Nataka niende Moshi na Boxer X150 nipeni ushauri wakuu

kiukweli barabara kubwa za kutoboa mikoani huwa sina mazoea nazo kabisaaa!!! eti niingie lami na pikipki nitembee zaidi ya km 100? Aisee kuna maFuso, malori na mabasi huwa yana fujo mbovu sana, hayathamini waenda kwa miguu, waendesha baiskeli na pikipiki.....

Be careful its too risk jombaa.....
Kingine boxer ni nyepesi mno labda utembelee spidi chini ya 90km/hr
ungekuwa na XL, XRL, BMW, na sport bikes.
 
Kaka utaikaanga..trust me mwenye Sanlg mchina anatoboa lakini hizi boxer za siku hizi majanga! itamwaga moshi hutaamini..zinakufa sana ring piston..i stand to be corrected!
Unaweza ukawa sahihi mkuu maana siku nyingi sijaendesha pikipiki tangu katikati ya 2008, pikipiki haina rejeta hivyo ikiendeshwa kwa muda mrefu kuna uwezekano wa injini kupata moto na hata block kutanuka (sijui hizi za sasa maana wengine tulitumia XL na Yamaha DT those days na zilikuwa imara kabla ya pikipiki za sasa kushika kasi)...labda kama ataendesha kila baada ya kilometre 150 anapumzika nusu saa alafu anaendelea pia asiendeshee sifa ya speed kali maana sidhani hata kama hizo kilometa 150 atazifikia
 
Ondoka saa 11 alfajiri na kila baada ya km 200 pumzika vua koti kbs ili mwili upumue kdg na kupunguza tension. Uwe makini sana na magari yanayoovertake kutikea upande unaokwenda na ndio risk ya sisi waendesha pkpk safari ndefu. Wao wanakuja tu wakijua ww ndio utahama kwenda pembeni. Muda wote kama hakuna kijiji au magari mengi tembea 100km/h au 90km/h. Hakikisha una helmet nzuri, koti zuri lisiloingiza upepo na pia cover la kifuani. Utaenjoy sana ila kama ni mara yakwanza safari ndefu utachoka sana kiuno na mikono.
 
Nenda Jombaa utafika salama kabisa,ila usiwe na haraka hata kidogo usizidi speed 80 na ukifika korongwe pumzika masaa mawili chombao kipoa kabisa kama vile ndio unaanza safari kua makini sana na malori na mabasi ni hatari sana sana....ukizingatia hayo hakika utafika....ila anza safari saa kumi alfajiri.
Nakutakia safari njema tukutane x-mass
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom