindwe

Status
Not open for further replies.
Mmh, ushindwe weye usitake kutuchochea kama kuni alafu wee uote moto sie wengne hatuna milion 10 ya dhaman sembuse ya kuweka wakili
 
Nope.

Msimamo bado uko palepale.

Ikija kwenye demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa watu kujieleza, bado nataka Magufuli ashindwe kama nia na malengo yake ni kuviminya.

Lakini sitegemei uelewe nilichokiandika hapo....
What a coincidence!
Sitegemei utanielewa. Tukubaliane tu kwa hilo Mkuu
 
 
Mtamwelewa tu...Lisu mwenyewe anamwogopa....press conference zake zinajieleza..huwa anstutuma anayo ongea tumwambie Rais...
Mshindwe na mlegee magufuli viva
 
NN ulichokipost wakati huo ulikuwa unamaanisha nini? na sasa ni nini kimebadilika?
Nilikuwa namaanisha aache watu wawe huru.

Hakuna sababu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa. Hakuna sababu ya kuwakamata na kuwanyanyasa wapinzani. Hakuna sababu ya kuvifungia vyombo vya habari na kuwanyanyasa wamiliki wake.

Kwenye hayo nataka ashindwe.

Hata kwenye kupiga marufuku wanafunzi wa kike wanaopata mimba kurudi mashuleni nataka ashindwe.

Kumtaka ashindwe kwenye hayo haimaanishi namtaka ashindwe kwenye kuinyoosha nchi hususan kwenye ufisadi na kuleta nidhamu kwenye ofisi za serikali.

Ndo maana nikiona kapatia kwenye jambo fulani nampongeza. Nikiona kakosea, nampinga.

Kigumu kuelewa hapo ni kipi?
 
Pole.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…